Next
Previous
Showing posts with label Taifa Stars. Show all posts

Wednesday, August 21, 2013

0

WACHEZAJI 24 WAITWA TAIFA STARS

Posted in ,
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen amewaita kambini wachezaji 24 ili kujiandaa na mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu nchini humo.

Wachezaji hao wanatakiwa kuripoti kambini Agosti 29 mwaka huu kabla ya saa 1 kamili usiku.

Kambi ya Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itakuwa kwenye hoteli ya Accommondia jijini Dar es Salaam.

Wachezaji walioitwa katika timu Taifa makipa Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ali (Azam), Ally Mustafa (Yanga) na Aishi Manula (Azam).

Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (Simba), Nadir Haroub (Yanga), Erasto Nyoni (Azam), Vincent Barnabas (Mtibwa Sugar) na David Luhende (Yanga).

Viungo ni Khamis Mcha (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Dilunga (Ruvu Shooting), Frank Domayo (Yanga), Athuman Idd (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Amir Kiemba (Simba), Mrisho Ngasa (Yanga), Simon Msuva (Yanga), John Boko (Azam), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo) na Juma Liuzio (Mtibwa Sugar).

Katika mechi dhidi ya Gambia ni kukamilisha ratiba ya mechi za kutafuta nafasi ya kushiriki katika kombe la Dunia hapo mwakani nchini Brazil.

Thursday, May 16, 2013

0

KOCHA MKUU TAIFA STARS ATAJA KIKOSI CHA KUIVAA MOROCCO | TIKETI ZA MECHI YA SIMBA NA YANGA ZAANZA UZWA

Posted in , , ,
Na Soka In Bongo
TAIFA_STARS-FRAMED>> TANZANIA YAJITOA MICHUANO YA COSAFA
>> TIKETI SIMBA, YANGA KUANZA KUUZWA KESHO
>>TIKETI NI KUANZIA SH. 5,000 HADI 30,000
PATA HABARI KAMILI:






Release No. 084
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mei 16, 2013
KIM ATAJA 26 STARS WA KUIVAA MOROCCO
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen leo (Mei 16 mwaka huu) ametaja kikosi cha wachezaji 26 watakaoingia kambini kujiwinda kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco itakayochezwa Juni 8 mwaka huu jijini Marrakech, Morocco.
Katika kikosi hicho, Kim ameita wachezaji wapya sita ingawa baadhi yao wamewahi kuchezea timu hiyo, huku akiacha wengine watatu aliokuwa nao kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Morocco ambapo Taifa Stars ilishinda mabao 3-1.
Wapya aliowaita katika kikosi hicho kitakachoingia kambini Mei 20 mwaka huu, saa 1 jioni kwenye hoteli ya Tansoma jijini Dar es Salaam ni Ally Mustafa, Vicent Barnabas, Juma Luzio, Haruna Chanongo, Mudhathiri Yahya na Zahoro Pazi. Wachezaji aliowaacha ni Shabani Nditi, Nassoro Masoud Cholo na Issa Rashid.
Kikosi kamili cha Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ambacho kabla ya kwenda Morocco kitapita jijini Addis Ababa, Ethiopia kucheza mechi ya kirafiki Juni 2 mwaka huu dhidi ya Sudan ni kama ifuatavyo;
Makipa ni nahodha Juma Kaseja (Simba), Aishi Manula (Azam), Ally Mustafa (Yanga) na Mwadini Ally (Azam). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Shomari Kapombe (Simba), Vicent Barnabas (Mtibwa Sugar) na Waziri Salum (Azam).
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Khamis Mcha (Azam), Mwinyi Kazimoto (Simba), Mudathiri Yahya (Azam) na Salum Abubakar

Saturday, December 22, 2012

0

TUSIWALAUMU SAMATTA NA ULIMWENGU

Posted in , , ,
Samatta


Hii Post Niliitoa katika group moja maarufu la kisoka (SPORTS EXTRA CLOUDS FM), Iliandikwa na Mdau Mmoja huku akitoa somo:
Ulimwengu
Nasikitishwa na wadau wachache wanao walaumu Mbwana Ally Sammata na Thomas Ulimwengu tena na kwenda zaidi kuwatusi na kuwalaani.
Ningependa mtambue kwamba hawa vijana ni proffesional and not Amatuers kama Kaseja na Tegete [nami ni mdau wa simba lakini], walikuja kucheza Match na Kenya tena wakaonyesha kiwango cha juu sana, hio match na Kenya ilikua ni International Friendly na inatambulika na FIFA. Sasa jamani tujiulize kwanza hio Friendly Match na CHIPOLOPOLO inatambulika na FIFA???? au inahadhi kama ya CECAFA Challenge ambayo haitambulika atakama ukishinda goli mia kiwango hakipandishi na ndio maana unaona hata kwenye Challenge hawavijana hawajacheza kabisa coz hazitambuliki FIFA..
Vilevile kumbukeni hawamadogo wamerudi huku na Majeruhi ambayo hata TFF imeshindwa kuwalipia Medical Bills pale Muhimbili alafu unategemea watacheza, na sio hawa tu ambao wanafanywa waonekane vibaya kunawachezaji wengi mmoja wapo ni Nditi ambae anachezea Chelsea TFF ilishindwa kumleta kwa mashariti machache tu kama kumlipia hotel na madaktari.
sasa mfikrie hizo blames apewe nani either the Coach Kim au TFF.
MAWAZO YAKO MDAU??????

Friday, November 9, 2012

0

KUTOKA TFF NA WENZETU SOKAinBONGO.com>> RATIBA YAREKEBISHWA KUPISHA MECHI YA STARS

Posted in , , ,
>> UCHAGUZI TAREFA, TAFCA SASA DESEMBA 22
>> TFF YATOA PONGEZI KWA UONGOZI MPYA FA MWANZA
TFF_LOGO12Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, TFF, imefanya mabadiliko madogo ya ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom, VPL, ili kupitisha Mechi ya Kirafiki ya Kalenda ya FIFA kati ya Taifa Stars na Kenya, Harambe Stars, itakayochezwa Novemba 14 Jijini Mwanza na mabadiliko mengine yanahusu Ratiba ya Ligi Daraja la Kwanza, FDL.
Zifuatazo ni Taarifa kamili za TFF:
Release No. 180
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Novemba 9, 2012
MECHI TANO VPL ZAPISHA TAIFA STARS
Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imefanya mabadiliko madogo ya ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom ili kupitisha mechi ya kirafiki ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kati ya Taifa Stars na Kenya (Harambe Stars) itakayochezwa Novemba 14 mwaka huu jijini Mwanza.
Mechi tano za ligi hiyo zilizokuwa zichezwe Novemba 11 mwaka huu, zimerejeshwa nyuma kwa siku moja ambapo sasa zitafanyika Novemba 10 mwaka huu. Mechi hizo ni Simba vs Toto Africans (Uwanja wa Taifa), Kagera Sugar vs Polisi Morogoro (Uwanja wa Kaitaba) na Oljoro JKT vs Ruvu Shooting (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid).
Nyingine ni Tanzania Prisons vs JKT Ruvu (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine) na African Lyon vs Mtibwa Sugar (Azam Complex). Mechi ya Mgambo Shooting vs Azam (Azam Complex) yenyewe itachezwa Novemba 10 mwaka huu kama ilivyokuwa imepangwa.
Nayo mechi ya Coastal Union vs Yanga (Uwanja wa Mkwakwani) itabaki Novemba 11 mwaka huu kwa vile Novemba 10 mwaka huu uwanja huo utakuwa na mechi nyingine. TFF imepanga utaratibu wa kuwapata kwa wakati wachezaji wa Yanga walioitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars.
Mabadiliko mengine ni ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ambapo mechi ya Villa Squad vs Transit Camp iliyokuwa ichezwe Novemba 8 mwaka huu sasa inachezwa Novemba 9 mwaka huu, na ile ya Novemba 7 mwaka huu kati ya Burkina Faso na Small Kids inachezwa Novemba 9 mwaka huu. Viwanja ni vilevile.

Thursday, June 7, 2012

0

TOKA TFF: Taifa Stars, Gambia Marefa ni wa Zimbabwe

Posted in , ,


  • BRAZIL_2014_ORIJINO11• GAMBIA wachelewa, kutua leo Saa 9 Usiku!
Kufuatia Taarifa iliyosambazwa na Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, lile pambano kati ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars,na Gambia liitakalochezwa Jumapili Juni 10 Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam la Kundi C la Kanda ya Afrika kusaka Timu 5 zitakazocheza Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil Mwaka 2014, litachezeshwa na Waamuzi kutoka Zimbabwe.
Pia, Taarifa hiyo imejulisha kuhusu kuchelewa kuwasili kwa Msafara wa Gambia.
IFUATAYO NI TAARIFA KAMILI:
Release No. 087
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Juni 7, 2012
WAZIMBABWE KUCHEZESHA TAIFA STARS, GAMBIA
Waamuzi kutoka Zimbabwe ndiyo watakaochezesha mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia hatua ya makundi Kanda ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Gambia itakayochezwa Juni 10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) mwamuzi wa kati atakuwa Ruzive Ruzive. Waamuzi wasaidizi ni Salani Ncube na Edgar Rumeck wakati mwamuzi wa akiba ni Norman Matemera.
Kamishna wa mechi hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni ni Fanie Wallace Mabuza kutoka Swaziland wakati mtathmini wa waamuzi (referee assessor) ni Ali Baligeya Waiswa.
Waamuzi hao watawasili nchini kesho (Juni 8 mwaka huu) saa 1.20 usiku kwa ndege ya Kenya Airways wakati Kamishna wa mechi hiyo atawasili siku hiyo hiyo saa 12.50 jioni kwa ndege ya South African Airways. Mtathmini wa waamuzi atatua pia Juni 8 mwaka huu saa 7.55 mchana kwa ndege ya Kenya Airways.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inaendelea na mazoezi leo saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam chini ya Kocha Mkuu Kim Poulsen.
GAMBIA KUWASILI LEO USIKU
Timu ya Taifa ya Gambia (The Scorpions) ambayo awali ilikuwa iwasili nchini leo (Juni 7 mwaka huu) saa 1.40 asubuhi sasa itawasili leo saa 9.20 usiku kwa ndege ya Kenya Airways tayari kwa ajili ya mechi dhidi ya Taifa Stars.
The Scorpions ilipaswa kubadili ndege Dakar, Senegal jana usiku lakini kukawa na ucheleweshaji (delay), hivyo ikashindwa kuwahi Nairobi, Kenya ambapo ingeunganisha kwa ndege ya alfajiri kuja Dar es Salaam.
Kikosi cha timu hiyo chenye wachezaji 22 wakiwemo tisa wanaocheza mpira wa kulipwa nje ya nchi hiyo kitafikia kwenye hoteli Sapphire iliyopo Mtaa wa Lindi na Sikukuu eneo la Kariakoo.
Wachezaji walioko katika msafara huo ni Musa Camara, Abdou Jammeh, Momodou Futty Danso, Lamin Basmen Samateh, Ousman Koli, Pa Saikou Kujabi, Mustapha Kebba Jarju, Yankuba Mal Ceesay na Demba Savage.
Wengine ni Saihou Gassama, Alieu Darboe, Momodou Ceesay, Pa Modou Jagne, Tijan Jaiteh, Bubacarr Sanyang, Christopher Allen, Musa Yaffa, Sulayman Marr, Mamut Saine, Hamsa Barry, Ali Sowe, Omar Colley na Saloum Faal.
PROGRAMU YA MAZOEZI YA GAMBIA
IJUMAA JUNI 8
01.00 asubuhi Mazoezi- Uwanja wa Karume
10.00 jioni   Mazoezi- Uwanja wa Taifa
JUMAMOSI JUNI 9
04.00 asubuhi  Mkutano na Waandishi wa Habari- Ukumbi wa TFF
10.00 jioni  Mazoezi- Uwanja wa Taifa
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Source: sokainbongo.com

Thursday, May 10, 2012

0

TBL kudhamini Taifa Stars dola million 10 kupitia bia ya Kilimanjaro!

Posted in , , , ,
Kampuni ya Bia Tanzania Limited (TBL) pamoja na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) zimesaini mkataba ambapo TBL itakuwa mdhamini mpya wa Timu ya Taifa-Taifa Stars.
Kwa mujibu wa maridhiano hayo, TBL kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager itaidhamini Taifa Stars kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo.
Mkataba huo ulisainiwa jijini Dar es Salaam jana mbele ya maafisa waandamizi wa TFF, wawakilishi kutoka TBL, vyombo vya habari na wadau wengine wa soka nchini Tanzania.
Hii ni mara ya kwanza kwa kampuni hiyo kubwa ya bia kutoa udhamini kwa timu ya taifa, hata hivyo huko nyumba TBL iliwahi kushiriki katika udhamini wa masuala ya soka kwa miaka minne nyuma huku ikidhamini Taifa Cup na vilabu vikubwa vya Simba na Yanga.
Akizungumza katika hafla hiyo ya kutiliana saini, Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Robin Goetzsche alisema udhamini huoi utafungua mwanga mpya katika medani ya soka nchini Tanzania.
“Tunasaini mkataba wa miaka mitano wenye thamani ya dola za Marekani milioni 10 na katika kipindi chote hicho kaulimbiu yetu itakuwa “Fikisha Soka ya Tanzania Katika Kilele cha Mafanikio” na kutupa kila sababu ya kujivunia kilicho chetu
Tuna matarajio makubwa sana na timu ya taifa kwani tunaamini kuwa ina uwezo wa kufanya maajabu, na kama nilivyosema awali, hili ni pambazuko la kuelekea mafanikio. Uwekezaji wetu umelenga katika kuhakikisha kambi za mazoezi zinaimarishwa, wachezaji watalala katika hoteli zenye ubora wa juu zenye zaidi ya ngazi tatu zilizo na bwawa la kuogelea na vifaa vya mazoezi, vifaa vinaboreshwa na pia vijana watapata fursa za kucheza mechi nyingi za kirafiki ili wajipime nguvu na kupata uzoefu zaidi na timu zinapata basi jipya la kisasa.
Kwa kuongeza, alisema udhamini wao utasaidia katika:
a) Ununuzi wa vifaa mbalimbali vya kisasa.
b) Mafunzo kwa wafanyakazi wa TFF ndani na nje ya nchi.
c) Uendeshaji wa tovuti ya TFF.
d) Semina na mikutano ya utawala bora.


Grand Malt, ambacho ni kinywaji kisicho na kilevi kitakuwa kikidhamini Ligi Kuu ya Zanzibar. Hii ni kuonyesha namna TBL ilivyo mstari wa mbele katika kuhamasisha soka si kwa Bara tu bali na Visiwani. Mkataba huu ni wa miaka mitatu na utamalizika mwaka 2015 ukiwa na thamani ya Sh milioni 140 kila mwaka. Kwa upande wake, Rais wa TFF, Lodger Tenga aliahidi kutoa ushirikiano thabiti kwa wadhamini wapya kwani anaamini mkataba huo utaleta mapinduzi chanya katika soka nchini Tanzania. Hata hivyo, aliwaomba Watanzania kuwa na uzalendo kwa timu yao ya taifa kwa kuishangilia kwa wingi kwenye mechi zake.
“Hakuna jema lolote kama tutakuwa na ari ya kuzishabikia timu za nje badala ya ya timu ya nyumbani, wachezaji wetu wanahitaji moyo wawapo uwanjani kwa kushangiliwa ipasavyo,” alisema.
Naye Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe alisema udhamini huo ni wa thamani na kwamba watafanya kila liwezekanalo kuisaidia TFF kuhakikisha kuwa Taifa Stars inang’ara katika anga za kimataifa na hivyo kukidhi kiu ya Watanzania.
“Hii ni mara ya kwanza kuidhamini Taifa Stars na tunataka kuja kwa mtindo mpya na wa kipekee, tunataka Watanzania wajivunie timu yao kwa sababu ukarimu huanzia nyumbani…tuwape moyo wachezaji wetu na tujivunie kilicho chetu,” alisema.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ