Next
Previous
Showing posts with label Barnaba. Show all posts

Wednesday, August 14, 2013

0

BARNABA NA AMINI WAANZISHA KUNDI JIPYA NJE YA THT

Posted in , ,
Wale wakali toka jumba la vipaji Tzee- THT walioishi kama pacha kwenye jumba hilo (Amini & Barnaba) wameungana na kuunda crew yao mpya kimziki iitwayo “GEMENIH” wakimaanisha wao ni kama mwezi na nyota angani. 


“Yap, Tumeungana kufanya kazi pamoja kama kundi nje ya THT tukiwa ni matunda ya THT na tumeamua kujiita hivyo kutokana na kutegemeana kwetu kwenye kazi na umuhimu wa uwepo wa kila mmoja kwenye mziki wa bongo kama umuhimu wa nyota na mwezi angani.” Barnaba alilidokeza BK.
Kundi hilo kwa sasa lina-bang hewani na ngoma yao ya ‘Why me’ huku wakiwa na mipango mingi ya utendaji wao wa kazi kama Gemenih. Pia waliongeza kitu juu ya Gemenih na THT.
“Kikubwa ni kwamba, watu wasidhani tumetoka au tuna ugomvi na THT ila tumehitimu mafunzo pale na kutunukiwa vyeti nasi ni matunda ya THT na bado tunashirikiana nao kwa kuwapa ushauri hata kuwatungia nyimbo. Kwa ufupi tumewaachia wengine nafasibaada ya sisi kufuzu mafunzo pale.” Amini aliongeza.
Gemenih ipo chini ya meneja aitwaye Moses Clemence ambaye ndiye ana-control mambo yote yahusuyo vijana hao.

Friday, July 12, 2013

0

VIDEO ILIYOSUBIRIWA KWA HAMU: Izzo Bizness feat Barnaba & Shaa - LOVE ME

Posted in , ,

Monday, June 24, 2013

0

BAADHI YA PICHA KWENYE MSIBA WA MAMA YAKE BARNABA(THT)

Posted in , ,



Msanii wa mziki wa kizazi kipya Barnaba Elias, siku ya Jumamosi alifiwa na Mama yake mzazi ambae alikuwa akijulikana kwa jina la Bi. Mariam Arubeth. Shughuli za mazishi zilifanyika siku ya Jumapili nyumbani kwa marehemu kigogo/mburahati ambapo msiba huo ulihudhuriwa na watu wengi wakiwemo wasanii mbalimbali .
IMG_0008
IMG_0015
IMG_0021

Wednesday, May 15, 2013

0

BARNABA NA LINAH HATIMAYE KUFANYA SHOW YA LADY JAY DEE | ANGALIA VIDEO WAKILIONGELEA

Posted in , ,
Zikiwa zimebaki wiki kadhaa kufikia show ya mwanadada LADY JAYDEE kufanyika, mwanamuziki BARNABA na LINAH [THT] wameongelea ushiriki wao katika MIAKA 13 ya mwanadada huyo ...
Hivi karibuni kulikuwa na minong'ono kuwa huenda kuna baadhi ya wasanii kutoka THT ambao nao walikuwa kwenye orodha ya wasanii watakaotumbuiza siku hiyo huenda wasitokee siku ya show hiyo ...
Wasanii hao ambao walitajwa kuwa ni BARNABA pamoja na LINAH walikuwa wakihisiwa kutokutokea siku ya show hiyo sababu huenda wanaweza kuwa wamezuiwa na kiongozi wa Tanzania House Of Talent (THT) ...

Wednesday, May 8, 2013

0

MSANII BARNABA ASAINI MKATABA MNONO NA BARCLAYS

Posted in , ,

 
Yule mkali kutoka TANZANIA HOUSE OF TALENT (TH) Mkali wa hit single ya AM SORRY ELIAS BARNABAS A.K.A BARNABA hivi karibuni alikuwa nchini kenyakwa ajili ya kusign mkataba mnono  na bank ya barclays na kutengeneza nyimbo maalum ambayo itakuwa kama nyimbo ya kuamasisha wananchi wa kitanzania afya za wakina mama na wajawazito na afya zao, BARNABA NA KIDUMU ndio mabalozi wa huo mradi, Wameshaingia studio na kidumu kwa ajili yakupata sound tofauti na test tofauti. na baada ya hapo mradi huo na wimbo huo utazinduliwa mapematarehe 8mwenzi ujao.hyperhk.blog inamtakia kila la heri barnaba katika mafanikio yake kimuziki.

Sunday, May 5, 2013

0

TAARIFA KUHUSU VIJANA WA THT LINAH NA BARNABA KUTOHUDHURIA SHEREHE YA LADY JAY DEE

Posted in ,

Linah na Barnaba wameiambia Bongo5 kuwa hawatakuwepo kwenye show ya miaka 13 ya muziki ya Lady Jaydee itakayofanyika May 31, kwa kile walichodai ni kutoafikiana kwenye malipo.
Wamesema licha ya kuendelea kuwepo kwa majina yao kwenye poster ya show hiyo, hawatotumbuiza siku hiyo. Maadhimisho ya miaka 13 ya muziki ya Lady Jaydee yatakwenda sambamba na Uzinduzi wa Album yake ya 'Nothing but the truth'.
“Dada yetu alituita, akatuambia kwamba ana kazi yake ya kutumiza miaka 13 kwahiyo akawa anasema anahitaji wasanii ambao watamsupport kwaajili ya kufanya show,” amesema Linah.
 “Sisi tulifuata protocol zote kwasababu kama wasanii tuna viongozi, tukafuata protocol zote kuweza kukubaliana naye mpaka tukafikia hatua kwenye masuala ya biashara, yaani malipo.
Kwenye upande huo kidogo tukawa tumepishana, kwenye upande wa masuala ya maslahi. Lakini sasa tunashangaa yeye kuanza kuweka posters.”

Friday, May 3, 2013

0

13TH ANNIVERSARY YA LADY JAY-DEE: HAWA NDO WASANII WATAKAOSHIRIKI HUKU WAKIWEMO WA THT

Posted in , , , ,
List ya wasanii ambao watamshindikiza Lady Jaydee aka Komando aka Anaconda kwenye sherehe za miaka 13 na uzinduzi wa Album yake mpya ya 6 'Nothing but the Truth'.Kwa mujibu wa ukurasa wa facebook wa Lady Jaydee wasanii ambao wataperform ni TID, Hamza Kalala, Barnaba, Grace Matata,Linah,Profesa Jay na Matonya
Itakuwa ni tarehe 31 May kama unavyoona kwenye Posters pande za Nyumbani Lounge.Tickets za show ya miaka 13 ya LADY JAYDEE za VIP, 50,000/= zitaanza kuuzwa tarehe 10 May 2013.
Katika ticket hii utapata Dinner, Wine zitakuwepo mezani pamoja na free CD Album mpya.
Meza ziko 50 tu zenye viti 10@. Wahi nafasi yako mapema.

Saturday, May 5, 2012

0

Angalia Nyimbo 'MBONI YANGU-Tanzania All Stars for SAJUKI'

Posted in , , , , , , ,
Wasanii waungana Kumuimbia nyimbo Mboni Yangu kwa ajili ya Sajuki. Iangalie hii hapa. Umoja Ni NGUVU, Pamoja Tutafika na tutajenga Taifa lenye neema.
Kutoa Ni Moyo.
Madee
Kimodo na Barnaba
Ditto
Madee akirekodi sauti
Ditto,Amini na Afande Sele
Zamu ya Amini
Peter Msechu
Profesa Jay akiandika mistari yake
Afande Sele nae akiandaa mistari yake
Fid Q hakubakia

Friday, May 4, 2012

0

Mr Nice Kuzindua Album Bilicanas

Posted in , , , ,
Mwanamuziki aliyetamba kwa staili ya TAKEU, Lucas Mkenda ‘Mr Nice’ anatarajia kufanya Show ya kuzindua albamu yake ya Tabia Gani katika ukumbi wa Bilicanas.
Mr Nice alisema hii itakuwa mara yake ya kwanza kupanda jukwaani baada ya takribani miaka sita kupita.
Alisema anatarajia kufanya mambo makubwa katika uzinduzi huo, ambao anatarajia kusindikizwa na wasanii kama Aman Temba, Saidi Juma ‘Chege’, Robart Mangwer ‘Ngwea’ na wengine.
Alisema pia atakumbushia nyimbo zake ambazo zilivuma sana kama Fagilia, Kikulacho,Bwana Shamba na nyingine nyingi ambazo zilifanya vizuri.
“Mashabiki wangu natakakuwakumbusha kile ambacho zamani nilikuwa nafanya, narudi
tena kama zamani” alisema.
0

Wasanii na Wanasiasa waungana kutunga nyimbo ya kumsaidia Sajuki.

Posted in , , , , , , , , ,

Zaidi ya wasanii 25,baadhi ya watu maarufu,na wanasiasa vijana wakiwemo Zitto Kabwe, Halima Mdee, Esther Bulaya, Vicky Kamata na January Makamba wameshiriki katika wimbo,Mboni Yangu ,ambao umetungwa maalumu kwa ajili ya kuhamasisha michango kwa ajili ya msanii Sajuki.
Wimbo huo ambao umetengenezwa katika studio za THT pale Kinondoni jijini Dar-Es-Salaam chini ya produsa Tudd Thomas umefanywa maalum kwa ajili ya kuhamasisha uchangiaji wa fedha za matibabu ya Sajuki ambaye anasumbuliwa na uvimbe ndani ya tumbo lake.
Kwa mujibu wa vyanzo mbali mbali vilvyokuwepo katika utengenezaji wa nyimbo hiyo Jumla ya wasanii 27 wanaofanya aina mbali mbali za muziki kama Bongo Fleva, Hip hop, Taarab na Afro Pop walishirikiana vizuri na wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kufanikisha wimbo huo wa Mboni Yangu .
Nyimbo hiyo pia itakuwepo katika muvi ya msanii wastara ambaye ndiye ameshirikiana na Dina Marios wa kipindi cha Leo Tena Clouds Fm kwa pamoja walichagua jina la wimbo huo Mboni Yangu.Kwa mujibu wa Matangazo ya radio clouds asubuhi hii kwenye kipindi cha Teo Tena watu binafsi, ama kampuni au kikundi wanaweza kwenda mjengoni na kuchangia pesa kwa ajili ya matibabu ya msanii huyo ambayo yanatakiwa yakafanyike nchini India baadae mwezi huu.
Malengo ya ukusanyaji ambayo yamewekwa kwa siku ya leo ni angalau shilingi milioni 12.
Baadhi ya waliohusika katika nyimbo hiyo ni pamoja na Chidi Benz, Prof Jay, Ali kiba, Queen Darlin, WemaSepetu, Barnaba, Halima Mdee, Wastara, Mwasiti, Amini, Viki Kamata, Madee, afande Sele, Fid Q, Linex, William Mtitu na Wema Sepetu.
Tayari harambee ya kuchangisha pesa imeshaanza na kwa habari ambazo zimetangazwa mchangiaji wa kwanza ametoa dola 5000 na pia mkurugenzi wa Clouds Media Joseph Kusaga naye ametoa mchango wa Kiasi cha shilingi Milioni 1.

Credits to: bongo5.com

Tuesday, April 17, 2012

0

KILI MUSIC AWARDS 2012

Posted in , , , , ,
♦Kili Music Awards Winners♦
1. Wimbo Bora Wa Reggae- Arusha Gold by Warriors from East
2. Wimbo Bora wa Dancehall- Maneno Maneno by Queen Darlin'
3. Wimbo Bora Zouk Rhumba- Dushelele By Ally Kiba
4. Wimbo bora wenye vionjo vya asili- Vifuu Tundu By A.T
5. Wimbo Bora wa Taarab- Nani kama Mama By Isha Mashauzi
###########A.B93##########
6. Wimbo Bora wa Kiswahili(Bendi)- Dunia Daraja By Twanga Pepeta
7. wimbo Bora wa Afro Pop- Hakunaga By Suma Lee
8. Wimbo Bora wa R&B- My Number 1 Fan By Ben Pol
9. Wimbo Bora wa Hip Hop- Mathematics By Roma
10. Msanii Bora Anayechipukia- Ommy Dimpoz
*********A.B 93*****
11. Rapa Bora wa Bendi- Kitokololo
12. Msanii Bora wa Hip Hop- ROMA
13. Wimbo Bora wa Kushirikiana- Nai Nai By Ommy dimpoz ft Ally Kiba
14. Wimbo Bora Afrika Mashariki- Kigeugeu By Jaguar
15. Mtumbuizaji Bora wa kike- Khadija Koppa
16. Mtumbuizaji Bora wa Kiume- Diamond Platnumz
17. Mtunzi Bora wa Mwaka- Diamond
18. Producer Bora Wa Mwaka- Maneck
19. Video Bora ya Muziki ya mwaka- Moyo Wangu By Diamond
20. Wimbo Bora wa mwaka- Hakunaga by Suma Lee
21. Hall Of Fame(Taasisi)-JkT Taarab
-Hall of Fame(Binafsi)-King Kiki
-Hall of Fame(Binafsi)-Remmy Ongalla
22. Mwimbaji Bora wa Kike- Lady Jay Dee
23. Mwimbaji Bora wa Kiume- Barnaba
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ