Rapper wa kundi la Weusi, Lord Eyez amewataka wananchi kuiachia mahakama iamue hatma yake na kujizuia kumuita mhalifu kwakuwa bado chombo hicho cha sheria hakijatoa maamuzi yake.
Rapper huyo ametoa wito huo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa hoteli ya Double View iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam.
Lord Eyez alikuwa ameambatana na mwanasheria wake Peter Kibatala pamoja na members wenzie wa Weusi, Nikki wa Pili na G-Nako.
“Naomba tuipe muda mahakama naamini ntapata haki yangu na uhakika Mungu yuko pamoja nami na mafans wangu poleni sana naomba mnipe nafasi yenu nipate haki yangu niendelee kulisha madini sababu ninayo mengi lakini nimekuwa na misukosuko mingi ambayo Mungu pekee ndio anaweza kujua ukweli,” alisema Lord Eyez.
Unajua maisha yana milima na mabonde ndio nimekuwa mtoto wa kiume naweza kuvumilia lakini ni wakati mgumu sana kwangu na vitu ambavyo sijazoea, nimepitia maisha ambayo sijawahi kuyaona mengine,lakini all in all King Eazy kuna trak mpya inakuja so keep tuning, media support nini cause am not a criminal.”
Kwa upande wake mwanasheria wake ambaye alisema lengo la kukutana na waandishi wa habari ni kuweka ‘record’ sawa tofauti na watu walivyolisikia tuki hilo, alidai kuwa tarehe 20 mwezi uliopita Lord Eyez alipigwa simu na mtu ambaye walikuwa wamefahamiana kwa muda mfupi na kuamini kuwa alimtaka kwenda kuzungumza masuala ya kijamii.