Takribani yapata wikii ya tatu baada ya Msanii Nay wa Mitego kuachia kibao chake kinachotamba kama Salamu zao....ndani ya nyimbo hiyo ametoa kama kufikisha ujumbe kwa watu kadhaa, lakini kuna mstari alikuwa akimuongelea Chief Judge wa EBBS & Benchmark Production Manager Madam Rita Poulsen. Kuna tetesi zilizuka kuwa Madam Rita alikuwa yupo mbioni kumfungulia mashitaka Nay wa Mitego,lakini nataka kukuambia na kukujuza kiundani kabisa kuwa amna lolote kati ya hayo ukweli ni Nay wa Mitego na Madam Rita wapo sawa kabisa na upendo umeshamiri kati yao.....
Jana Kwenye Launching Party ya video yangu iliyofanyika Serena Hotel, Madam Rita alikuwepo na Nay pia alikuwepo na muda ulipozidi kuyoyoma nilipata fursa ya kuongea nao na kunipongeza kutokana na kazi nzuri toka kwangu na kizuri zaidi niliwakuta pamoja wakiwa wanaongea......
Unaweza zicheki picha kadhaa za Nay & Madam Rita wakiwa pamoja. |
0 Maoni/comments: