Wednesday, August 1, 2012

0

Mrisho Ngassa Asababisha Kocha wa Azam kutimuliwa

Posted in , , , ,

STEWART Hall, kocha Muingereza wa Azam FC jana amefukuzwa rasmi katika klabu hiyo kwa kosa la kukaidi maagizo ya Bodi ya Ukurugenzi ya klabu hiyo, kumpanga Mrisho Khalfan Ngassa katika mechi ya fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame. Habari ambazo BIN ZUBEIRY imezipata kutoka ndani ya Azam, zimesema kwamba kikao cha jana cha pamoja baina ya Bodi ya Ukurugenzi ya Azam FC, Mwanasheria wa kampuni na kocha
Stewart kimeafiki kuvunj ndoa hiyo na sasa Azam FC itakuwa chini ya kocha
kutoka India, Vivek Nagul ambaye alikuwa anafundisha timu ya vijana.
Habari zinasema kwamba mapema baada ya mechi ya Nusu Fainali ya Kagame, kati ya Azam na AS Vita ya DRC, Stewart aliitwa na kuambiwa asimtumie tena Ngassa kwa kitendo cha mchezaji huyo kwenda kuibusu na kuivaa jezi ya Yanga, baada ya kufunga bao la ushindi.
Lakini Stewart katika kikao hicho, kwanza alimtetea Ngassa kutokana na
kufunga bao la ushindi na\ kumuelezea kama mchezaji
muhimu kwake, lakini msimamo wa bodi ulikuwa
ni asipangwe tena. Katika fainali, Stewart
alimvalisha jezi Ngassa akamuanzishia benchi, lakini
kama ilivyokuwa kwenye Nusu Fainali alimuingiza
kipindi cha pili timu ikiwa nyuma kwa 1-0 na mwisho
wa mchezo ikashinda 2-2 yeye akifunga la pili, dhidi
ya Yanga pia alimuingiza timu ikiwa nyuma kwa 1-0.
Lakini Ngassa alishindwakurudia kile alichofanya kwenye mechi na AS Vita na
Yanga ikashinda 2-0. Kwa sasa mazungumzo
yanaendelea kati ya Yanga na Azam juu ya Ngassa ili
mchezaji huyo arejee Jangwani, lakini wakati huo
huo, Simba nao wameweka dau la Sh. Milioni 25 katika
50 zinazotakiwa na Azam ili kumuuza mchezaji huyo.
Mbali na Ngassa, kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’
pia yuko katika wakati mgumu na jana inadaiwa
alionekana akilia wakati anazungumza na kiongozi
mmoja wa Azam, akiuliza ni lipi kosa lake.
Sure Boy, ambaye ni mtoto wa kocha wa timu ya vijana
ya Yanga, Abubakar Salum ‘Sure Boy’ jana hajafanya
mazoezi na leo pia, naye pia akituhumiwa kucheza kinazi
katika mechi dhidi ya Yanga. Stewart anakuwa kocha wa
nne ndani ya miaka minne kufukuzwa Azam, tangu
Neider dos Santos, Sylvester Marsh na Itamar Amorin,
Mbrazil mwingine. Lakini ni Stewart angalau
anaacha kumbukumbu ya taji na Medali Azam, baada
ya kuiwezesha kutwa Kombe la Mapinduzi Januari,
kushika nafasi ya pili katika Ligi Kuu Aprili, kabla ya
kushika nafasi ya pili Kombe la Urafiki na Kagame mwezi
uliopita

0 Maoni/comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ