Next
Previous
Showing posts with label Maximo. Show all posts

Wednesday, June 13, 2012

0

YANGA YA THIBITISHA UJIO WA MARCIO MAXIMO BONGO JUMAPILI HII

Posted in ,

Baada ya siku chache zilizopita klabu ya Yanga kulipoti ipo katika hatua za mwisho za kumsaini Marcio Maximo, leo hii imefahamika kwamba kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ Mbrazil, Marcio Maximo anatarajia kutua nchini kwa mara nyingine tena toka aondoke nchini mwezi juni mwaka 2010 siku ya jumapili juni 17 saa 9 alasiri…
Maximo anakuja nchini kuchukua mikoba ya Mserbia wa Yanga Kostadin Papic aliyenyimwa mkataba mpya, baada ya ule wa awali wa miezi 6 kuisha wakati ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2011/12 ukielekea mwishoni

Saturday, June 9, 2012

0

MAXIMO kutua Yanga???

Posted in ,

YANGA_MJENGOZipo taarifa zilizozagaa kuwa aliekuwa Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, kutoka Brazil, Marcio Maximo, ambae kwa sasa anafundisha Soka huko kwao Brazil, yupo njiani kurudi Nchini ili kuinoa Yanga kwa ajili ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na ya Kati, Kagame Cup, inayotarajiwa kuanza kuchezwa Jijini Dar es Salaam kuanzia Juni 23 hadi Julai 7.
Yanga ndio Mabingwa Watetezi wa Kombe hilo ambalo walilitwaa Mwaka jana kwa kuifunga Simba bao 1-0 Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam.
MARCIO_MAXIMO
Yanga, ambayo kwa sasa ipo kwenye mchakato wa Uchaguzi mdogo utakaofanyika Julai 15 ili kuziba nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti  pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji, ipo kwenye harakati kamambe za usajili ambao unadaiwa unatokana na ushauri wa Maximo.
Inasemekana Maximo atatua Dar es Salaam pamoja na Kocha Msaidizi ambae ni Mtaalam wa Mazoezi ya Viungo.
Inadaiwa Wachezaji ambao Maximo ameshauri wasajiliwe ni pamoja na Kipa Ali Mustapha ‘Barthez’ na Beki toka Simba, Kelvin Yondani, ambae tayari ameshaanza kuleta vuta nikuvute kati ya Yanga na Simba.
Mpaka sasa inadaiwa Yanga imeshawasajili Beki wa Kagera Sugar David Luhende, Mussa Hassan Mgossi [DC Motema Pembe], Owen Kasule, Raia wa Uganda [Hoang Anh Gia Lai ya Vietnam], Meddie Kagere [Polisi, Rwanda], Nizar Khalfan na Wachezaji wawili wa Mtibwa Sugar, Said Bahanuzi na Juma Abdul.

source: sokainbongo.com
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ