Nani Kuibuka Kidedea??: Yanga VS Azam
Posted in Azam FC, Kagame Cup, Simba SC, Yanga SC
Ijumaa, 27 Julai 2012 11:59
- • NANI kulikwaa ‘BUTI la DHAHABU??’
Jumamosi Julai 28 Fainali ya Kagame Cup,
Kombe la Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, itafanyika Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam kwa Mechi kati ya Mabingwa watetezi Yanga na Azam
FC.
Hakuna Mdau yeyote wa Soka mwenye
uhakika kama Yanga watafanikiwa kutetea vyema Taji lao walilolitwaa
Mwaka jana kwa kuwafunga Mahasimu wao Simba bao 1-0 kwenye Fainali au
Timu mpya kwenye Mashindano haya, Azam, inaweza kujiwekea historia kwa
kulibeba Kombe hili kwa mara ya kwanza.
Uhakika pekee uliokuwepo ni kuwa Kagame Cup inabaki tena Tanzania kwa mara ya pili mfululizo.
==========================
WAMEFIKAJE FAINALI:
YANGA KUNDI C: -Atletico 0-2 -El Salaam Wau 7-1 -APR 2-0 ROBO FAINALI: -Mafunzo 1-1 [Penati 5-3] NUSU FAINALI: -APR 1-0 [Baada ya Dakika 120] |
AZAM KUNDI B: -Mafunzo 1-1 -Tusker 0-0 ROBO FAINALI: -Simba 3-1 NUSU FAINALI: -Vita Club 2-1 |
==========================
Hakika
Fainali hii ni ngumu na imezua mjadala mkubwa hasa ikikumbukwa mara ya
mwisho Timu hizi kukutana ilikuwa ni kwenye Ligi Kuu Vodacom Mechi
ambayo Azam walishinda bao 3-1 lakini Mechi hii ilizua balaa kubwa baada
kutokea vurugu kwa Mwamuzi Israel Nkongo mara baada ya kumpa Kadi
Nyekundu Niyonzima wa Yanga na kusababisha Wachezaji kadhaa wa Yanga
kupigwa Faini na kufungiwa kwa madai ya kumpiga Refa huyo.
==========================
WAGOMBEA ‘BUTI la DHAHABU’:
-Teddy Etekiama [Vita Club]=Bao 6
-Said Bahanuzi [Yanga]=5
-Hamisi Kiiza [Yanga]=5
-John Bocco [Azam]=5
-Suleiman Ndikumana [APR]=3
-Preus [APR]=2
-Abdallah Juma [Simba]=2
==========================
Mbali ya kuwa na Timu
zilizosheheni Wachezaji mahiri Timu hizi pia zina Mastraika hatari mno
ambao pia wana vita kubwa kati yao ya kuwania Tuzo ya Mfungaji Bora
kwenye michuano hii ambayo hadi sasa alieshika Nambari Wani kwenye safu
ya ufungaji ni Teddy Etekiam wa Vita Club mwenye Bao 6 na anafukuzwa na
Wachezaji watatu wenye Bao 5 kila mmoja ambao ni Said Bahanuzi na Hamisi
Kiiza wa Yanga na John Bocco wa Azam.
Wachezaji wote hawa wana nafasi nzuri ya
kuongeza Mabao wakati Timu zao zitakapocheza Fainali na ile Mechi ya
kutafuta Mshindi wa Tatu.
RATIBA:
MSHINDI WA 3:
Julai 28 Jumamosi
[Saa 8 Mchana]
Vita v APR
FAINALI:
Julai 28 Jumamosi
[Saa 10 Mchana]
Azam v Yanga
KWA RATIBA na HABARI NYINGINE BOFYA: http://www.sokainbongo.com/kagame-cup-2012
0 Maoni/comments: