Next
Previous
Showing posts with label Joseph Mbilinyi ''Mr. II''. Show all posts

Thursday, September 5, 2013

0

TAARIFA KAMILI JUU YA KILICHOJIRI BUNGENI

Posted in , , , , , , ,
Kiongozi wa kambi rasmi ya Upinzani Bungeni Mh Mbowe alitolewa nje ya Bunge leo  mchana baada ya kukaidi amri ya Naibu spika Mh Ndugai alipomwamuru akae na Mh Mbowe kutokutii amri hiyo.

Mh ngudai aliamuru askari wa Bunge kumtoa nje, hata hivyo baadaye wabunge karibu wote wa upinzani walitoka pia isipokuwa Mh. Augustin Mrema wa TLP.

 MH. KINGWANGALA AMTUKANA MBOWE
Mbunge wa Nzega Dr. Kigwangalla, ametumia muda wake karibu wote wa kuchangia Muswada wa Katiba kwa kumshambulia Mwenyekiti wa CHADEMA, Mhe. Mbowe kuwa ni Mjinga, Mpuuzi, ametia aibu aibu

Kigwangalla  amempongeza  Naibu  Spika  kwa  kumtimua  Mbowe  bungeni  na  kusema  kuwa  kitendo  hicho  kimemshikisha  adabu...




Aidha, mbunge  huyo  wa  Nzega amedai kuwa Mbowe sio Mchaga bali ni mhuni fulani  aliyejivika  sura  ya  Uchaga  kwa  masilahi  yake  binafsi !.

Kigwangalla  alihitimisha  mchango wake  kwa  kudai  kuwa wapinzani wana akili za shetani  zisizovumilika!


SUGU AKAMATWA
Taarifa kutoka Dodoma zinadai kuwa kuna Askari mmoja ambaye ni miongoni mwa walinzi wa Bunge ameenda kufungua faili Polisi Dodoma na kusema kuwa ametishiwa kupigwa na Mbunge Sugu...

Baada ya kufungua Jalada hilo polisi wamechukua Difenda 6 na wameingia mitaani kumtafuta ili awekwe ndani mpaka kesho ndio afikishwe mahakamani asubuhi.

Saturday, October 6, 2012

0

MH. SUGU, ASEMA TRA WAMTOZE KODI RICK ROSS KUTOKANA NA MAPATO ATAKAYOPATA LEO KATIKA FIESTA

Posted in , , ,
MWANAMUZIKI nguli wa Hip hop Tanzania na Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Osmund Mbilinyi amewapa mwongozo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhusu ziara ya mwanamuziki nyota wa Hip hop Marekani, William Leonard Roberts II anayetambulika kama Rick Ross au The Boss, kwamba anastahili kulipa kodi kutokana na pato atakalaolingiza katika shoo yake ya leo. Rick Ross atatumbuiza usiku wa leo katika tamasha la Serengeti Fiesta 2012 kwenye viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar es Salaam, ambalo linaandaliwa na Prime Time Promotions na  kudhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL). 

Mbunge Mbilinyi ambaye anajulikana kwa majina ya kimuziki kama Mr II au Sugu, ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook;
“RICKY ROSS ANAKUJA, SAWA HAINA SHIDA… ILA TUNATAKA KUJUA AMELIPWA KIASI GANI NA ATAKATWA KIASI GANI KIBAKI KWENYE KODI YA TAIFA LETU KAMA AMBAVYO MIMI NIKIENDA KUFANYA SHOW/CONCERT MAREKANI NAKATWA KODI NA SERIKALI YAO…”. 
The Boss, ameahidi kukonga nyoyo za mashabiki watakaohudhuria tamasha la Serengeti Fiesta 2012 jioni ya leo kwenye viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar es Salaam. Rapa huyo, aliyefikia katika  hoteli ya Hyatt, zamani Kilimanjaro Kempensky, Dar es Salaam, ambaye alizaliwa JanuarI 28, mwaka 1976 huko Carol City, Florida, Marekani alisema hayo baada ya kutua Dar es Salaam usiku wa jana. “Rick Ross ametua na ameahidi kufanya shoo kali sana,”alisema Allan Chonjo, Meneja wa Bia ya Serengeti, wadhamini wakuu wa Fiesta.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ