Next
Previous
Showing posts with label Ally Kiba. Show all posts

Friday, August 2, 2013

0

ALLY KIBA KUFANYA SHOW YA KIHISTORIA YA MWAKA

Posted in

NDANI ya wiki moja ijayo, Sikukuu ya Idd Mosi itaadhimishwa ambapo sambamba na hilo, mkali wa wakali kwenye Bongo Fleva, Ali Kiba anatarajia kuiandika historia kubwa ya mwaka katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem, jijini Dar.
Mkali huyo anayetamba na nyimbo kali kama Dushelele, Single Boy, Nakshi Nakshi, Mac Muga, Cinderella na Karim amesema ataitumia shoo hiyo kuweka heshima yake kwa levo za kimataifa hivyo mashabiki watarajie maajabu.
“Ni shoo ambayo nitaandika historia ya mwaka, mara ya mwisho Dar Live nilifanya shoo mwaka jana lakini mwaka huu itakuwa balaa zaidi,” alisema Kiba.
Mratibu wa Dar Live, Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’ amesema siku hiyo itakuwa ni shangwe mwanzo mwisho kwani asubuhi kutakuwa na shoo maalum ya watoto kabla Kiba, Wanaume Family (Chegge, Temba, Aslay na Bi. Cheka), Bendi ya Mapacha Watatu na H. Baba hawajalivamia jukwaa kuanzia nyakati za jioni.

Sunday, June 23, 2013

0

NEW VIDEO: ABDU KIBA FT. ALLY KIBA - KIDELA

Posted in ,

Saturday, May 18, 2013

0

LIST YA WATU MAARUFU KUTOKA KENYA NA TANZANIA, AMBAO WAMETAJWA NA MTANDAO WA KENYA KUA NI MAFREEMASONS | WACHAFUZI WA MAJINA YA WATU |

Posted in , , , , ,
Inawezekana kila kitu kina wakati wake, kuna muda watu walikuwa wakisikia neno ‘Freemason’ ama ‘Illuminate’ kama inavyojulikana nchini Kenya wengi walikuwa wanaiona ni habari kubwa, lakini kwa sasa hivi inaweza kuchukuliwa kama sio big deal.

Sababu ni ile ile kuwa wengi wanaoendelea kwa haraka ama kuwa juu katika kile wanachokifanya basi utasikia huyo ni member wa Freemason, kwa upande wa Marekani wanasema ‘he/she just sold her/his soul to the devil’.  Japo kwa upande wa Marekani wapo wanaokiri kufanya hivyo kweli, ila kwa Africa Mashariki hakuna msanii aliyewahi kukiri.
Lakini yote hayo ni kama yanakanganya na kuonekana kama hayana mantiki hasa pale ambapo vithibitisho vya kinachoongelewa huwa havileti mantiki ya moja kwa moja. Pengine watu wanatafuta pesa kwa bidii na kumuomba Mungu lakini kwa kuwa kwenye mstari wa juu wanajikuta wanahisiwa kuwa member wa secret society (Freemason). Oh..au labda ndo vile kwa upande mwingine lisemalo lipo na kama halipo laja !
Tunathubutu kuziita blaa blaa kwa upande mwingine, lakini tukiweka kwenye mabano kuwa inaweza kuwa na ukweli, who knows!
Mtandao wa malimwengu wa nchini Kenya huenda ukawa na mfano mzuri wa kile nilichokitaja hapo juu, mtandao huo kupitia mwandishi wake imetaja majina ya wasanii wa Tanzania na Kenya wanaosemekana kuwa ni wafuasi wa Freemason, lakini kizuri zaidi ni kwamba mtandao huo umejaribu kuonesha vithibitisho na kushindwa kupata jibu la moja kwa moja kwa nini wasanii hawa wamekumbwa na hili. Inabaki hivyo hivyo kuwa tetesi tu.
Hawa ni wasanii waliotajwa na maelezo yanayowahusu:
TANZANIA:
1.Naseeb Abdul Jumaa (Diamond Platinum)
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgGeqkjTssTPVEn-y8y0T9B9xxMaWSQ1GrqKKJUBNRefij-CUg4Tkfq9ZQRgeX5-G4EyJbSu3qdQ9Piwa54oeKp77YZ5PotfboxVflRImxBnIzfftBd4B0thxnHVV7x4FEHBQg-tIYxbW0/s1600/DiamondFreemason.jpg
Picha aliyopiga mwaka jana akiwa na mzungu anaeaminika kuwa ni moja kati ya viongozi wa Freemason wakiwa wameweka pozi na kuonesha ishara inayooaminika kuwa ni ya Freemason, na kwamba alipoulizwa yeye alisema hakufahamu kama alikuwa anaelekezwa kupiga picha kwa pozi la ki-freemason. Kwa mujibu wa mwandishi anaona inaweza kuwa kweli kwa sababu anaonekana kuenjoy!

Saturday, October 6, 2012

0

UKIPEWA NAFASI YA KUCHAGUA MTU WA KUPIGA COLLABO NA RICK ROSS HAPA TZ UTAMPA NANI???

Posted in , , , , , , , ,
Tumekua Tukizoea Kuona Ambwene Yesaya Akipiga Collabo na Wasanii wa Kimataifa, JE INAPOTOKEA UNAPEWA NAFASI YA KUCHAGUA MTU WA KUPIGA COLLABO NA ''THE BOSS'' UTAMCHAGUA NANI??? Pah One, MwanaFA, JohMakini Mwamba Wa Kaskazini Na Weusi, FID Q, Stamina SuperMario, Godzilla, Young Dee, Diamond Platnumz, Ally Kiba AU Msanii Gaani???
#WEKA WAZO LAO HAPA>>>

Thursday, October 4, 2012

0

TULIKUA HATUJAIWEKA HII>> SHARO MILIONEA FT ALLY KIBA-CHANGANYA CHANGANYA

Posted in ,
Sharo Millionea anakuja Na Nyimbo mpya aliyoimba na Ally Kiba, Nyimbo Hii ni ya Kuchangamsha kama ilivyo kawaida ya nyimbo za Sharo Millionea.

Thursday, July 12, 2012

0

Ningependa Arusha Wawe Na Joint Nzuri Kama KIGOMA ALL-STARS, NYEUSI haitoshi.

Posted in , , , , ,
Ningependa Arusha Wawe Na Joint Nzuri Kama KIGOMA ALL-STARS, NYEUSI haitoshi.

Huu ni mwaka ambao mkoa wa Kigoma utaongelewa sana kwenye burudani. Hongera nyingi ziende kwa yule aliyekuja na wazo hili lenye thamani ambalo limeunyanyua mkoa wa Kigoma katika kipindi kifupi mno.
Tangu itoke Leka Dutigite, Kigoma imejipatia sifa kubwa kwa kujulikana miongoni mwa wasanii waliojuu kwenye muziki wa kizazi kipya nchini kuwa wanatokea huko.
Ukizungumzia Diamond Platnumz na ukaona jinsi kijana alivyofanikiwa mpaka kupiga show Big Brother, ni halali uheshimu mkoa ulio asili yake, Kigoma. Tunafahamu kimaendeleo Kigoma ni miongoni mwa mikoa iliyonyuma kwa Tanzania. Wanapaita ‘Kigoma mwisho wa reli’. Jitihada hizi za mbunge wa Kigoma kaskazini, Mheshima Zitto Kabwe kuwapa support wasanii wenye asili ya Kigoma, sasa zimegeuka mfano wa kuigwa. 
Tangu wimbo ‘Leka Dutigite’, neno la kiha lenye maana ya Acha Tujidai, Kigoma umekuwa ni mkoa unaojadiliwa sana na wapenzi wa burudani mitaani na kwenye mitandao ya kijamii. Na hapo ndo utakapogundua kuwa Tanzania hakuna ukabila. Watu wa mikoa mingine wameupenda wimbo huu na kuwapongeza wasanii hao.
Ni wimbo uliofanywa na masupastaa haswaa wa Tanzania. Diamond, Peter Msechu,Ommy Dimpoz, Baba Levo, Banana Zorro, Chege, Mwasiti, Linex, Queen Darling, Rachel na wengine wasanii waliojuu sana nchini. Ni movement ambayo ikiwa nyuma ya mbunge mwenye kipaji cha uongozi, Mhe. Zitto, inayoweza kuleta mabadiliko makubwa kwenye mkoa huo, kiuchumi na kisiasa.
Ni muungano unaoweza kupeleka maendeleo makubwa kwa kutumia mwavuli wa burudani. Ni movement ambayo itawaamsha wasanii wengine na hata watu wa kawaida kuthamini asili yao. Wanasema mtu asiyekuwa na kwao ni sawa na mtumwa. Itawaamsha wasanii waliopo Dar es Salaamn(kitovu cha tasnia ya burudani nchini) kujivunia mkoa ama hata kijiji anachotokea. Chema vizuri kuigwa.
Mikoa mingine haitakuwa na hasara ikifanya hivyo pia. Uzuri wa muungano kama huu, huchangia kukua kwa sanaa kwenye mkoa husika. Tangu Leka Dutigite itoke, kuna wasanii wengi wachanga wa mkoani Kigoma waliopata morali ya kuongeza juhudi zaidi kimuziki ili wafanikiwe na hatimaye kupewa heshima kama hiyo ya kujiunga na wakali wa mkoa huo. Japo baadhi yao kama wanavyosema kuwa Kigoma ni asili yao tu lakini hawakukulia huko, asili ipo pale pale na ni jambo la msingi kuutangaza.
Baada ya kitendo hicho, leo hii watu wengi wametamani wasanii wa mikoa yao wafanye kitu kama hicho pia. Huo ni wivu wa maendeleo kama asemavyo Monty Khatau Ezel, “Nimevutiwa na hiyo kitu, natamani ningekuwa natokea Kigoma,nina ugonjwa wa wivu wa maendeleo,najivunia kutokea kusini,LINDI wajiandae mafanikio yanawajia.”
Ibrahim Athumani Masokola naye anasema, “Nahisi katika mambo ya kuiga kwa baadhi ya watu kama waheshimiwa ni pamoja na hili analofanya mhe Zitto kwani ni njia mojawapo ya kuwafikia wananchi kwa urahisi HONGERENI SANA WOTE mlohusika kwa namna moja au nyingine.”
Naye Zulu Agrey Mnkeni anasema, “Natamani nami ningekuwa wa KIGOMA ila ndo bahati mbaya natoka KILIMANJARO naogopa kuitwa MKABILA.”
Kitendo hicho cha Mheshimiwa Zitto kuungana na wasanii ili kuutangaza mkoa wa Kigoma,kinamweka karibu zaidi na vijana waliowengi nchini na kumsafishia njia yake kwa mambo makubwa zaidi katika career yake kama mwanasiasa. Hongereni Kigoma All Stars!
Photos by: Bongo5.com

Tuesday, April 17, 2012

0

KILI MUSIC AWARDS 2012

Posted in , , , , ,
♦Kili Music Awards Winners♦
1. Wimbo Bora Wa Reggae- Arusha Gold by Warriors from East
2. Wimbo Bora wa Dancehall- Maneno Maneno by Queen Darlin'
3. Wimbo Bora Zouk Rhumba- Dushelele By Ally Kiba
4. Wimbo bora wenye vionjo vya asili- Vifuu Tundu By A.T
5. Wimbo Bora wa Taarab- Nani kama Mama By Isha Mashauzi
###########A.B93##########
6. Wimbo Bora wa Kiswahili(Bendi)- Dunia Daraja By Twanga Pepeta
7. wimbo Bora wa Afro Pop- Hakunaga By Suma Lee
8. Wimbo Bora wa R&B- My Number 1 Fan By Ben Pol
9. Wimbo Bora wa Hip Hop- Mathematics By Roma
10. Msanii Bora Anayechipukia- Ommy Dimpoz
*********A.B 93*****
11. Rapa Bora wa Bendi- Kitokololo
12. Msanii Bora wa Hip Hop- ROMA
13. Wimbo Bora wa Kushirikiana- Nai Nai By Ommy dimpoz ft Ally Kiba
14. Wimbo Bora Afrika Mashariki- Kigeugeu By Jaguar
15. Mtumbuizaji Bora wa kike- Khadija Koppa
16. Mtumbuizaji Bora wa Kiume- Diamond Platnumz
17. Mtunzi Bora wa Mwaka- Diamond
18. Producer Bora Wa Mwaka- Maneck
19. Video Bora ya Muziki ya mwaka- Moyo Wangu By Diamond
20. Wimbo Bora wa mwaka- Hakunaga by Suma Lee
21. Hall Of Fame(Taasisi)-JkT Taarab
-Hall of Fame(Binafsi)-King Kiki
-Hall of Fame(Binafsi)-Remmy Ongalla
22. Mwimbaji Bora wa Kike- Lady Jay Dee
23. Mwimbaji Bora wa Kiume- Barnaba
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ