Next
Previous
Showing posts with label Tash. Show all posts

Wednesday, August 21, 2013

0

TASH WA MULE MULE aka MASAI TOZI, KUACHIA NGOMA MPYA HIVI KARIBUNI

Posted in


Mwanamuziki anaetamba na style yake ya Mulemule, Allan Elirehema aka Tash baada ya kutamba na ngoma zake kibao kama vile Chapia, Barida, Unagundu na nyingine kibao.

Kwa sasa anakuja na ujio wa ngoma mpya inayofahamika kwa jina la ‘AU’ wimbo huo ameufanyia katika studio ya Defetality Rec. Chini ya producer ‘Mensen Selekta’.

Tash anatarajia kuiachia ngoma yake mpya tarehe 14/9/2013, Fans wa Tash tega sikio lako upate kusikia jiwe jipya.

Friday, March 29, 2013

0

NEW TRACK: TASH-UNA GUNDU

Posted in
CLICK HAPA http://hu.lk/fceaob8bllvk

Sunday, December 30, 2012

0

YALIYOJIRI 2012 KATIKA SANAA YA MUZIKI BONGO

Posted in , , , , , , ,

Muziki wa bogno umepiga hatua kubwa sana hasa katika mwaka huu. Mengi Yametokea, Vipaji vingi vimejitokeza. Mitindo mingi ya Kimziki na Dansi iliongezeka.

1. Kupaa Kwa Ommy Dimpoz
Pooooz kwa Poz...
Ommy Dimpoz Na Vanessa Mdee
Huu ulikua ni mwaka wa kijana huyu ambaye alianza kwa kutoka na Nyimbo NAI NAI iliyompa tuzo za kili kwa kumshirikisha Ally Kiba, Akaja na BAADAE, na baadae akafunga mwaka kwa nyimbo ya  ME & YOU ft. Vanessa Mdee. Kijana huyu ameepata mafanikio mengi na kupiga hatua moja ikiwa ni kufanya video nchini Afrika Kusini. Kijana huyu pia alitoa malalamiko ya kumshutumu Lord Eyez kuiba PowerWindow za Gari Lake(Rav4).



2. Kuendelea Kuvuma kwa WEUSI.
WEUSI ni Kundi Muanganiko wa wasanii wa Arusha toka kundi la N2N na RiverCamp likijumuisha Wasanii kama Lord Eyez, Joh Makini, G-Nako, Nikki Wa pili na Bonta. Kundi hili limekua na mafanikio mengi huku kashfa aliyoipata Lord Eyez, kulifanya lipate sifa mbaya na wale walioamini hilo.






3. Udhamini wa OSTAZ JUMA NAMUSOMA kwa WATANASHATI
Watanashati wamevuma sana katika mwaka huu, Wamemrudisha PnC katika Fani, Wameokoa kipaji cha Dogo Janja, Suma Mnazaleti kwa udhamini mzuri walionao. Kundi hilo lilizidi kuwa kubwa kadri mda ulivyokwenda, na wamevuma zaidi kwa nyimbo zao. Uwepo wa Marehemu Sharo Millionea na Teja Kitale uliweka uamsho katika kundi.
HONGERA OSTAZ JUMA


Saturday, October 27, 2012

0

TASH BABLENYE ft. PAPPY CATALOG-BARIDA

Posted in
 
Artist: Tash Ft Pappy Catalog
Track: Barida
Produced by Mesen Selekta
De Fatality Music
Hii ni kazi mpya ya TASH inayoitwa BARIDA. Ni nyimbo ya pili baada ya CHAPIA...  Official itatambulishwa rasmi Tarehe 26 Mwezi huu wa October Mwaka 2012..

Thursday, March 15, 2012

0

Interview With Tanzanian upcoming Artist TASH, The CHAPIA singer

Posted in , ,
Jina Kamili: ALLAN ELIREHEMA aka TASH


A.B: JE nini Asili Ya Jina TASH?
TASH: JIna limetoka kwenye CREW yake ya zamani iliyoitwa Watashi Flani. Hvyo mi nkawa naitwa A-Tash.

A.B: so kwa sasa unajihusisha na crew yoyote?
Tash: Right now nko mwenyewe coz, masela kwa sasa wanapiga ishu nyingine

A.B: Unategemea lini kutoa Album?
Tash: Kwa sasa hivi bado sijawaza sana hatua hiyo, maana bado mapema ila ntakapopanga itakua hvyo.

A.B: Muziki wa sasa unaenda na kisomo. Je umejipanga vpy kielimu au Umeshamaliza??
Tash: Suala la Elimu Muhmu hvyo najipanga kuingia chuo, ndo nasbiria mda ufike.

A.B: Pembeni ya mziki we ni mpenzi wa nin hasa??
Tash: Napenda soka sana sana, na ni shabiki wa YANGA kwa hapa nyumbani, Na MAN-UTD ulaya ila hata Movies pia.
 A.B: Hapo kwa MAnUTD tuko pamoja, ila kwa TZ mimi SIMBA.

A.B: NAni alikuvutia ukaingia kwenye Game la mziki??
Tash: Wapo wengi ila G.Nako nmetokea kumuelewa sana, maana ni mtu mwenye style yake peke yake, ila Hata Kanye West, AY, Fid Q nawaelewa sana na napenda kufata nyayo zao.

A.B: Ulivyoingia kwenye mziki wazazi walikuchukuliaje?
Tash: Hawakunielewa ila baada ya kushnda Freestyle Battle Arusha wakanielewa na sa hivi ni maSuporters wangu wakubwa.

A.B:Unaonekana umekaa sana pande za Chugga?? And unaonaje ushindani, coz upcoming artists mko wengi saana?
Tash: Kwetu ni A-Town kabisa, na ushindani ni mkubwa sana, ila tunatofautiana style ya kuimba na ubunifu, ivyo ili utoke unaitaji akili ya ziada.

A.B: Tena akili ya Chapia kama yako........ So mpaka sasa umepiga show ngapi? na unaonaje mapato yake?
Tash: Nimepiga show kadhaa kaka, ila naamini zitakuja nyingi zaidi, kwani huu ndo mwanzo, na mapato ni ya kawaida, coz ni bora kupata kidogo kuliko kukosa kabisa, naamini ntapaata zaidi ya hiki nnachokipata sasa.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ