Thursday, September 5, 2013

0

TAARIFA KAMILI JUU YA KILICHOJIRI BUNGENI

Posted in , , , , , , ,
Kiongozi wa kambi rasmi ya Upinzani Bungeni Mh Mbowe alitolewa nje ya Bunge leo  mchana baada ya kukaidi amri ya Naibu spika Mh Ndugai alipomwamuru akae na Mh Mbowe kutokutii amri hiyo.

Mh ngudai aliamuru askari wa Bunge kumtoa nje, hata hivyo baadaye wabunge karibu wote wa upinzani walitoka pia isipokuwa Mh. Augustin Mrema wa TLP.

 MH. KINGWANGALA AMTUKANA MBOWE
Mbunge wa Nzega Dr. Kigwangalla, ametumia muda wake karibu wote wa kuchangia Muswada wa Katiba kwa kumshambulia Mwenyekiti wa CHADEMA, Mhe. Mbowe kuwa ni Mjinga, Mpuuzi, ametia aibu aibu

Kigwangalla  amempongeza  Naibu  Spika  kwa  kumtimua  Mbowe  bungeni  na  kusema  kuwa  kitendo  hicho  kimemshikisha  adabu...




Aidha, mbunge  huyo  wa  Nzega amedai kuwa Mbowe sio Mchaga bali ni mhuni fulani  aliyejivika  sura  ya  Uchaga  kwa  masilahi  yake  binafsi !.

Kigwangalla  alihitimisha  mchango wake  kwa  kudai  kuwa wapinzani wana akili za shetani  zisizovumilika!


SUGU AKAMATWA
Taarifa kutoka Dodoma zinadai kuwa kuna Askari mmoja ambaye ni miongoni mwa walinzi wa Bunge ameenda kufungua faili Polisi Dodoma na kusema kuwa ametishiwa kupigwa na Mbunge Sugu...

Baada ya kufungua Jalada hilo polisi wamechukua Difenda 6 na wameingia mitaani kumtafuta ili awekwe ndani mpaka kesho ndio afikishwe mahakamani asubuhi.

0 Maoni/comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ