YANGA KUKABIDHIWA KOMBE KATIKA MECHI DHIDI YA SIMBA
Posted in Simba SC, Vodacom Premier League, Yanga SCShirikisho la Soka Tanzania (TFF) litakabidhi kombe kwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, Yanga katika mechi yao ya mwisho ya ligi hiyo dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Simba kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Mei 18.
Akizungumza na NIPASHE jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi ya TFF, Wallace Karia alisema kuwa wataikabidhi Yanga kombe hilo baada ya kumalizika kwa mechi hiyo ya kufunga msimu wa 2012/13 wa ligi.
0 Maoni/comments: