VIDEO YA MY NUMBER 1 REMIX KUONEKANA KWA MARA YA KWANZA NA WATOTO YATIMA - DIAMOND
Posted in Diamond Platnumz
Kwa mara ya kwanza nchini Tanzania, Naseeb Abdul a.k.a Diamond ameweka
wazi kuwa video yake ya ‘My Number One rmx’feat Davido iliyofanyika
nchini Nigeria watu wa kwanza kuitazama watakuwa ni watoto yatima na
watu wasiojiweza kabla ya mtu watu wengine.
Akiongea ndani ya 255 ya XXL- Clouds fm amesema kuwa video hiyo itatazamwa kwanza na watoto yatima na watu wasiojiweza ili kuwapa fursa sawa na watu wengine na sio kila siku kuwasahau na kuwatenga bali kuwa nao karibu kwa kila kitu.
Hali hii itakuwa ni muendelezo wa Diamond kuweka rekodi mpya kila siku kwenye muziki wa Bongo Fleva. Baabkubwa inamtakia mafanikio mema na kuipeleka Bongo Fleva kwenye level nyingi ne kubwa kimataifa zaidi.
0 Maoni/comments: