HAYA NDO MANENO ALIYOSEMA DK. SLAA DHIDI YA RAISI JAKAYA KIKWETE
Posted in Chadema, Dr. Slaa, Mh. Jakaya Mrisho Kikwete, Paul Kagame
#NANUKUU
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, amemkosoa Rais Jakaya Kikwete, kuhusu kauli yake ya kumshauri Rais wa Rwanda, Paul Kagame, kuzungumza na waasi wa serikali yake ...
Dk. Slaa amesema haoni busara kwa Rais Kikwete kuwaambia viongozi wa Rwanda, akiwamo Rais Kagame, kuzungumza na wafuasi wa chama cha FDRL walioko Congo.
Slaa aliyasema hayo wakati akizungumza katika kongamano la vijana wa Chadema (BAVICHA) la uchumi na ajira lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.
“Rais Kikwete hapa nyumbani hawezi kuzungumza na wapinzani na hajachukua hatua dhidi ya wauaji wa mwandishi Daudi Mwangosi..."
"Alishauriwa amuwajibishe Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda na badala yake amempandisha cheo,” alisema Slaa.
Kauli Dk Slaa imekuja siku moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kueleza kuwa Tanzania haina mgogoro na nchi ya Rwanda, kutokana na kauli za kejeli na matusi zilizokuwa zikitolewa na viongozi wa nchi hiyo dhidi yake na Tanzania.
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, amemkosoa Rais Jakaya Kikwete, kuhusu kauli yake ya kumshauri Rais wa Rwanda, Paul Kagame, kuzungumza na waasi wa serikali yake ...Dk. Slaa amesema haoni busara kwa Rais Kikwete kuwaambia viongozi wa Rwanda, akiwamo Rais Kagame, kuzungumza na wafuasi wa chama cha FDRL walioko Congo.