KAGAME CUP: Klabu 12 kushiriki Dar, kugharimu Milioni 900!!
Posted in Kagame Cup, Simba SC, Yanga SC
Katibu Mkuu wa CECAFA, Baraza la Vyama
vya Soka Afrika Mashariki na Kati, Nicholas Musonye, amesema Timu 12
zitashiriki Mashindano ya Mwaka huu ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na
Kati, Kagame Cup, ambayo yatagharimu Dola 600,000 (zaidi ya Shilingi
Milioni 900) na yatachezwa Jijini Dar es Salaam kuanzia Juni 23 hadi
Julai 7.
Mwaka jana, michuano ya Kagame Cup, iliyodhamini wa na Kampuni ya Bia Tanzania TBL kupitia Bia yake ya Castle kwa Sh300 milioni, Ilifanyika Jjini Dar es Salaam na Yanga kuibuka Bingwa kwa kuichapa Simba kwa bao 1-0 kwa bao la dakika za majeruhi lililofungwa na Straika kutoka Ghana, Kenneth Asamoah.
Musonye alisema Ratiba ya michuano hiyo, ambayo itaonyeshwa moja kwa moja na Kituo cha TV cha Supersport, itapangwa baada ya Timu zote 12 kuthibitisha ushiriki wao.
Akifafanua kwa nini Tanzania inakuwa Mwenyeji wa Mashindano hayo kwa Miaka mitatu mfululizo, Musonye alisema ni sababu ya mafanikio yaliyopatikana katika mashindano ya Kombe la Chalenji na Kombe la Kagame Mwaka jana pamoja na uhakika wa udhamini.
Kawaida, zawadi za Washindi zimekuwa zikitolewa na Rais wa Rwanda, Paul Kagame, ambae ndie ametoa Kombe na pia hutoa Tuzo ya Dola 60,000 kwa Bingwa.
Mwaka jana timu 13 zilishiriki, ambazo ni Ulinzi (Kenya), Ports (Djibouti), St George (Ethiopia), El Merreikh (Sudan), Red Sea (Eritrea), Elman (Somalia), APR na Etincelles (zote toka Rwanda), Bunamwaya (Uganda), Vital'O (Burundi), Simba na Yanga za Tanzania

More News: www.sokainbongo.com
0 Maoni/comments: