Next
Previous
Showing posts with label Kagame Cup. Show all posts

Wednesday, August 1, 2012

0

Mrisho Ngassa Asababisha Kocha wa Azam kutimuliwa

Posted in , , , ,

STEWART Hall, kocha Muingereza wa Azam FC jana amefukuzwa rasmi katika klabu hiyo kwa kosa la kukaidi maagizo ya Bodi ya Ukurugenzi ya klabu hiyo, kumpanga Mrisho Khalfan Ngassa katika mechi ya fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame. Habari ambazo BIN ZUBEIRY imezipata kutoka ndani ya Azam, zimesema kwamba kikao cha jana cha pamoja baina ya Bodi ya Ukurugenzi ya Azam FC, Mwanasheria wa kampuni na kocha
Stewart kimeafiki kuvunj ndoa hiyo na sasa Azam FC itakuwa chini ya kocha
kutoka India, Vivek Nagul ambaye alikuwa anafundisha timu ya vijana.
Habari zinasema kwamba mapema baada ya mechi ya Nusu Fainali ya Kagame, kati ya Azam na AS Vita ya DRC, Stewart aliitwa na kuambiwa asimtumie tena Ngassa kwa kitendo cha mchezaji huyo kwenda kuibusu na kuivaa jezi ya Yanga, baada ya kufunga bao la ushindi.
Lakini Stewart katika kikao hicho, kwanza alimtetea Ngassa kutokana na
kufunga bao la ushindi na\ kumuelezea kama mchezaji
muhimu kwake, lakini msimamo wa bodi ulikuwa
ni asipangwe tena. Katika fainali, Stewart
alimvalisha jezi Ngassa akamuanzishia benchi, lakini
kama ilivyokuwa kwenye Nusu Fainali alimuingiza
kipindi cha pili timu ikiwa nyuma kwa 1-0 na mwisho
wa mchezo ikashinda 2-2 yeye akifunga la pili, dhidi
ya Yanga pia alimuingiza timu ikiwa nyuma kwa 1-0.
Lakini Ngassa alishindwakurudia kile alichofanya kwenye mechi na AS Vita na
Yanga ikashinda 2-0. Kwa sasa mazungumzo
yanaendelea kati ya Yanga na Azam juu ya Ngassa ili
mchezaji huyo arejee Jangwani, lakini wakati huo
huo, Simba nao wameweka dau la Sh. Milioni 25 katika
50 zinazotakiwa na Azam ili kumuuza mchezaji huyo.
Mbali na Ngassa, kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’
pia yuko katika wakati mgumu na jana inadaiwa
alionekana akilia wakati anazungumza na kiongozi
mmoja wa Azam, akiuliza ni lipi kosa lake.
Sure Boy, ambaye ni mtoto wa kocha wa timu ya vijana
ya Yanga, Abubakar Salum ‘Sure Boy’ jana hajafanya
mazoezi na leo pia, naye pia akituhumiwa kucheza kinazi
katika mechi dhidi ya Yanga. Stewart anakuwa kocha wa
nne ndani ya miaka minne kufukuzwa Azam, tangu
Neider dos Santos, Sylvester Marsh na Itamar Amorin,
Mbrazil mwingine. Lakini ni Stewart angalau
anaacha kumbukumbu ya taji na Medali Azam, baada
ya kuiwezesha kutwa Kombe la Mapinduzi Januari,
kushika nafasi ya pili katika Ligi Kuu Aprili, kabla ya
kushika nafasi ya pili Kombe la Urafiki na Kagame mwezi
uliopita

Friday, July 27, 2012

0

Nani Kuibuka Kidedea??: Yanga VS Azam

Posted in , , ,
Ijumaa, 27 Julai 2012 11:59
Chapisha Toleo la kuchapisha
  • KAGAME_CUP_2012• NANI kulikwaa ‘BUTI la DHAHABU??’
Jumamosi Julai 28 Fainali ya Kagame Cup, Kombe la Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, itafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa Mechi kati ya Mabingwa watetezi Yanga na Azam FC.
Hakuna Mdau yeyote wa Soka mwenye uhakika kama Yanga watafanikiwa kutetea vyema Taji lao walilolitwaa Mwaka jana kwa kuwafunga Mahasimu wao Simba bao 1-0 kwenye Fainali au Timu mpya kwenye Mashindano haya, Azam, inaweza kujiwekea historia kwa kulibeba Kombe hili kwa mara ya kwanza.
Uhakika pekee uliokuwepo ni kuwa Kagame Cup inabaki tena Tanzania kwa mara ya pili mfululizo.
==========================
WAMEFIKAJE FAINALI:
YANGA
KUNDI C:
-Atletico 0-2
-El Salaam Wau 7-1
-APR 2-0
ROBO FAINALI:
-Mafunzo 1-1 [Penati 5-3]
NUSU FAINALI:
-APR 1-0 [Baada ya Dakika 120]
AZAM
KUNDI B:
-Mafunzo 1-1
-Tusker 0-0
ROBO FAINALI:
-Simba 3-1
NUSU FAINALI:
-Vita Club 2-1
==========================
YANGA-AZAM3NATIONAL_STADIUM2Hakika Fainali hii ni ngumu na imezua mjadala mkubwa hasa ikikumbukwa mara ya mwisho Timu hizi kukutana ilikuwa ni kwenye Ligi Kuu Vodacom Mechi ambayo Azam walishinda bao 3-1 lakini Mechi hii ilizua balaa kubwa baada kutokea vurugu kwa Mwamuzi Israel Nkongo mara baada ya kumpa Kadi Nyekundu Niyonzima wa Yanga na kusababisha Wachezaji kadhaa wa Yanga kupigwa Faini na kufungiwa kwa madai ya kumpiga Refa huyo.
==========================
WAGOMBEA ‘BUTI la DHAHABU’:
-Teddy Etekiama [Vita Club]=Bao 6
-Said Bahanuzi [Yanga]=5
-Hamisi Kiiza [Yanga]=5
-John Bocco [Azam]=5
-Suleiman Ndikumana [APR]=3
-Preus [APR]=2
-Abdallah Juma [Simba]=2
==========================
Mbali ya kuwa na Timu zilizosheheni Wachezaji mahiri Timu hizi pia zina Mastraika hatari mno ambao pia wana vita kubwa kati yao ya kuwania Tuzo ya Mfungaji Bora kwenye michuano hii ambayo hadi sasa alieshika Nambari Wani kwenye safu ya ufungaji ni Teddy Etekiam wa Vita Club mwenye Bao 6 na anafukuzwa na Wachezaji watatu wenye Bao 5 kila mmoja ambao ni Said Bahanuzi na Hamisi Kiiza wa Yanga na John Bocco wa Azam.
Wachezaji wote hawa wana nafasi nzuri ya kuongeza Mabao wakati Timu zao zitakapocheza Fainali na ile Mechi ya kutafuta Mshindi wa Tatu.
RATIBA:
MSHINDI WA 3:
Julai 28 Jumamosi
[Saa 8 Mchana]
Vita v APR
FAINALI:
Julai 28 Jumamosi
[Saa 10 Mchana]
Azam v Yanga
KWA RATIBA na HABARI NYINGINE BOFYA: http://www.sokainbongo.com/kagame-cup-2012

Thursday, May 17, 2012

0

KAGAME CUP: Klabu 12 kushiriki Dar, kugharimu Milioni 900!!

Posted in , ,


kagamecup07
Katibu Mkuu wa CECAFA, Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati, Nicholas Musonye, amesema Timu 12 zitashiriki Mashindano ya Mwaka huu ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kagame Cup, ambayo yatagharimu Dola 600,000 (zaidi ya Shilingi Milioni 900) na yatachezwa Jijini Dar es Salaam kuanzia Juni 23 hadi Julai 7.
Mwaka jana, michuano ya Kagame Cup, iliyodhamini wa na Kampuni ya Bia Tanzania TBL kupitia Bia yake ya Castle kwa Sh300 milioni, Ilifanyika Jjini Dar es Salaam na Yanga kuibuka Bingwa kwa kuichapa Simba kwa bao 1-0 kwa bao la dakika za majeruhi lililofungwa na Straika kutoka Ghana, Kenneth Asamoah.
Musonye alisema Ratiba ya michuano hiyo, ambayo itaonyeshwa moja kwa moja na Kituo cha TV cha Supersport, itapangwa baada ya Timu zote 12 kuthibitisha ushiriki wao.
Akifafanua kwa nini Tanzania inakuwa Mwenyeji wa Mashindano hayo kwa Miaka mitatu mfululizo, Musonye alisema ni sababu ya mafanikio yaliyopatikana katika mashindano ya Kombe la Chalenji na Kombe la Kagame Mwaka jana pamoja na uhakika wa udhamini.
Kawaida, zawadi za Washindi zimekuwa zikitolewa na Rais wa Rwanda, Paul Kagame, ambae ndie ametoa Kombe na pia hutoa Tuzo ya Dola 60,000 kwa Bingwa.
Mwaka jana timu 13 zilishiriki, ambazo ni Ulinzi (Kenya), Ports (Djibouti), St George (Ethiopia), El Merreikh (Sudan), Red Sea (Eritrea), Elman (Somalia), APR na Etincelles (zote toka Rwanda), Bunamwaya (Uganda), Vital'O (Burundi), Simba na Yanga za Tanzania
 
More News: www.sokainbongo.com
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ