TBL kudhamini Taifa Stars dola million 10 kupitia bia ya Kilimanjaro!
Posted in Ephraim Kibonde, Kilimanjaro Premium Lager, Leodger Tenga, Taifa Stars, TFF
Kampuni ya Bia Tanzania Limited (TBL) pamoja na Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) zimesaini mkataba ambapo TBL itakuwa mdhamini mpya wa
Timu ya Taifa-Taifa Stars.
Kwa mujibu wa maridhiano hayo, TBL kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager itaidhamini Taifa Stars kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo.
Mkataba huo ulisainiwa jijini Dar es Salaam jana mbele ya maafisa waandamizi wa TFF, wawakilishi kutoka TBL, vyombo vya habari na wadau wengine wa soka nchini Tanzania.
Hii ni mara ya kwanza kwa kampuni hiyo kubwa ya bia kutoa udhamini kwa timu ya taifa, hata hivyo huko nyumba TBL iliwahi kushiriki katika udhamini wa masuala ya soka kwa miaka minne nyuma huku ikidhamini Taifa Cup na vilabu vikubwa vya Simba na Yanga.
Akizungumza katika hafla hiyo ya kutiliana saini, Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Robin Goetzsche alisema udhamini huoi utafungua mwanga mpya katika medani ya soka nchini Tanzania.
“Tunasaini mkataba wa miaka mitano wenye thamani ya dola za Marekani milioni 10 na katika kipindi chote hicho kaulimbiu yetu itakuwa “Fikisha Soka ya Tanzania Katika Kilele cha Mafanikio” na kutupa kila sababu ya kujivunia kilicho chetu
Tuna matarajio makubwa sana na timu ya taifa kwani tunaamini kuwa ina uwezo wa kufanya maajabu, na kama nilivyosema awali, hili ni pambazuko la kuelekea mafanikio. Uwekezaji wetu umelenga katika kuhakikisha kambi za mazoezi zinaimarishwa, wachezaji watalala katika hoteli zenye ubora wa juu zenye zaidi ya ngazi tatu zilizo na bwawa la kuogelea na vifaa vya mazoezi, vifaa vinaboreshwa na pia vijana watapata fursa za kucheza mechi nyingi za kirafiki ili wajipime nguvu na kupata uzoefu zaidi na timu zinapata basi jipya la kisasa.
Kwa kuongeza, alisema udhamini wao utasaidia katika:
a) Ununuzi wa vifaa mbalimbali vya kisasa.
b) Mafunzo kwa wafanyakazi wa TFF ndani na nje ya nchi.
c) Uendeshaji wa tovuti ya TFF.
d) Semina na mikutano ya utawala bora.
Grand Malt, ambacho ni kinywaji kisicho na kilevi kitakuwa kikidhamini Ligi Kuu ya Zanzibar. Hii ni kuonyesha namna TBL ilivyo mstari wa mbele katika kuhamasisha soka si kwa Bara tu bali na Visiwani. Mkataba huu ni wa miaka mitatu na utamalizika mwaka 2015 ukiwa na thamani ya Sh milioni 140 kila mwaka. Kwa upande wake, Rais wa TFF, Lodger Tenga aliahidi kutoa ushirikiano thabiti kwa wadhamini wapya kwani anaamini mkataba huo utaleta mapinduzi chanya katika soka nchini Tanzania. Hata hivyo, aliwaomba Watanzania kuwa na uzalendo kwa timu yao ya taifa kwa kuishangilia kwa wingi kwenye mechi zake.
“Hakuna jema lolote kama tutakuwa na ari ya kuzishabikia timu za nje badala ya ya timu ya nyumbani, wachezaji wetu wanahitaji moyo wawapo uwanjani kwa kushangiliwa ipasavyo,” alisema.
Naye Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe alisema udhamini huo ni wa thamani na kwamba watafanya kila liwezekanalo kuisaidia TFF kuhakikisha kuwa Taifa Stars inang’ara katika anga za kimataifa na hivyo kukidhi kiu ya Watanzania.
“Hii ni mara ya kwanza kuidhamini Taifa Stars na tunataka kuja kwa mtindo mpya na wa kipekee, tunataka Watanzania wajivunie timu yao kwa sababu ukarimu huanzia nyumbani…tuwape moyo wachezaji wetu na tujivunie kilicho chetu,” alisema.

0 Maoni/comments: