TOKA TFF: Taifa Stars, Gambia Marefa ni wa Zimbabwe
Posted in Taifa Stars, TFF, World Cup 2014 Brazil- • GAMBIA wachelewa, kutua leo Saa 9 Usiku!
Kufuatia Taarifa iliyosambazwa na Ofisa
Habari wa TFF, Boniface Wambura, lile pambano kati ya Taifa ya Tanzania,
Taifa Stars,na Gambia liitakalochezwa Jumapili Juni 10 Uwanja wa Taifa
Jijini Dar es Salaam la Kundi C la Kanda ya Afrika kusaka Timu 5
zitakazocheza Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil Mwaka 2014,
litachezeshwa na Waamuzi kutoka Zimbabwe.
Pia, Taarifa hiyo imejulisha kuhusu kuchelewa kuwasili kwa Msafara wa Gambia.
IFUATAYO NI TAARIFA KAMILI:
Release No. 087
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Juni 7, 2012
WAZIMBABWE KUCHEZESHA TAIFA STARS, GAMBIA
Waamuzi kutoka Zimbabwe ndiyo
watakaochezesha mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia hatua ya makundi Kanda
ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Gambia itakayochezwa Juni
10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Shirikisho la Kimataifa la
Mpira wa Miguu (FIFA) mwamuzi wa kati atakuwa Ruzive Ruzive. Waamuzi
wasaidizi ni Salani Ncube na Edgar Rumeck wakati mwamuzi wa akiba ni
Norman Matemera.
Kamishna wa mechi hiyo itakayoanza saa
10 kamili jioni ni Fanie Wallace Mabuza kutoka Swaziland wakati
mtathmini wa waamuzi (referee assessor) ni Ali Baligeya Waiswa.
Waamuzi hao watawasili nchini kesho
(Juni 8 mwaka huu) saa 1.20 usiku kwa ndege ya Kenya Airways wakati
Kamishna wa mechi hiyo atawasili siku hiyo hiyo saa 12.50 jioni kwa
ndege ya South African Airways. Mtathmini wa waamuzi atatua pia Juni 8
mwaka huu saa 7.55 mchana kwa ndege ya Kenya Airways.
Taifa Stars inayodhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager inaendelea na mazoezi leo saa 10 jioni kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam chini ya Kocha Mkuu Kim Poulsen.
GAMBIA KUWASILI LEO USIKU
Timu ya Taifa ya Gambia (The Scorpions)
ambayo awali ilikuwa iwasili nchini leo (Juni 7 mwaka huu) saa 1.40
asubuhi sasa itawasili leo saa 9.20 usiku kwa ndege ya Kenya Airways
tayari kwa ajili ya mechi dhidi ya Taifa Stars.
The Scorpions ilipaswa kubadili ndege
Dakar, Senegal jana usiku lakini kukawa na ucheleweshaji (delay), hivyo
ikashindwa kuwahi Nairobi, Kenya ambapo ingeunganisha kwa ndege ya
alfajiri kuja Dar es Salaam.
Kikosi cha timu hiyo chenye wachezaji 22
wakiwemo tisa wanaocheza mpira wa kulipwa nje ya nchi hiyo kitafikia
kwenye hoteli Sapphire iliyopo Mtaa wa Lindi na Sikukuu eneo la
Kariakoo.
Wachezaji walioko katika msafara huo ni
Musa Camara, Abdou Jammeh, Momodou Futty Danso, Lamin Basmen Samateh,
Ousman Koli, Pa Saikou Kujabi, Mustapha Kebba Jarju, Yankuba Mal Ceesay
na Demba Savage.
Wengine ni Saihou Gassama, Alieu Darboe,
Momodou Ceesay, Pa Modou Jagne, Tijan Jaiteh, Bubacarr Sanyang,
Christopher Allen, Musa Yaffa, Sulayman Marr, Mamut Saine, Hamsa Barry,
Ali Sowe, Omar Colley na Saloum Faal.
PROGRAMU YA MAZOEZI YA GAMBIA
IJUMAA JUNI 8
01.00 asubuhi Mazoezi- Uwanja wa Karume
10.00 jioni Mazoezi- Uwanja wa Taifa
JUMAMOSI JUNI 9
04.00 asubuhi Mkutano na Waandishi wa Habari- Ukumbi wa TFF
10.00 jioni Mazoezi- Uwanja wa Taifa
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Source: sokainbongo.com
Source: sokainbongo.com
0 Maoni/comments: