Next
Previous
Showing posts with label Chadema. Show all posts

Thursday, September 5, 2013

0

TAARIFA KAMILI JUU YA KILICHOJIRI BUNGENI

Posted in , , , , , , ,
Kiongozi wa kambi rasmi ya Upinzani Bungeni Mh Mbowe alitolewa nje ya Bunge leo  mchana baada ya kukaidi amri ya Naibu spika Mh Ndugai alipomwamuru akae na Mh Mbowe kutokutii amri hiyo.

Mh ngudai aliamuru askari wa Bunge kumtoa nje, hata hivyo baadaye wabunge karibu wote wa upinzani walitoka pia isipokuwa Mh. Augustin Mrema wa TLP.

 MH. KINGWANGALA AMTUKANA MBOWE
Mbunge wa Nzega Dr. Kigwangalla, ametumia muda wake karibu wote wa kuchangia Muswada wa Katiba kwa kumshambulia Mwenyekiti wa CHADEMA, Mhe. Mbowe kuwa ni Mjinga, Mpuuzi, ametia aibu aibu

Kigwangalla  amempongeza  Naibu  Spika  kwa  kumtimua  Mbowe  bungeni  na  kusema  kuwa  kitendo  hicho  kimemshikisha  adabu...




Aidha, mbunge  huyo  wa  Nzega amedai kuwa Mbowe sio Mchaga bali ni mhuni fulani  aliyejivika  sura  ya  Uchaga  kwa  masilahi  yake  binafsi !.

Kigwangalla  alihitimisha  mchango wake  kwa  kudai  kuwa wapinzani wana akili za shetani  zisizovumilika!


SUGU AKAMATWA
Taarifa kutoka Dodoma zinadai kuwa kuna Askari mmoja ambaye ni miongoni mwa walinzi wa Bunge ameenda kufungua faili Polisi Dodoma na kusema kuwa ametishiwa kupigwa na Mbunge Sugu...

Baada ya kufungua Jalada hilo polisi wamechukua Difenda 6 na wameingia mitaani kumtafuta ili awekwe ndani mpaka kesho ndio afikishwe mahakamani asubuhi.

Monday, September 2, 2013

0

CHADEMA WAMKANA AFANDE SELE, HIKI NDO WALICHOKISEMA

Posted in ,


Gazeti la Habari Leo la siku ya leo tarehe 2 Septemba lenye kichwa cha habari "Chadema kuzoa wasanii mastaa" pamoja na mambo mengine, mwandishi amemnukuu mmoja wa wasanii toka mkoa wa Morogoro akisema amewahi kuombwa na viongozi wa mkoa wa CHADEMA kugombea Ubunge.

NAOMBA KUWEKA KUMBUKUMBU SAHIHI.
1. Mimi ndiye mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Morogoro, ninayeongoza Baraza la Uongoz la mkoa lenye wajumbe wa5 tu tangu mwaka 2009.
2. Katika vikao vyetu vyote hukujawahi kuwepo kwa AGENDA ya kumuomba/ kumshawishi mtu yeyote kugombea nafasi yoyote.

Sunday, August 4, 2013

0

HAYA NDO MANENO ALIYOSEMA DK. SLAA DHIDI YA RAISI JAKAYA KIKWETE

Posted in , , ,
#NANUKUU
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, amemkosoa Rais Jakaya Kikwete, kuhusu kauli  yake ya  kumshauri Rais wa Rwanda, Paul Kagame, kuzungumza na waasi wa serikali yake ...


Dk. Slaa amesema haoni busara kwa Rais Kikwete kuwaambia viongozi wa Rwanda, akiwamo Rais Kagame, kuzungumza na wafuasi wa chama cha FDRL walioko Congo.

Slaa  aliyasema hayo wakati akizungumza katika kongamano la vijana wa Chadema (BAVICHA) la uchumi na ajira lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.

“Rais Kikwete hapa nyumbani hawezi kuzungumza na wapinzani  na hajachukua hatua dhidi ya wauaji wa mwandishi Daudi Mwangosi..."

"Alishauriwa amuwajibishe Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda  na  badala  yake amempandisha cheo,” alisema Slaa.


Kauli  Dk Slaa imekuja siku moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kueleza kuwa Tanzania haina mgogoro na nchi ya Rwanda, kutokana na kauli za kejeli na matusi zilizokuwa zikitolewa na viongozi wa nchi hiyo dhidi yake na Tanzania.

Thursday, July 11, 2013

0

KAULI YA POLISI TANZANIA -PT- JUU YA SUALA LA CHADEMA KUANZISHA KUNDI LA KUJIHAMI

Posted in ,
.

Saturday, June 22, 2013

0

HIKI NDICHO ALICHOKISEMA MREMA JUU YA CHADEMA

Posted in , ,
Nassari akiwa Hospitali

Akizungumza na Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari aliyelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kupigwa na Wanachama wa CCM wakati wa uchaguzi mgodo wa Udiwani Kata ya Makuyuni Wilayani Monduli Mkoani Arusha Juni 16

“Dola haina huruma kupiga mabomu wananchi,kutesa viongozi na kuwafungulia kesi ili wawadhoofishe wasifanye kazi ya kuwatumikia wananchi, au kufanya shuguli za kisiasa”alisema Mrema. Mrema aliongeza kuwa ingawa Serikali inatumia nguvu kama walizotumia kumdhoofisha yeye, lakini ana imani kuwa mbinu hizo kwa CHADEMA hazitafua dafu, kwa chama hiki wamekutana na kisiki cha mpingo,huku akishauri pande zote mbili zitumie busara katika kufanya siasa ili wasije waka hatarisha amani ya nchi.


"Mbinu za Serikali hazifui dafu kwa CHADEMA"-Mrema

Thursday, June 20, 2013

0

MTAMBUE ALIYERUSHA BOMU KWA KUSOMA HAPA (TAARIFA TOKA CHADEMA DIASPORA)

Posted in ,


Kati ya hawa waliotajwa, Nani karusha bomu?! Mtambue

Soma kwa makini na nanukuu (neno kwa neno) gazeti la Mwananchi toleo Na: 4741;
Jumanne, Juni 18 2013 ukurasa wa 4;

Majeruhi Mwengine Majeruhi mwingine, Abdallah Hilali (39) aliyelazwa katika Hospitali ya Arusha Lutheran Center amedai kuwa majeraha aliyopata miguuni yametokana na kupigwa risasi na Polisi na kudondekewa na vipande vya bomu.

Alisema alikuwa nyma ya jukwa kuu akimsikiliza Mbowe na alipomaliza kuhutubia alishuka jukwaani kukusanya sadaka, ndipo alipoona mfuko wa mweusi mdogo wa plasitiki ukipeperuka juu.“Nilidhani ni upepo unapeperusha kitu, lakini ghafla nilisikia kishindo na nikamsikia mama mmoja akipiga kelele kuwa aliyerusha mfuko anakimbia, nilipogeuka nikajikuta nipo chini,” alisema Hilali.

Wednesday, June 19, 2013

0

TAARIFA KWA WANA-CHADEMA WOTE WA ARUSHA

Posted in , ,


Judith Moshi Kuzikwa
20/06/2013 SOKON ONE ARUSHA.

Wananchi, wapenzi na wanachama
wote wa CHADEMA tukutane Mount
Meru Mortuary asubuhi saa tatu
kutoa heshima za mwisho kwa
marehemu Judith Moshi aliyefia
kwenye tukio la bomu tarehe
15/2013.
Mhe. Mbowe ataongoza tukio hilo

0

ANGALIA VIDEO YA MLIPUKO WA BOMU ARUSHA

Posted in ,

Tuesday, June 18, 2013

0

PICHA ZAIDI ZA TUKIO LA MABOMU ARUSHA

Posted in ,







Photo Credits to: Albert Balati
0

PHOTOS: TUKIO ZIMA LA MABOMU ARUSHA (JINSI MJI ULIVYOCHAFUKA)

Posted in , ,
Raia walipoamua kufunga barabara na kuchoma moto




HABARI KAMILI JUU YA KILICHOSABABISHA:
Jeshi la polisi limekipiga marufuku chama cha demokrasia na maendelo(CHADEMA)kufanya shughuli zozote za kuaga miili ya marehemu kwenye viwanja vya Soweto kwani zoezi la uchunguzi bado linaendelea kwenye viwanja hivyo .

Akizungumza ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas amesema kutokana na uchunguzi unaoendelea wa tukio la bomu kwenye viwanja hivyo imeonelea kuwa si busara kuweka mkusanyiko wa watu kwani kutaharibu upelelezi.


Kamanda Sabas amedai  kuwa  jeshi la polisi  liliwataka viongozi wa chama hicho kuwaeleza wafuasi wao mahali sahihi watakapoweza kufanyia shughuli hiyo lakini si kwenye viwanja hivyo.

Hali kwenye viwanja hivyo imekuwa ya pilika pilika tangu juzi kwa wafuasi wa chama hicho kujikusanya tokea asubuhi hadi jioni kwa madai ya kuomboleza ..

Hata hivyo viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo walikaidi agizo hilo na  kuanza  kujikusanya uwanjani hapo pamoja na wafuasi wa CHADEMA , hali iliyoleta  mvutano kati ya viongozi  wa jeshi la polisi na  wafuasi hao.

Wakati mabishano hayo yakiendelea, Askari Polisi mmoja  alijichanganya na kuingia katikati ya wafuasi wa Chadema pembeni mwa uwanja huo ambao walikua wanasubiri kujua utaratibu wa kuaga miili ya Marehemu waliolipuliwa na bomu June 15 2013.

Baada ya hapo,Wafuasi hao hawakupenda kitendo cha Polisi kujichanganya nao hivyo ikazuka ugomvi huku wakitaka atoke, baada ya dakika kadhaa  mabumu yalianza kusikika.

Baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho waliokuwepo uwanjani haponi mbunge wa jimbo la ubungo John Mnyika,Ezekia Wenje,Tundu lissu, Halima Mdee...
 

Monday, June 17, 2013

0

LIVE KUTOKA SOWETO ARUSHA | PICHA MBALIMBALI KATIKA MAOMBOLEZO YA NDUGU ZETU WALIOATHIRIWA NA BOMU

Posted in ,

Hivi sasa hali iliyopo soweto mkoani Arusha, ni ya utulivu huku watu wakisubiri viongozi wa chama hicho wafike eneo hilo, huku pia Makamu wa Raisi akitegemewa kuwasili eneo hilo.
Hali ya ulinzi iko shwari hasa ukizingatia kuna uwepo wa askari mahiri wa JWTZ wakiwa pamoja na FFU na jeshi la Polisi Tanzania. ambao walifika eneo hilo mapema asubuhi.



Sunday, June 16, 2013

0

HALI ILIVYO SASA SOWETO, ARUSHA

Posted in ,

HIVI SASA UCHUNGUZI BADO UNAENDELEA HUKU ENEO LA TUKIO LIKIWA LIMEZIBWA NA TURUBALI UCHUNGUZI UKIENDELEA KUFANYWA. ENEO HILO BADO LIMEJAA WATU AMBAO HAWAAMINI KILICHOTOKEA JANA NA KUENDELEA KULALAMA. HABARI ZAIDI ZITAKUJIA.
Photo Credits: ALBERT BALATI



Saturday, June 15, 2013

0

HALI ILIVYO SOWETO ARUSHA HIVI SASA

Posted in ,


Polisi wakifanya Uchunguzi

Makamanda wa chadema waombwa kwenda kuchangia damu katika hospitali ya seliani. Watu zaidi ya wawili wamefariki kwenye
bomu lililolipuliwa saa kumi na mbili jioni ambapo majeruhi ni zaidi ya 10, pia gari la wagonjwa
la Hospitali ya Mount Meru STK
8493 limevunjwa vioo kwa madai
ya wananchi kwamba
limeshindwa kuokoa maisha ya
majeruhi, inaripotiwa pia bomu
lililolipuliwa sio la polisi.
- Bomu lililolipuka linadaiwa kuejeruhi watu sana. Inaonekana bomu lilitegwa karibu na gari la matangazo.
Gari Ya Freeman Mbowe 





0

PICHA: MLIPUKO WA BOMU KATIKA KAMPENI ZA CHADEMA SOWETO, ARUSHA

Posted in ,

Monday, April 29, 2013

0

MBUNGE LEMA AACHIWA KWA MDHAMANA (ANGALIA MABANGO YA WAFUASI WA CHADEMA YAKIMKOSOA MKUU WA MKOA)

Posted in ,
mH.akiwa kizimbani

Wednesday, April 24, 2013

0

BAADA YA MWANAFUNZI KUULIWA, CHUONI IAA WAJIANDAA KUANDAMANA HUKU MH. GODBLESS LEMA AKIWANUSURU

Posted in ,


Habari zilizo tufikia: Baada ya kuuwawa kwa mwanafunzi wa mwaka wa pili jana, wanafunzi wanajiandaa kuandamana. Mh. Godbless Lema amewasili kunusuru maandamano.

Hali bado ni tete Chuoni Njiro.

Stay tuned…
SOURCE: CHADEMA DIASPORA
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ