Thursday, September 5, 2013

0

SHEDDY CLEVER AKATA MZIZI WA FITINA JUU YA BITI YA NYIMBO MPYA YA DIAMOND PLATNUMZ

Posted in , ,
Baada ya sakata la kuibiana nyimbo lilichokua takribani siku mbili kati ya msanii Diamond Platnum na Dayna Nyange,producer Shedy  ameamua  kukata  mzizi  wa  fitina  kwa  kuuanika  ukweli  wa  mambo....

Akiongea  na  #Team tizniz,Shedy  amefunguka  kama  ifuatavyo:

“Beat hii nilitengeneza mimi kwa idea zangu mwenyewe. Alikuja Dayna akaupenda ule mdundo na mimi sikumnyima , akafanya demo lakini hakulipia kitu.

"Sasa ikapita zaidi ya miezi sita kila nikimuliza vipi anasema bado atakuja kufanya.Kuna siku Diamond akaja studio ,akataka kusikia midundo  niliyonayo.

"Bila  hiyana, nilimchezea midundo mbalimbali  kama  mteja,  ila jamaa akavutiwa sana na ule mdundo ambao Dayna aliufanyia demo.

"Baada  ya Diamond   kuupenda  mdundo  huo, niliamua  kumpigia simu Dayna na kumuelezea kwamba Diamond kapenda kufanya kazi katika ile beat,Dayna akakubali kabisa,

"Sasa nashangaa yeye kusema diamond kamuibia wakati alikubali  yeye  mwenyewe."

0 Maoni/comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ