KLABU YA DAR YOUNG AFRICANS, YAINGIA MKATABA MNONO
Posted in Yanga SC
Klabu ya mpira wa miguu kutoka Jangwani Young Africans maarufu kama Yanga, imeingia mkataba na SGM
ya Ufaransa kwa ajili ya kurusha mchezo wake wa hatua ya kwanza ya
mashindano ya klabu Bingwa Afrika dhidi ya timu ya Alh Ahly ya Misri kwa
gharama ya dola za kimarekani elfu 55,000 sawa na mil 90/= za
kitanzania kwa muda wa dakika 90.
Katibu Mkuu wa Young Africans Bw. Beno Njovu amesema wameingia mkataba huo na kampuni ya SGM kutoka nchini Ufaransa ambapo kampuni hiyo wameipa uwakala kampuni ya MGB ya Zamaleki ya Cairo kama wawakilishi wa kampuni hiyo ya SGM.
Mkataba huo unawapa kibali kampuni ya SGM kurusha moja kwa moja (Live) michezo yote ya Yanga ya Klabu Bingwa Africa ukiwamo mchezo dhidi ya Al Ahly utakaofanyika Tanzania na marudiano kufanyikia nchini Misri. Yanga itaanza michuano hiyo ya Klabu Bingwa Africa kwa kukipiga dhidi ya timu ya Komoronize ya Visiwa vya Comoro Februari 8 mwakani katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kabla ya kurudiana nao wiki baadae nchini kwao Comoro na kama Yanga itafanikiwa kuvuka hatua hiyo ndio itakutana na Al Ahly Februari 28.
0 Maoni/comments: