
Mapema leo hii, kimeonekana kichwa cha habari katika moja ya magazeti ya udaku kikiongelea OMMY DIMPOZ kumkashifu/kumtusi marehemu ALBERT MANGWEA [R.I.P] … Baadae kidogo Ommy Dimpoz aliandika mtandaoni kuwa si kweli na ni story ya kutunga tu kutaka kumchafua kisanii … Ommy, “Nimesikitishwa sana na hii habari iliyotoka global publishers Wanatengeneza story ili wauze magazeti yao” … alimaliza Dimpoz na kutupia picha hii hapa …

Lakini Ommy hakuishia hapo, alionesha kukerwa zaidi na front page hiyo na kuandika sababu ya gazeti hilo kumchafua namna hiyo …
Hichi ndicho Ommy alichoandika …
“Nilipigiwa simu ya kibiashara kwa ajili ya kufanya show na global publishers kwa sababu hatukuafikiana kwenye malipo ndo wameamua kunichafua ..”
0 Maoni/comments: