Next
Previous
Showing posts with label Yanga SC. Show all posts

Thursday, December 19, 2013

0

KLABU YA DAR YOUNG AFRICANS, YAINGIA MKATABA MNONO

Posted in
yanga-logo
Klabu ya mpira wa miguu kutoka Jangwani Young Africans maarufu kama Yanga, imeingia mkataba na  SGM ya Ufaransa kwa ajili ya kurusha mchezo wake wa hatua ya kwanza ya mashindano ya klabu Bingwa Afrika dhidi ya timu ya Alh Ahly ya Misri kwa gharama ya dola za kimarekani elfu 55,000 sawa na mil 90/= za kitanzania kwa muda wa dakika 90.


Katibu Mkuu wa  Young Africans Bw. Beno Njovu amesema wameingia mkataba huo na kampuni ya SGM kutoka nchini Ufaransa ambapo kampuni hiyo wameipa uwakala kampuni ya MGB ya Zamaleki ya Cairo kama wawakilishi wa kampuni hiyo ya SGM.
Mkataba huo unawapa kibali kampuni ya SGM kurusha moja kwa moja (Live) michezo yote ya Yanga ya Klabu Bingwa Africa ukiwamo mchezo dhidi ya Al Ahly utakaofanyika Tanzania na marudiano kufanyikia nchini Misri. Yanga itaanza michuano hiyo ya Klabu Bingwa Africa kwa kukipiga dhidi ya timu ya Komoronize ya Visiwa vya Comoro Februari 8 mwakani katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kabla ya kurudiana nao wiki baadae nchini kwao Comoro na kama Yanga itafanikiwa kuvuka hatua hiyo ndio itakutana na Al Ahly Februari 28.

Thursday, August 15, 2013

0

NI YANGA VS AZAM WEEKEND HII | NGAO YA JAMII - MATCH REPORT

Posted in ,

Bingwa mtetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom, Yanga na makamu bingwa Azam wanavaana keshokutwa (Jumamosi) kwenye mechi ya Ngao ya Jamii (Community Shield) kuashiria uzinduzi wa msimu mpya wa ligi kuu 2013/2014.

Mechi hiyo inayotarajiwa kuwa kivutio kwa wapenzi wa mpira wa miguu nchini itachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10.30 jioni ambapo mshindi atakabidhiwa ngao.

Iwapo dakika 90 za mechi hiyo hazitatoa mshindi, timu hizo zitatenganishwa kwa mikwaju ya penalti huku asilimia 10 ya mapato ya mechi hiyo yakienda kwa kituo cha kulelea watoto cha SOS.

Sunday, May 19, 2013

0

NYIMBO SPECIAL KWA MASHABIKI WA YANGA

Posted in

Thursday, May 16, 2013

0

KOCHA MKUU TAIFA STARS ATAJA KIKOSI CHA KUIVAA MOROCCO | TIKETI ZA MECHI YA SIMBA NA YANGA ZAANZA UZWA

Posted in , , ,
Na Soka In Bongo
TAIFA_STARS-FRAMED>> TANZANIA YAJITOA MICHUANO YA COSAFA
>> TIKETI SIMBA, YANGA KUANZA KUUZWA KESHO
>>TIKETI NI KUANZIA SH. 5,000 HADI 30,000
PATA HABARI KAMILI:






Release No. 084
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mei 16, 2013
KIM ATAJA 26 STARS WA KUIVAA MOROCCO
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen leo (Mei 16 mwaka huu) ametaja kikosi cha wachezaji 26 watakaoingia kambini kujiwinda kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco itakayochezwa Juni 8 mwaka huu jijini Marrakech, Morocco.
Katika kikosi hicho, Kim ameita wachezaji wapya sita ingawa baadhi yao wamewahi kuchezea timu hiyo, huku akiacha wengine watatu aliokuwa nao kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Morocco ambapo Taifa Stars ilishinda mabao 3-1.
Wapya aliowaita katika kikosi hicho kitakachoingia kambini Mei 20 mwaka huu, saa 1 jioni kwenye hoteli ya Tansoma jijini Dar es Salaam ni Ally Mustafa, Vicent Barnabas, Juma Luzio, Haruna Chanongo, Mudhathiri Yahya na Zahoro Pazi. Wachezaji aliowaacha ni Shabani Nditi, Nassoro Masoud Cholo na Issa Rashid.
Kikosi kamili cha Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ambacho kabla ya kwenda Morocco kitapita jijini Addis Ababa, Ethiopia kucheza mechi ya kirafiki Juni 2 mwaka huu dhidi ya Sudan ni kama ifuatavyo;
Makipa ni nahodha Juma Kaseja (Simba), Aishi Manula (Azam), Ally Mustafa (Yanga) na Mwadini Ally (Azam). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Shomari Kapombe (Simba), Vicent Barnabas (Mtibwa Sugar) na Waziri Salum (Azam).
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Khamis Mcha (Azam), Mwinyi Kazimoto (Simba), Mudathiri Yahya (Azam) na Salum Abubakar

Wednesday, May 15, 2013

0

HIVI NDIVYO JINSI UWANJA WA KLABU YA YANGA UTAKAVYOKUWA

Posted in

Klabu ya mpira wa miguu ya YANGA SC inatarajia kuwa na UWANJA wake binafsi ... UWANJA huo wa kisasa kabisa unatarajia kuanza ujenzi wake mapema mwezi ujao chini ya kampuni ya BEIJING CONSTRUCTION ENGINEERING GROUP ...
Klabu hiyo pia inatarajia kusaini mkataba mwisho wa mwezi huu kuashiria kuanza kwa ujenzi wa UWANJA huo ...

Saturday, May 11, 2013

0

KLABU YA SIMBA NA MASHABIKI WAO WAJIPANGA KUTIBUA RAHA YA KUSHANGILIA UBINGWA KWA YANGA

Posted in ,

Mashabiki wa klabu ya Simba wamesema wanaimani na chipukizi wao kuwa watawafunga Yanga katika mchezo wa mwisho wa ligi kuu Tanzania bara utakaofanyika tarehe 18 mwezi Mei. Mashabiki hao wamesema wanauhakika na ushindi dhidi ya Yanga, kwani nia yao ni kuondoa utamu wa kutwaa kombe la ligi kwa vile wanajua siku ya tarehe 18 baada ya mechi ndipo Yanga atakabidhiwa kombe hivyo kama Yanga atafungwa na Simba kwenye huo mchezo basi raha ya kushangilia itakuwa imeingia dosari, lakini mchezaji wa zamani wa Simba Zamoyoni Mogella amesema chipukizi hao wa Simba wataweza kufanya maajabu hayo kama wataweza kutumia vyema kipindi cha kwanza ili wajipatie magoli ya kutosha mapema bila kuchelewa hadi kipindi cha pili ambapo huwa wanachoka na kuwapa mwanya wapinzani wao. Simba inayoshikilia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kwasasa imeamua kuwapa nafasi chipukizi wake kuonesha uwezo wao lakini vilevile kuwajenga ili waje kuchukua nafasi kwenye kikosi cha kwanza, chipukizi hao wamekuwa wakicheza mechi kadhaa za mwisho wa ligi na wanatarajiwa kushuka dimbani tarehe 18 dhidi ya Yanga. 

Wednesday, May 8, 2013

0

YANGA KUKABIDHIWA KOMBE KATIKA MECHI DHIDI YA SIMBA

Posted in , ,

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) litakabidhi kombe kwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, Yanga katika mechi yao ya mwisho ya ligi hiyo dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Simba kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Mei 18.

Akizungumza na NIPASHE jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi ya TFF, Wallace Karia alisema kuwa wataikabidhi Yanga kombe hilo baada ya kumalizika kwa mechi hiyo ya kufunga msimu wa 2012/13 wa ligi.

Sunday, April 21, 2013

0

NA SOKA IN BONGO: VPL-YANGA 3 JKT RUVU 0, YANGA BADO POINTI 1 BINGWA!!

Posted in , ,
>>YANGA BADO COASTAL, SIMBA!!
>>LAKINI, AZAM AKIFUNGWA NA COASTAL JUMAMOSI IJAYO, YANGA BINGWA!!
Vinara wa VPL, Ligi Kuu Vodacom, Yanga leo wameipiga JKT Ruvi Bao 3-0 na kujiweka nafasi nzuri ya kutwaa Ubingwa kwa kuhitaji Pointi 1 tu kati ya Mechi 2 walizobakisha bila ya kujali matokeo yeyote ya Timu ya Pili Azam FC.
+++++++++++
MAGOLI:
Yanga 3
-Simon Msuva Dakika ya 45
-Hamis Kiiza 59
-Nizar Khalfan 65
JIK Ruvu 0
+++++++++++
Yanga sasa imefikisha pointi 56 wakifuatiwa na Azam FC wenye Pointi 47 na waliobakisha Mechi 3.
++++++++++++++++++++++++++++
MECHI WALIZOBAKISHA YANGA:
Mei 1: COASTAL v YANGA YANGA [MKWAKWANI]
Mei 18: YANGA v SIMBA [UWANJA wa TAIFA]

Saturday, October 27, 2012

0

YALIYOJIRI LIGI KUU TANZANIA BARA NA RATIBA YA MECHI ZIJAZO:: NA WENZETU SOKA IN BONGO

Posted in , , , ,

VPL: Simba yaipiga Azam, Yanga yaipiku Azam nafasi ya 2!!

Jumamosi, 27 Oktoba 2012 20:14
Chapisha Toleo la kuchapisha
VPL_LOGOKatika mfululizo wa Mechi za Ligi Kuu Vodacom, VPL, zilizochezwa leo, Mabingwa watetezi Simba wamefanikiwa kuichapa Azam bao 3-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuendelea kubaki kwenye uongozi huku Yanga, wakiwa huko Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha wakiifunga JKT Oljoro bao 1-0 na kuipokonya Azam nafasi ya Pili kwenye Msimamo wa Ligi.
++++++++++++++++++++++++++
MATOKEO/RATIBA:
Oktoba 27
Simba 3 Azam 1
JKT Oljoro 0 Yanga 1
African Lyon v Kagera Sugar
Mgambo JKT v Tanzania Prisons
Ruvu Shootings v Polisi Morogoro
++++++++++++++++++++++++++
Bao la ushindi la Yanga lilifungwa na Mbuyu Twite katika Dakika ya 53.
Katika Mechi ya Simba na Azam, John Bocco ndie alietangulia kuifungia Azam bao moja katika Dakika ya 5 lakini Simba ikazinduka na kupiga Bao 3 kupitia Felix Sunzu, Dakika ya 7, na bao mbili za Emmanuel Okwi.
++++++++++++++++++++++++++

Saturday, October 6, 2012

0

MPYA ZA LEO KUTOKA TFF, Na Wenzetu SOKA-IN-BONGO

Posted in , , , , , ,
>> YANGA, AFRICAN LYON KUTOVAA BEJI YA MDHAMINI!
>> WAAMUZI WATATU WAONDOLEWA, SIMBA YAPIGWA FAINI!
>> MECHI YA KAGERA SUGAR, YANGA YASOGEZWA!
>> LIGI DARAJA LA KWANZA KUANZA OKTOBA 20!

LIGI DARAJA LA KWANZA KUANZA OKTOBA 20
Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilikutana jana (Oktoba 5 mwaka huu) kupitia na kufanya uamuzi katika masuala mbalimbali na kupanga Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ianze kutimua vumbi Oktoba 20 mwaka huu.
TFF_LOGO12Timu zimepangwa katika makundi matatu ya timu nane nane ambapo zitacheza ligi hiyo kwa mtindo wa nyumbani na ugenini. Mshindi wa kila kundi ndiye atakayepata tiketi ya kucheza Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao wakati timu ya mwisho kila kundi itashuka daraja kurudi Ligi ya Mkoa.
Kundi A lina timu za Burkina Moro ya Morogoro, Kurugenzi Mufindi ya Iringa, Majimaji ya Songea, Mbeya City ya Mbeya, Mlale JKT ya Ruvuma, Mkamba Rangers ya Morogoro, Polisi Iringa na Small Kids ya Rukwa.
Ndanda FC ya Mtwara, Ashanti United, Green Warriors, Moro United, Polisi, Tessema, Transit Camp na Villa Squad zote za Dar es Salaam ndizo zinazounda kundi B wakati kundi C ni Kanembwa JKT ya Kigoma, Morani ya Manyara, Mwadui ya Shinyanga, Pamba ya Mwanza Polisi Dodoma, Polisi Mara, Polisi Tabora na Rhino Rangers ya Tabora.
Ada ya ushiriki wa ligi ni sh. 200,000 zinazotakiwa kulipwa kabla ya Oktoba 13 mwaka huu. Pia Oktoba 13 mwaka huu kutakuwa na kikao kati ya wenyeviti wa klabu zote zinazoshiriki ligi hiyo na Kamati ya Ligi ambapo pia itafanyika draw (ratiba).

Wednesday, October 3, 2012

0

MECHI YA WATANI WA JADI YAMALIZIKA KWA SULUHU.

Posted in , , , ,
Simba Na Yanga
Ni magoli ya Bahanuzi na Kiemba yaliyofanya mechi hii ya watani hawa irembwe kwa sare ya bao moja kwa moja. Amri Kiemba aliipatia timu yake ya Simba bao la kwanza katika dakika ya 5, huku Kijana toka Sengerema Saidi Bahanuzi akisawazisha bao hilo katika kipindi cha pili mnamo dakika ya 65, kwa njia ya mkwaju wa penati baada ya mchezaji wa Simba kuunawa Mpira.
Katika mchezo huo mchezaji wa Yanga alizawadiwa Kadi nyekundu mnamo mwishoni mwa mechi, Huku Juma Kasseja akionesha umahiri wake kwa kuokoa Michomo mbalimbali.

Wednesday, August 1, 2012

0

Mrisho Ngassa Asababisha Kocha wa Azam kutimuliwa

Posted in , , , ,

STEWART Hall, kocha Muingereza wa Azam FC jana amefukuzwa rasmi katika klabu hiyo kwa kosa la kukaidi maagizo ya Bodi ya Ukurugenzi ya klabu hiyo, kumpanga Mrisho Khalfan Ngassa katika mechi ya fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame. Habari ambazo BIN ZUBEIRY imezipata kutoka ndani ya Azam, zimesema kwamba kikao cha jana cha pamoja baina ya Bodi ya Ukurugenzi ya Azam FC, Mwanasheria wa kampuni na kocha
Stewart kimeafiki kuvunj ndoa hiyo na sasa Azam FC itakuwa chini ya kocha
kutoka India, Vivek Nagul ambaye alikuwa anafundisha timu ya vijana.
Habari zinasema kwamba mapema baada ya mechi ya Nusu Fainali ya Kagame, kati ya Azam na AS Vita ya DRC, Stewart aliitwa na kuambiwa asimtumie tena Ngassa kwa kitendo cha mchezaji huyo kwenda kuibusu na kuivaa jezi ya Yanga, baada ya kufunga bao la ushindi.
Lakini Stewart katika kikao hicho, kwanza alimtetea Ngassa kutokana na
kufunga bao la ushindi na\ kumuelezea kama mchezaji
muhimu kwake, lakini msimamo wa bodi ulikuwa
ni asipangwe tena. Katika fainali, Stewart
alimvalisha jezi Ngassa akamuanzishia benchi, lakini
kama ilivyokuwa kwenye Nusu Fainali alimuingiza
kipindi cha pili timu ikiwa nyuma kwa 1-0 na mwisho
wa mchezo ikashinda 2-2 yeye akifunga la pili, dhidi
ya Yanga pia alimuingiza timu ikiwa nyuma kwa 1-0.
Lakini Ngassa alishindwakurudia kile alichofanya kwenye mechi na AS Vita na
Yanga ikashinda 2-0. Kwa sasa mazungumzo
yanaendelea kati ya Yanga na Azam juu ya Ngassa ili
mchezaji huyo arejee Jangwani, lakini wakati huo
huo, Simba nao wameweka dau la Sh. Milioni 25 katika
50 zinazotakiwa na Azam ili kumuuza mchezaji huyo.
Mbali na Ngassa, kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’
pia yuko katika wakati mgumu na jana inadaiwa
alionekana akilia wakati anazungumza na kiongozi
mmoja wa Azam, akiuliza ni lipi kosa lake.
Sure Boy, ambaye ni mtoto wa kocha wa timu ya vijana
ya Yanga, Abubakar Salum ‘Sure Boy’ jana hajafanya
mazoezi na leo pia, naye pia akituhumiwa kucheza kinazi
katika mechi dhidi ya Yanga. Stewart anakuwa kocha wa
nne ndani ya miaka minne kufukuzwa Azam, tangu
Neider dos Santos, Sylvester Marsh na Itamar Amorin,
Mbrazil mwingine. Lakini ni Stewart angalau
anaacha kumbukumbu ya taji na Medali Azam, baada
ya kuiwezesha kutwa Kombe la Mapinduzi Januari,
kushika nafasi ya pili katika Ligi Kuu Aprili, kabla ya
kushika nafasi ya pili Kombe la Urafiki na Kagame mwezi
uliopita

Friday, July 27, 2012

0

Nani Kuibuka Kidedea??: Yanga VS Azam

Posted in , , ,
Ijumaa, 27 Julai 2012 11:59
Chapisha Toleo la kuchapisha
  • KAGAME_CUP_2012• NANI kulikwaa ‘BUTI la DHAHABU??’
Jumamosi Julai 28 Fainali ya Kagame Cup, Kombe la Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, itafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa Mechi kati ya Mabingwa watetezi Yanga na Azam FC.
Hakuna Mdau yeyote wa Soka mwenye uhakika kama Yanga watafanikiwa kutetea vyema Taji lao walilolitwaa Mwaka jana kwa kuwafunga Mahasimu wao Simba bao 1-0 kwenye Fainali au Timu mpya kwenye Mashindano haya, Azam, inaweza kujiwekea historia kwa kulibeba Kombe hili kwa mara ya kwanza.
Uhakika pekee uliokuwepo ni kuwa Kagame Cup inabaki tena Tanzania kwa mara ya pili mfululizo.
==========================
WAMEFIKAJE FAINALI:
YANGA
KUNDI C:
-Atletico 0-2
-El Salaam Wau 7-1
-APR 2-0
ROBO FAINALI:
-Mafunzo 1-1 [Penati 5-3]
NUSU FAINALI:
-APR 1-0 [Baada ya Dakika 120]
AZAM
KUNDI B:
-Mafunzo 1-1
-Tusker 0-0
ROBO FAINALI:
-Simba 3-1
NUSU FAINALI:
-Vita Club 2-1
==========================
YANGA-AZAM3NATIONAL_STADIUM2Hakika Fainali hii ni ngumu na imezua mjadala mkubwa hasa ikikumbukwa mara ya mwisho Timu hizi kukutana ilikuwa ni kwenye Ligi Kuu Vodacom Mechi ambayo Azam walishinda bao 3-1 lakini Mechi hii ilizua balaa kubwa baada kutokea vurugu kwa Mwamuzi Israel Nkongo mara baada ya kumpa Kadi Nyekundu Niyonzima wa Yanga na kusababisha Wachezaji kadhaa wa Yanga kupigwa Faini na kufungiwa kwa madai ya kumpiga Refa huyo.
==========================
WAGOMBEA ‘BUTI la DHAHABU’:
-Teddy Etekiama [Vita Club]=Bao 6
-Said Bahanuzi [Yanga]=5
-Hamisi Kiiza [Yanga]=5
-John Bocco [Azam]=5
-Suleiman Ndikumana [APR]=3
-Preus [APR]=2
-Abdallah Juma [Simba]=2
==========================
Mbali ya kuwa na Timu zilizosheheni Wachezaji mahiri Timu hizi pia zina Mastraika hatari mno ambao pia wana vita kubwa kati yao ya kuwania Tuzo ya Mfungaji Bora kwenye michuano hii ambayo hadi sasa alieshika Nambari Wani kwenye safu ya ufungaji ni Teddy Etekiam wa Vita Club mwenye Bao 6 na anafukuzwa na Wachezaji watatu wenye Bao 5 kila mmoja ambao ni Said Bahanuzi na Hamisi Kiiza wa Yanga na John Bocco wa Azam.
Wachezaji wote hawa wana nafasi nzuri ya kuongeza Mabao wakati Timu zao zitakapocheza Fainali na ile Mechi ya kutafuta Mshindi wa Tatu.
RATIBA:
MSHINDI WA 3:
Julai 28 Jumamosi
[Saa 8 Mchana]
Vita v APR
FAINALI:
Julai 28 Jumamosi
[Saa 10 Mchana]
Azam v Yanga
KWA RATIBA na HABARI NYINGINE BOFYA: http://www.sokainbongo.com/kagame-cup-2012

Wednesday, June 13, 2012

0

YANGA YA THIBITISHA UJIO WA MARCIO MAXIMO BONGO JUMAPILI HII

Posted in ,

Baada ya siku chache zilizopita klabu ya Yanga kulipoti ipo katika hatua za mwisho za kumsaini Marcio Maximo, leo hii imefahamika kwamba kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ Mbrazil, Marcio Maximo anatarajia kutua nchini kwa mara nyingine tena toka aondoke nchini mwezi juni mwaka 2010 siku ya jumapili juni 17 saa 9 alasiri…
Maximo anakuja nchini kuchukua mikoba ya Mserbia wa Yanga Kostadin Papic aliyenyimwa mkataba mpya, baada ya ule wa awali wa miezi 6 kuisha wakati ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2011/12 ukielekea mwishoni

Saturday, June 9, 2012

0

MAXIMO kutua Yanga???

Posted in ,

YANGA_MJENGOZipo taarifa zilizozagaa kuwa aliekuwa Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, kutoka Brazil, Marcio Maximo, ambae kwa sasa anafundisha Soka huko kwao Brazil, yupo njiani kurudi Nchini ili kuinoa Yanga kwa ajili ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na ya Kati, Kagame Cup, inayotarajiwa kuanza kuchezwa Jijini Dar es Salaam kuanzia Juni 23 hadi Julai 7.
Yanga ndio Mabingwa Watetezi wa Kombe hilo ambalo walilitwaa Mwaka jana kwa kuifunga Simba bao 1-0 Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam.
MARCIO_MAXIMO
Yanga, ambayo kwa sasa ipo kwenye mchakato wa Uchaguzi mdogo utakaofanyika Julai 15 ili kuziba nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti  pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji, ipo kwenye harakati kamambe za usajili ambao unadaiwa unatokana na ushauri wa Maximo.
Inasemekana Maximo atatua Dar es Salaam pamoja na Kocha Msaidizi ambae ni Mtaalam wa Mazoezi ya Viungo.
Inadaiwa Wachezaji ambao Maximo ameshauri wasajiliwe ni pamoja na Kipa Ali Mustapha ‘Barthez’ na Beki toka Simba, Kelvin Yondani, ambae tayari ameshaanza kuleta vuta nikuvute kati ya Yanga na Simba.
Mpaka sasa inadaiwa Yanga imeshawasajili Beki wa Kagera Sugar David Luhende, Mussa Hassan Mgossi [DC Motema Pembe], Owen Kasule, Raia wa Uganda [Hoang Anh Gia Lai ya Vietnam], Meddie Kagere [Polisi, Rwanda], Nizar Khalfan na Wachezaji wawili wa Mtibwa Sugar, Said Bahanuzi na Juma Abdul.

source: sokainbongo.com

Wednesday, May 23, 2012

0

TFF yapinga ‘Mapinduzi’ Yanga!

Posted in ,

YANGASHIRIKISHO la Soka Tanzania, TFF, limetangaza kutoutambaua uongozi wa muda uliowekwa madarakani na Wanachama wa Yanga. 
Majuzi, zaidi ya wanachama 600 wa Yanga wakiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Yanga, Bakili Makele, pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee, Ibrahim Akilimali, walitangaza kumng’oa madarakani Mwenyekiti wao, Lloyd Nchunga.
Jana TFF imesambaza Taarifa iliyosainiwa na Katibu Mkuu wake, Angetile Osiah, ikitaka Wananachama wao kufuata Katiba zao zinavyosema kuhusu utaratibu mzima wa uongozi na namna ya kuwaondoa viongozi wao madarakani. 
Osiah alisema hakuna Katiba yoyote inayomlinda kiongozi aendelee kukaa madarakani, lakini Klabu zinapaswa kufuata utashi wa Katiba zao zinavyosema ili kufanya mabadiliko ya uongozi ndani ya vyama vyao na si kupitia Vikao visivyo halali. 
TFF imesema haiko tayari kufanya kazi na uongozi wa Kamati za muda na imewaonya Wanachama wa TFF kuwa lazima waheshimu Katiba zao katika kufikia maamuzi mbalimbali wanayofanya. 
Kuhusu kujiuzulu Wajumbe wa Kamati ya Utendaji wa Klabu hiyo, Osiah alifafanua kuwa Katiba ya Yanga inasema wazi kuwa lazima nafasi za Wajumbe hao kujazwa kwenye Mkutano Mkuu wa Klabu hiyo uliopangwa kufanyika Julai 15. 
Tayari wajumbe saba kati ya 13 wa Kamati ya Utendaji ya Yanga wamejiuzulu na mmoja, Theonist Rutashoborwa, amefariki dunia Mwezi uliopita. 
Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ambao hawajajiuzulu ni Mwenyekiti Nchunga, Sarah Ramadhani, Charles Mngodo, Salum Rupia na Tito Ossoro.

Thursday, May 17, 2012

0

KAGAME CUP: Klabu 12 kushiriki Dar, kugharimu Milioni 900!!

Posted in , ,


kagamecup07
Katibu Mkuu wa CECAFA, Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati, Nicholas Musonye, amesema Timu 12 zitashiriki Mashindano ya Mwaka huu ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kagame Cup, ambayo yatagharimu Dola 600,000 (zaidi ya Shilingi Milioni 900) na yatachezwa Jijini Dar es Salaam kuanzia Juni 23 hadi Julai 7.
Mwaka jana, michuano ya Kagame Cup, iliyodhamini wa na Kampuni ya Bia Tanzania TBL kupitia Bia yake ya Castle kwa Sh300 milioni, Ilifanyika Jjini Dar es Salaam na Yanga kuibuka Bingwa kwa kuichapa Simba kwa bao 1-0 kwa bao la dakika za majeruhi lililofungwa na Straika kutoka Ghana, Kenneth Asamoah.
Musonye alisema Ratiba ya michuano hiyo, ambayo itaonyeshwa moja kwa moja na Kituo cha TV cha Supersport, itapangwa baada ya Timu zote 12 kuthibitisha ushiriki wao.
Akifafanua kwa nini Tanzania inakuwa Mwenyeji wa Mashindano hayo kwa Miaka mitatu mfululizo, Musonye alisema ni sababu ya mafanikio yaliyopatikana katika mashindano ya Kombe la Chalenji na Kombe la Kagame Mwaka jana pamoja na uhakika wa udhamini.
Kawaida, zawadi za Washindi zimekuwa zikitolewa na Rais wa Rwanda, Paul Kagame, ambae ndie ametoa Kombe na pia hutoa Tuzo ya Dola 60,000 kwa Bingwa.
Mwaka jana timu 13 zilishiriki, ambazo ni Ulinzi (Kenya), Ports (Djibouti), St George (Ethiopia), El Merreikh (Sudan), Red Sea (Eritrea), Elman (Somalia), APR na Etincelles (zote toka Rwanda), Bunamwaya (Uganda), Vital'O (Burundi), Simba na Yanga za Tanzania
 
More News: www.sokainbongo.com
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ