Friday, August 2, 2013

0

ALLY KIBA KUFANYA SHOW YA KIHISTORIA YA MWAKA

Posted in

NDANI ya wiki moja ijayo, Sikukuu ya Idd Mosi itaadhimishwa ambapo sambamba na hilo, mkali wa wakali kwenye Bongo Fleva, Ali Kiba anatarajia kuiandika historia kubwa ya mwaka katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem, jijini Dar.
Mkali huyo anayetamba na nyimbo kali kama Dushelele, Single Boy, Nakshi Nakshi, Mac Muga, Cinderella na Karim amesema ataitumia shoo hiyo kuweka heshima yake kwa levo za kimataifa hivyo mashabiki watarajie maajabu.
“Ni shoo ambayo nitaandika historia ya mwaka, mara ya mwisho Dar Live nilifanya shoo mwaka jana lakini mwaka huu itakuwa balaa zaidi,” alisema Kiba.
Mratibu wa Dar Live, Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’ amesema siku hiyo itakuwa ni shangwe mwanzo mwisho kwani asubuhi kutakuwa na shoo maalum ya watoto kabla Kiba, Wanaume Family (Chegge, Temba, Aslay na Bi. Cheka), Bendi ya Mapacha Watatu na H. Baba hawajalivamia jukwaa kuanzia nyakati za jioni.

“Tunawasihi wazazi wawalete watoto wao mapema, kutakuwepo na mtaalam wa kuchezesha mazingaombwe anayeitwa Profesa Calabash, bembea, bwawa la kuogelea, disko toto na michezo mbalimbali.
“Ikifika saa kumi na mbili jioni, watoto watakwenda kulala na jukwaa litahimili midundo mfululizo ya wakali kibao wenye heshima kubwa kwenye Bongo Fleva,” alisema Abby Cool.
Pazia la burudani halitaishia hapo, Rais wa Ngumi za Kimataifa (TPBO), Yasin Abdallah ‘Ustaadhi’ ameiambia Showbiz kuwa bondia kutoka Kusini mwa Afrika, Zambia, Darius Lupupa atavaana na Mbongo, Francis Miyeyusho katika ndondi za kimataifa huku Chupaki Chipindi ‘Double C’ akizipiga na Ramadhan Kido ndondi za uzito wa juu.
“Ndondi za kufa mtu zitapigwa ukumbini pale, mashabiki wa ngumi wanatakiwa kufika mapema kushuhudia uwezo wa Miyeyusho kama ataibakiza heshima nyumbani au kuuachia ushindi uende Zambia,” alisema Ustaadhi.

0 Maoni/comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ