Friday, May 4, 2012

0

Wasanii na Wanasiasa waungana kutunga nyimbo ya kumsaidia Sajuki.

Posted in , , , , , , , , ,

Zaidi ya wasanii 25,baadhi ya watu maarufu,na wanasiasa vijana wakiwemo Zitto Kabwe, Halima Mdee, Esther Bulaya, Vicky Kamata na January Makamba wameshiriki katika wimbo,Mboni Yangu ,ambao umetungwa maalumu kwa ajili ya kuhamasisha michango kwa ajili ya msanii Sajuki.
Wimbo huo ambao umetengenezwa katika studio za THT pale Kinondoni jijini Dar-Es-Salaam chini ya produsa Tudd Thomas umefanywa maalum kwa ajili ya kuhamasisha uchangiaji wa fedha za matibabu ya Sajuki ambaye anasumbuliwa na uvimbe ndani ya tumbo lake.
Kwa mujibu wa vyanzo mbali mbali vilvyokuwepo katika utengenezaji wa nyimbo hiyo Jumla ya wasanii 27 wanaofanya aina mbali mbali za muziki kama Bongo Fleva, Hip hop, Taarab na Afro Pop walishirikiana vizuri na wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kufanikisha wimbo huo wa Mboni Yangu .
Nyimbo hiyo pia itakuwepo katika muvi ya msanii wastara ambaye ndiye ameshirikiana na Dina Marios wa kipindi cha Leo Tena Clouds Fm kwa pamoja walichagua jina la wimbo huo Mboni Yangu.Kwa mujibu wa Matangazo ya radio clouds asubuhi hii kwenye kipindi cha Teo Tena watu binafsi, ama kampuni au kikundi wanaweza kwenda mjengoni na kuchangia pesa kwa ajili ya matibabu ya msanii huyo ambayo yanatakiwa yakafanyike nchini India baadae mwezi huu.
Malengo ya ukusanyaji ambayo yamewekwa kwa siku ya leo ni angalau shilingi milioni 12.
Baadhi ya waliohusika katika nyimbo hiyo ni pamoja na Chidi Benz, Prof Jay, Ali kiba, Queen Darlin, WemaSepetu, Barnaba, Halima Mdee, Wastara, Mwasiti, Amini, Viki Kamata, Madee, afande Sele, Fid Q, Linex, William Mtitu na Wema Sepetu.
Tayari harambee ya kuchangisha pesa imeshaanza na kwa habari ambazo zimetangazwa mchangiaji wa kwanza ametoa dola 5000 na pia mkurugenzi wa Clouds Media Joseph Kusaga naye ametoa mchango wa Kiasi cha shilingi Milioni 1.

Credits to: bongo5.com

0 Maoni/comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ