Next
Previous
Showing posts with label Sharo Millionea. Show all posts

Thursday, April 4, 2013

0

MASTAA WAIGIZAJI MAARUFU WA AFRIKA KUTUA BONGO KATIKA UZINDUZI WA FILAMU YA MAREHEMU KANUMBA

Posted in ,


FILAMU ya mwisho kuigizwa na Steven Kanumba Kanumba The Great iliyopewa jina la Love And Power itazinduliwa kwa aina yake baada ya wasanii kutoka Afrika Magharibi kualikwa.

Mratibu wa tukio hilo, Mosses Mwanyilu, amesema kuwa msanii huyo aliyefariki dunia mwaka jana, alikuwa kipenzi cha wapenda filamu Bongo na nje ya mipaka ya Bongo, hivyo kwa kuliona hilo wameamua kualika wasanii mbalimbali. 

Tunatarajia kufanya tukio la kipekee kabisa katika uzinduzi wa filamu ya Love And Power ya marehemu Kanumba kwa sababu ni mtu wa watu. Kwa hiyo kutokana na habari ambazo tumekuwa tukizipata kutoka sehemu mbalimbali, kuna watu ambao bado hawaamini kuwa Kanumba amefariki, katika kumuenzi tumekusudia kuitendea haki filamu yake, anasema Mwanyilu. 

Filamu hiyo inadaiwa kutabiri kifo cha Kanumba. Katika filamu hiyo pia wapo wasanii kama Irene Paul, Patcho Mwamba, marehemu Sharomilionea na wasanii wengine wengi.

Monday, November 26, 2012

0

BREAKING NEWS>> MSIKILIZE KAMANDA WA POLISI AKIONGLEA KIFO CHA SHARO MILLIONEA

Posted in
 

Kuhusu kifo cha msanii/mwigizaji Sharo Milionea, namkariri Kamanda wa Polisi Tanga akisema “leo majira ya saa mbili usiku kwenye barabara ya Segera Muheza mtu mmoja alietambulika kwa jina la Hussein Ramadhani au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza alipofika eneo hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza” Kamanda amesema hakuna kona kali sana wala ubovu wa barabara kwenye sehemu aliyopata ajali Sharo Milionea, katikati ya Segera na Muheza ambapo gari imehifadhiwa mahali salama kwa sababu haitembei. Kwenye gari alikua mwenyewe.

0

RIPOTI: KIFO CHA SHARO MILLIONEA {R.I.P}

Posted in
 
Kamanda wa Polisimkoani Tanga,
Constatine Masawe
amekiri kutokea
kwa msiba wa Sharobaro,
baada ya kupata ajali katika kijiji
cha Lusanga, Muheza
ambapo pia ndio nyumbani
kwao. Sasa naweza kusema
R.I.P Sharomilonea.
#HABARI ZAIDI ZITAKUJIA HIVI PUNDE>>

Thursday, October 4, 2012

0

TULIKUA HATUJAIWEKA HII>> SHARO MILIONEA FT ALLY KIBA-CHANGANYA CHANGANYA

Posted in ,
Sharo Millionea anakuja Na Nyimbo mpya aliyoimba na Ally Kiba, Nyimbo Hii ni ya Kuchangamsha kama ilivyo kawaida ya nyimbo za Sharo Millionea.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ