MAXIMO kutua Yanga???
Posted in Maximo, Yanga SC
Yanga ndio Mabingwa Watetezi wa Kombe
hilo ambalo walilitwaa Mwaka jana kwa kuifunga Simba bao 1-0 Uwanja wa
Taifa, Jijini Dar es Salaam.
Yanga, ambayo kwa sasa ipo kwenye
mchakato wa Uchaguzi mdogo utakaofanyika Julai 15 ili kuziba nafasi za
Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji,
ipo kwenye harakati kamambe za usajili ambao unadaiwa unatokana na
ushauri wa Maximo.
Inasemekana Maximo atatua Dar es Salaam pamoja na Kocha Msaidizi ambae ni Mtaalam wa Mazoezi ya Viungo.
Inadaiwa Wachezaji ambao Maximo
ameshauri wasajiliwe ni pamoja na Kipa Ali Mustapha ‘Barthez’ na Beki
toka Simba, Kelvin Yondani, ambae tayari ameshaanza kuleta vuta nikuvute
kati ya Yanga na Simba.
Mpaka sasa inadaiwa Yanga imeshawasajili
Beki wa Kagera Sugar David Luhende, Mussa Hassan Mgossi [DC Motema
Pembe], Owen Kasule, Raia wa Uganda [Hoang Anh Gia Lai ya Vietnam],
Meddie Kagere [Polisi, Rwanda], Nizar Khalfan na Wachezaji wawili wa
Mtibwa Sugar, Said Bahanuzi na Juma Abdul.
source: sokainbongo.com
0 Maoni/comments: