Next
Previous
Showing posts with label Diamond Platnumz. Show all posts

Sunday, February 2, 2014

0

ONA JINSI JOKATE ALIVYOMMWAGIA MAHELA WEMA SEPETU HUKU WAKICHEZA NGOLOLO HUKO ARUSHA

Posted in , , , ,
Hii ilikuwa usiku wa jana tarehe 1 pale Triple A Club iliyopo pande za Arusha, ilikuwa ni show ya Ma divas ambapo walikuwepo kama Wema Sepetu, Kajala, Aunt Ezekiel pamoja na Jokate ambaye hakuwepo kwenye banners. Mara wakazi wa Arusha ndipo walipoanza kupiga shangwe pale Jokate alipoanza kumwagia mijihela mwanadada Wema stejini huku DJ akiwapigia wimbo wa Diamond unaoitwa My Number One.

Wednesday, January 8, 2014

0

NEW TRENDING BONGO VIDEOS

Posted in , ,

Friday, December 20, 2013

0

VIDEO YA MY NUMBER 1 REMIX KUONEKANA KWA MARA YA KWANZA NA WATOTO YATIMA - DIAMOND

Posted in
http://baabkubwamagazine.com/wp-content/uploads/2013/12/Davido_n.jpgKwa mara ya kwanza nchini Tanzania, Naseeb Abdul a.k.a Diamond ameweka wazi kuwa video yake ya ‘My Number One rmx’feat Davido iliyofanyika nchini Nigeria watu wa kwanza kuitazama watakuwa ni watoto yatima na watu wasiojiweza kabla ya mtu watu wengine.


Akiongea ndani ya 255 ya XXL- Clouds fm amesema kuwa video hiyo itatazamwa kwanza na watoto yatima na watu wasiojiweza ili kuwapa fursa sawa na watu wengine na sio kila siku kuwasahau na kuwatenga bali kuwa nao karibu kwa kila kitu.
Hali hii itakuwa ni muendelezo wa Diamond kuweka rekodi mpya kila siku kwenye muziki wa Bongo Fleva. Baabkubwa inamtakia mafanikio mema na kuipeleka Bongo Fleva kwenye level nyingi ne kubwa kimataifa zaidi.

Thursday, October 10, 2013

0

DIAMOND PLATNUMZ NA WEMA SEPETU WAKIWA LOCATION CHINA

Posted in ,

Thursday, September 5, 2013

0

SHEDDY CLEVER AKATA MZIZI WA FITINA JUU YA BITI YA NYIMBO MPYA YA DIAMOND PLATNUMZ

Posted in , ,
Baada ya sakata la kuibiana nyimbo lilichokua takribani siku mbili kati ya msanii Diamond Platnum na Dayna Nyange,producer Shedy  ameamua  kukata  mzizi  wa  fitina  kwa  kuuanika  ukweli  wa  mambo....

Akiongea  na  #Team tizniz,Shedy  amefunguka  kama  ifuatavyo:

“Beat hii nilitengeneza mimi kwa idea zangu mwenyewe. Alikuja Dayna akaupenda ule mdundo na mimi sikumnyima , akafanya demo lakini hakulipia kitu.

"Sasa ikapita zaidi ya miezi sita kila nikimuliza vipi anasema bado atakuja kufanya.Kuna siku Diamond akaja studio ,akataka kusikia midundo  niliyonayo.

"Bila  hiyana, nilimchezea midundo mbalimbali  kama  mteja,  ila jamaa akavutiwa sana na ule mdundo ambao Dayna aliufanyia demo.

"Baada  ya Diamond   kuupenda  mdundo  huo, niliamua  kumpigia simu Dayna na kumuelezea kwamba Diamond kapenda kufanya kazi katika ile beat,Dayna akakubali kabisa,

"Sasa nashangaa yeye kusema diamond kamuibia wakati alikubali  yeye  mwenyewe."

Wednesday, September 4, 2013

0

HUU NDO WIMBO WA DAYNA AMBAO DIAMOND AMEJIHALALISHIA

Posted in ,



Inasemekana awali Dayna alimtaka Diamond wakafanye wimbo kwa Shedy, Diamond akakubali, akaskiliza mdundo na kumuahidi Dayna kwamba wangefanya wote. Lakini baadae Diamond akamrubuni Shedy na kumwambia ile bit ampe na aachane na kazi ya Dayna.

Tuesday, September 3, 2013

0

DAYNA ALALAMIKA KUWA DIAMOND KAMWIBIA BEAT, KATIKA WIMBO "MY NUMBER 1"

Posted in ,


Nyota wakike wa muziki wa kizazi kipya anayefahamika kwa jina Dayna Nyange ameibuka na malalamiko zidi ya mwanamuziki Naseeb aka Diamond Platnumz.
Baada ya Dayna kuomba collabo kwa Diamond Platnumz na kukubaliwa na msanii huyo kutoka Wasafi Entertainment, kwa kigezo cha kumuachia wimbo Diamond ili aweze kuufanyia mazoezi.

Kwa sasa imekuwa ndivyo sivyo kwa Wasanii hao kuibiana kazi baada ya tetesi hizo mwandishi wa Baabkubwa ikamvutia waya Dyana Nyange ili kujua ukweli wa tetesi hizo”Mimi mashairi si yangu bali beat ndiyo yangu na wimbo niliutengenezea studio ya Burn Record chini ya producer Shedy Clever, baada ya kukamilika nilishauriana na producer mtu wa kushirikiana nae ndiyo akaniambia nifanye na Diamond Platnumz, so nikamtafuta Platnumz akaniambia niende kwake ndipo nikaamuamua kumuachia wimbo wangu baada ya kukutana nae”.

Baada ya hapo alitafutwa producer Shade crever na Diamond hawakupatikanika kwenye simu zao.

Monday, September 2, 2013

0

VIDEO MPYA TOKA KWA MSAFI: DIAMOND PLATNUMZ - MY NUMBER ONE (OFFICIAL VIDEO)

Posted in , ,

Friday, August 30, 2013

0

PHOTOS: JINSI UZINDUZI WA VIDEO MPYA YA DIAMOND ULIVYOFANYIKA NA RED CARPET

Posted in ,
Napenda kutoa Shukrani zangu za dhati kwa
Mwenyezi Mungu kwa kuweza kunifanikisha
hadi kufikia hapa muda na wakati kama huu...
Usiku wa tarehe 29.08.2013 nilikuwa na Launch
video yangu inayotambulika kama
My Number One,nilianda tafrija fupi kwenye
 hoteli ya nyota tano,Serena Hotel jijini Dar Es Salaam


,ili kuweza kujumuika
na ndugu,jamaa na marafiki wa karibu kuwonesha
kile kitu ambacho nimetumia muda mwingi
kutengeneza,kabla ya kuiachia nikaona vyema
waipitie kabla mtu wangu wa kweli ujaicheki.


Shukrani zangu nyingie ziwaende kwa wageni waalikwa 
wote kufika na kutoa support na kushow love kwangu
Sina cha kuwalipa bali kusema asante na mzidi kutegemea
kazi nzuri toka kwangu...

Napenda kuwashukur wasanii wenzangu waliofika
kuangalia video yangu na kuzishukur media zote
na Blogs zote zilizofika kuakikisha wakipata
matukio muhimu kabisa.

Mtu wangu wa kweli unaweza ukache Exclusive Photo kwaajili yako
ujione kilichojiri usiku wa My Number One video Launching 
Serena Hotel.
0

BIFU LA NAY WA MITEGO NA MADAM RITHA NI STORI ZA MTAANI: ANGALIA WAKIWA PAMOJA

Posted in , , ,

Takribani yapata wikii ya tatu baada ya Msanii
Nay wa Mitego kuachia kibao chake kinachotamba kama
Salamu zao....ndani ya nyimbo hiyo ametoa
kama kufikisha ujumbe kwa watu kadhaa,

Thursday, August 29, 2013

0

DIAMOND PLATNUMZ AMZAWADIA MZEE NGURUMO | HII NDO ZAWADI ALIYOMPATIA

Posted in ,
 
Msanii Diamond Platnum amefanya kufuru usiku huu kwa kutoa zawadi ya Gari kwa Mzee Ngurumo Mwanamziki wa miaka mingi na mkongwe nchini aliyestaafu majuzi kufanya kazi za mziiki.

Tukio hilo limetokea usiku huu ndani ya ukumbi wa SERNA HOTELkatikati ja jiji la DSM ambapo Diamond Platnum anazindua video yake ya wimbo wa #one fun.
Kiingilio cha show hiyo ni bureeeeeeeeeeeee....LAKINI UMEALIKWA?
Picha za tukio zima nitawaletea hivi punde.

Mzee Ngurumo amesema"Haamini macho na masikio yake,hanachakusema zaidi ya ASANTE kwa msanii huyo"Lakini pia amesema hajui hata mke wake atasemaje baada ya kumwona akiingia na gari ndani ya nyumba yake.
Mzee ngurumo amekuwa na matatizo ya kiafya siku za karibuni nakupelea kustaafu mziki kabisa.Wazee wa msondongoma ndio wanajua makali ya Mzee Ngurumo.

Wednesday, August 28, 2013

0

DIAMOND PLATNUMZ KUZINDUA VIDEO YAKE HAPO KESHO

Posted in ,
Siku ambayo mimi binafsi na wewe tumekuwa tunaisubiria sasa naona Nuru inaniangazia. 29.08.2013,Kuanzia saa 1 jioni hadi saa 3 usiku ndani ya SERENA HOTEL ntakuwa nikiachia Live video yangu mpya


itakayotambulika kama #MYNUMBERONE….

Kumbuka Party hii ya Launching Premier ya My Number One aina Kiingilio ni Special kwa waalikwa tu

Wednesday, August 21, 2013

0

ALICHOKISEMA DIAMOND PLATNUMZ BAADA YA KUHUSISHWA NA MADAWA YA KULEVYA

Posted in , , ,
  


MSANII Wa Muziki wa Bongofleva mwenye jina kubwa Town na mwenye Mkwanja mkubwa hapa nchini Nasseeb Abdulmaliki “Diamond Platnumz” amejitokeza na kukanusha kuwa hahusiki na biashara ya madawa ya kulevya.
Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na taarifa za Diamond kujihusisha na biashara hiyo hasa kutokana na ukaribu wake na wafanyabiashara wakubwa wa dawa za kulevya wenye maskani yao nchini Afrika Kusini.

 Taarifa zaidi zinasema ni wafanyabiashara hao waliohusika kwa karibu kuusafirisha mwili wa marehemu Albert Mangwair, aliyefia huko huko Afrika Kusini ambaye taarifa za kifo chake ziligubikwa na matumizi ya madawa ya kulevya.

Akikanusha taarifa hizo Diamond amesema  :

“Ni kweli mimi nina pesa za kutosha kuniwezesha kuishi maisha ninayotaka lakini sijawahi kujihusisha na biashara hiyo....

"Kufanya kazi kwa bidii kunalipa na kazi yangu inaonekana na ndiyo inayoniwezesha kuwa na fedha ambazo leo watu wameanza kuzitilia shaka. Sielewi nia ya watu hawa ni nini?”

Taarifa za Diamond kuhusishwa na mtandao huu zimeanza kushika kasi kufuatia miongoni mwa watu wake wa karibu kuonekana wakiwa karibu sana na akina Agnes Gerald “Masogange” (25) na Melisa Edward (24) kwenye uwanja wa kimataifa wa ndege wa Mwalimu JK Nyerere wa Dar es Salaam kabla hawajapanda ndege kuelekea Afrika Kusini ambako walikamatwa.
0

TAARIFA JUU HABARI YA DIAMOND PLATNUMZ KUJIHUSISHA NA MADAWA YA KULEVYA

Posted in , ,
Kutoka Jamii Forums

Mwanamuziki Nasseeb Abdulmaliki, maarufu zaidi kwa jina la Diamond
*Utajiri, safari zake nje ya nchi vyatiliwa shaka
*Ahusishwa na mtandao hatari wa Masogange
KWA mara ya kwanza tangu lilipoibuka sakata la watu maarufu kujihusisha ama na utumiaji au usafirishaji wa dawa za kulevya, jina la mwanamuziki anayeaminika kuwa na ukwasi mkubwa kwa sasa hapa nchini, Nasseeb Abdulmaliki, maarufu zaidi kwa jina la Diamond, limeanza kutajwa kuwa ni miongoni mwa vigogo wa ‘unga.’

Tayari mjadala mkubwa wa chini chini umeibuka kwa watu mbalimbali wakiwemo mashabiki wake, na taarifa ambazo zimelifikia MTANZANIA Jumatano kutoka vyanzo mbalimbali zimedai kuwa, mwenendo wa maisha ya Diamond sasa unachunguzwa na baadhi ya maofisa wa vyombo vya dola vya ulinzi na usalama.

Kutajwa kwa jina la Diamond katika sakata hili, kunatiwa nguvu zaidi na mwenendo binafsi wa maisha wa msanii huyo maarufu wa muziki wa kizazi kipya, unaokwenda sambamba na ukwasi mkubwa alioupata katika kipindi kifupi.

Sunday, August 11, 2013

0

HII NDO THAMANI YA PETE, CHENI, SAA NA BLING NYINGINE ZA MSANII DIAMOND PLATNUMZ | NOOMA

Posted in ,
Akihojiwa juzi kwenye kipindi cha The Trend cha NTV, mtangazaji wa show hiyo Larry Madowo aliuliza thamani ya bling alizokuwa amevaa.

“It’s a bit expensive,” alijibu Diamond huku akizishika bling hizo.

“Kama hii na hii it’s about dola 2000 something au 1,500, hii peke yake dola 2,000.”

Hata hivyo zingine alishindwa kukumbuka bei yake japo kwa kuangalia saa yenye diamond aliyokuwa nayo, pete zingine mbili za dhahabu na almasi na cheni mbili kubwa za dhahabu gharama yake kwa ujumla inaweza kufika dola 15,000 ukijumlisha na hizo zingine alizotaja gharama yake.

“Zina rates tofauti lakini ni gharama kidogo,” alisema staa huyo.

“Zina ishara? Maanake wengine wanaweza kusema ni Illuminati ama nini,” aliuliza Larry.

“Sidhani mimi navaa tu hii diamond ni jina langu, hii crown as mtu anayelead, kuna diamond nyingi hapa, hii ina alama flani kama ya batman as am flying,” alijibu Diamond.

Aidha Diamond alimtaja Usher Raymond kama msanii anayemtazama na kufuata nyayo zake zaidi.

“I don’t know men, namuona kama anajua sana anachokifanya, tangia nilipokuwa nikimfuatilia mpaka leo. Unajua wanamuziki wengi akitoka mwanamuziki flani yeye anapotea, Usher Raymond yupo. Ukiangalia vitu vyangu mimi namuiba sana.

Thursday, August 8, 2013

0

NEW VIDEO: NAY WA MITEGO FT. DIAMOND PLATNUMZ-MUZIKI GANI PART II

Posted in ,
0

PICHA ZA DIAMOND NA WENZAKE WAKIWA WAMEAHIRISHA SAFARI KUTOKANA NA MOTO ULIOWAKA AIRPORT JANA

Posted in ,


Tuesday, August 6, 2013

0

DIAMOND PLATNUMZ AFANYA KUFURU SOUTH AFRICA: HII NDO CIDEO ANAYOFANYA

Posted in ,


Bongo Flava Prince, Diamond Platnumz yupo nchini Afrika Kusini kishule na kikazi pia. Staa huyo wa Kesho ameshoot video ya wimbo wake mpya ambao bado haujulikani ni upi mpaka sasa.

Hata hivyo tofauti na video zake za awali, hii mpya amekata kisu kirefu zaidi kwa kushoot na miongoni mwa gari yenye thamani zaidi duniani, Ferrari. Cha kufurahisha zaidi ni kuwa gari hiyo inayotengenezwa na Waitaliano, imewekewa namba za gari binafsi kwa kuandikwa ‘Platnumz’ na Wasafi’.

Monday, July 22, 2013

0

NYIMBO YA DIAMOND ANAYOZUNGUMZIA KIFO CHAKE... KUTOKA HIVI KARIBUNI??

Posted in ,
 


One of my songs,always gets me crying whenever I listen to it, how I wish u would hear it, but then again I have no clue as to when I will release it... ‪#‎WCB‬-Diamond Platnumz

Wednesday, July 17, 2013

0

KUMUOMBA DIAMOND MSAMAHA KUPITIA TWITTER NI UTOTO - ASEMA PREZZO

Posted in ,


Rapcellency, Prezzo amesema hawezi kumuomba msamaha Diamond kwenye Twitter kwakuwa anaamini hakuna alichomkosea na ni jambo la kitoto.
Akiongea jana  mchana kwenye kipindi cha Mambo Mseto cha Radio Citizen, kinachoendeshwa Mzazi Willy M. Tuva, Prezzo amesema Diamond ndiye aliyemchokoza baada ya wasanii hao kutumbuiza mwanzoni mwa mwezi huu kwenye tamasha la Matumaini.
 Prezzo anadai aligundua kuwa Diamond alimponda kwenye magazeti ya Tanzania kuwa hamwezi kwa lolote kwenye muziki.

“Mimi sipendi kuwa na adui kwa sababu muziki unafaa kuleta muungano, sa me nikashangaa mbona huyu brother ananiingilia na huku sikumbuki kumkosea wala hatujawai kukutana ana kwa ana,” alisema Prezzo.

“Mtu yeyote anamjua Prezzo ni kama rattle snake, ukimchokoza you have to get prepared to be bitten.”
Rapper huyo aliendelea kudai kuwa alimpigia simu Diamond lakini hakupokea na ndio maana aliamua kumdiss kwenye Twitter.
   “Jamaa hakupokea simu nikaona ah! Basi liwalo na liwe, nikadecide ku-air my views.”

Hata hivyo Prezzo amesema hawezi kumuomba msamaha Diamond kwenye Twitter kama anavyomtaka afanye.
   “Unaona kwa saa hizi akianza kusema aende kwa Twitter aniombe msamaha, maisha huwa hayaendi hivo…kwa hivyo vitu vingine naona ni kama ni utoto unaingilia kati, kwani yeye kusema niombe msamaha kwa Twitter….niombe msamaha kwa kosa gani? Kusema ukweli,unajua mimini msema ukweli, mimi kuomba msamaha kwa Twitter naona kidogo ni utoto.”

Hata hivyo Prezzo amesema hataki beef na Diamond kwasababu anamheshimu na amemshukuru Willy Tuva kwa kujaribu kuwasuluhisha.
  Source: Mambo Mseto (Radio Citizen), Ghafla Kenya


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ