Thursday, May 24, 2012

0

Dimpoz ana SHEPU ya KIKE - Cyrill

Posted in ,


Siku chache baada ya msanii Cyrill kukataliwa kugonga show pale maisha club na Baraza la sanaa (Basata) kwa maelezo kuwa si mtanzania mpaka pale alipotoa vithibitisho, mengine yameibuka.
Hili limeibuka baada ya mkali wa 'nai nai' Ommy Dimpoz kuongea kwenye mahojiano na kituo kimoja cha Radio akimkandia live Cyrill kuwa msanii huyo hafanyi show kabisaaa.
Kwa upande wake Cyrill nae ktk mahojiano na Radio moja jijini Dsm amejibu mapigo hayo na kwenda mbali zaidi na kudai kuwa Ommy Dimpoz ana tabia za kike za kuzungumza zungumza hovyo na kumtaka siku nyingine akiwa na interview ajipange sio kuropoka hovyo mambo yasiyomhusu.
" Jamaa anaonyesha ni jinsi gani amechezea madarasa machache sana tena kwa muda mrefu, tena kuna siku nilimtizama nikamuona ana shape ya kike!!!!!!
Sasa unaambiwa yote haya yametokana na kuzuiliwa kwa Cyrill kuzuiliwa kugonga ile show na BASATA last week, huku Dimpoz akidai kuwa Cyrill anamtangazia kwa watu kuwa yeye ndiye aliyepeleka taarifa Basata kuwa jamaa sio mbongo ili azuiliwe kugonga show siku hiyo ambapo Dimpoz naye alikuwa na show yake pande za Bilicanas.

0 Maoni/comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ