>> UCHAGUZI TAREFA, TAFCA SASA DESEMBA 22
>> TFF YATOA PONGEZI KWA UONGOZI MPYA FA MWANZA

Kamati
ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, TFF, imefanya
mabadiliko madogo ya ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom, VPL, ili kupitisha
Mechi ya Kirafiki ya Kalenda ya FIFA kati ya Taifa Stars na Kenya,
Harambe Stars, itakayochezwa Novemba 14 Jijini Mwanza na mabadiliko
mengine yanahusu Ratiba ya Ligi Daraja la Kwanza, FDL.
Zifuatazo ni Taarifa kamili za TFF:
Release No. 180
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Novemba 9, 2012
MECHI TANO VPL ZAPISHA TAIFA STARS
Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) imefanya mabadiliko madogo ya ratiba ya Ligi Kuu
ya Vodacom ili kupitisha mechi ya kirafiki ya kalenda ya Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kati ya Taifa Stars na Kenya (Harambe
Stars) itakayochezwa Novemba 14 mwaka huu jijini Mwanza.
Mechi tano za ligi hiyo zilizokuwa
zichezwe Novemba 11 mwaka huu, zimerejeshwa nyuma kwa siku moja ambapo
sasa zitafanyika Novemba 10 mwaka huu. Mechi hizo ni Simba vs Toto
Africans (Uwanja wa Taifa), Kagera Sugar vs Polisi Morogoro (Uwanja wa
Kaitaba) na Oljoro JKT vs Ruvu Shooting (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh
Kaluta Amri Abeid).
Nyingine ni Tanzania Prisons vs JKT Ruvu
(Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine) na African Lyon vs Mtibwa Sugar (Azam
Complex). Mechi ya Mgambo Shooting vs Azam (Azam Complex) yenyewe
itachezwa Novemba 10 mwaka huu kama ilivyokuwa imepangwa.
Nayo mechi ya Coastal Union vs Yanga
(Uwanja wa Mkwakwani) itabaki Novemba 11 mwaka huu kwa vile Novemba 10
mwaka huu uwanja huo utakuwa na mechi nyingine. TFF imepanga utaratibu
wa kuwapata kwa wakati wachezaji wa Yanga walioitwa kwenye kikosi cha
Taifa Stars.
Mabadiliko mengine ni ya Ligi Daraja la
Kwanza (FDL) ambapo mechi ya Villa Squad vs Transit Camp iliyokuwa
ichezwe Novemba 8 mwaka huu sasa inachezwa Novemba 9 mwaka huu, na ile
ya Novemba 7 mwaka huu kati ya Burkina Faso na Small Kids inachezwa
Novemba 9 mwaka huu. Viwanja ni vilevile.