Friday, July 6, 2012

0

GUCCI V/S LOUIS VUITTON (Brand gani kali kati ya hizi?)

Posted in , , , , , , , , , , ,
Kwa wale walevi wa fashion kama mimi(najua haters wanajiuliza,wapi wewe fashion wakati mitumba tupu)poa yote maisha..
Haya,ngoja nibadilishe kauli,kwa wale wapenda fashion(nimejitoa) najua wengi wenu mna ufahamu wa kutosha japo sio saana juu ya bidhaa hizi kutoka nyumba kubwa mbili za fashion duniani(Gucci na Louis Vuitton),yaani GG na LV kama mnavyozifahamu kwa label na picha!!





GUCCI LOGO GG
LOUIS VUITTON LOGO WITH THE MONOGRAM LV


Majuzi kati nikiwa natoka shule,ile nimeshuka tu kutoka kwenye tube(treni) nikakuta vijana wawili wa kiafrica wanazozana juu ya ipi bora,Gucci au LV,si unajua tena wakongo wanavyopenda sifa?wako radhi waibe lakini wapendeze! na wanigeria walivyobobea kwenye taaluma ya kubishana(watabishana hata na wewe jina unalotumia sio lako)

Kwa kuwa sikuwa na cha maana cha kunifanya niwahi nyumbani basi nikaamua kuketi nao niwasikilize ili ikiwezekana na mimi nichangie ya kwangu(sikujua kama wataweza kunisikiliza mtanzania,maana wanakuwaga na madharau sana)
Basi nikawasikiliza vya kutosha,ghafla nikaona wanaanza kutoka nje ya mada(diverging)..ikabidi niwarudishe kwenye mada kwa kutoa ya kwangu ninayoyajua.Maana walikuwa washaanza kuleteana zile habari za ''kwanza wewe Gucci umekuja kuijulia UK,ulikua unaiona tu kwenye TV'' nikasema huyu kashindwa kujadili anaanza kukashifu! Nikawaweka chini na kuwapa yangu na yalikuwa kama yafuatayo..;
Si unajua nilivyo na sifa inavyokuja kwenye kitu kinachohusu maelezo?(ndo maana nilifaulu History tu)


1. UHALISIA
Japo kuna bidhaa kubwa zaidi ya hizi lakini ukweli ni kuwa Gucci na LV ni moja ya bidhaa kubwa hapa duniani,tukiongelea ulimwengu wa fashion.


2. HISTORIA

Gucci au ''the house of Gucci'' kama inavyofahamika ni label ya mavazi kutoka ITALY iliyogunduliwa mnamo mwaka 1921 huko Florence(mji mkuu wa ukanda wa Tuscany huko Italia) na Guccio Gucci ambapo watoto wake ndo walikuja kuikuza na kuifanya label ya kimataifa hapo baadae.Gucci ilikuwa label inayofahamika zaidi kwa ugomvi wa kifamilia uliokuwa unatokea mara kwa mara lakini pamoja na vikwazo hivyo iliweza kukua haraka na ku-branchout dunia nzima.
Kwa sasa inamilikiwa na Pinault-Printemps-Redoute(kampuni inayojihusisha na kununua label za biashara za rejareja duniani iliyogunduliwa na Francois Pinault mwaka 1963 na sasa inaendeshwa na kumilikiwa na mwanae FRANCOIS HENRY PINAULT.
GUCCI STORE?HATA ZAMANI ILIKUWA BUSY PIA



.LOUIS VUITTON au Louis Vuitton Malletier kama ilivyokua ikijulikana zamani kwa sababu Malletier ni neno la kifaransa likiwa na maana ya ''TRUNK MAKER'' yaani watengeneza matranka(wale waliosoma boarding watanielewa vizuri).Hii ni label ya FRANCE iliyoanza shughuli zake kwa kutengeneza mabegi makubwa na matranka mnamo mwaka 1854.Baadae ikaingia kwenye ushirikiano wa kibiashara na kampuni ya Vichy,baada ya vita ya pili ya dunia WWII hapo ndo ikaanza kutengeneza vitu vingine kama nguo na pochi
MOJA YA MATRANKA YA ZAMANI KABISA YA LOUIS VUITTON


3. BIDHAA ZINAZOPATIKANA

Gucci wanatengeneza nguo,saa,magegi,nguo za watoto,viatu,mikufu,bangili,kofia,mikanda n.k.Ushafahamu kwanini Gucci wanapenda kutengeneza bidhaa zenye rangi ya udongo kwa wingi?jee waifahamu miti aina ya Bamboo?na rangi yake je?Mnamo mwaka 1947 Gucci waliamua kuanza kutumia material ya bamboo tree kwenye handle za mabegi yake ambayo ilifanya vizuri sokoni,ikifuatiwa na kuzinduliwa kwa label yao ya GG unayoiona kwenye bidhaa zao siku hizi,label hiyo ilitumika kwa mara ya kwanza miaka ya '80.
GUCCI STUFFS


Louis Vuitton wanafahamika zaidi kwa utengenezaji na uuzaji wa mabegi japo nao pia wanatengeneza saa,viatu,nguo,pochi,mikufu n.k.Label yao inafahamika zaidi kwa monogram ya LV kwenye kila bidhaa yao.
LOUIS VUITTON 
ACCESSORIES


4. HESHIMA & STATUS

Bidhaa zote mbili zinajulikana kwa kutengeneza vitu vya kifahari na vya bei ghali vinavyohusishwa na mastaa na watu maarufu duniani.Na pia bidhaa zote mbili zinapata hasara kwa kuwepo sokoni kwa vitu feki(counterfeits) Huku nikiwa nakagua tshirt ya yule mkongo maana ilikuwa inaonekana ni feki kwa mbali!!
GWEN STEFANI AKIWA NDANI YA GUCCI


KIM KARDASHIAN NI MPENZI MZURI WA MABEGI YA LOUIS VUITTON.

Katika list iliyotoka mwaka huu January 30th Louis Vuitton ilikuwa ni brand ya 3 maarufu na ubora duniani,Versace ya 6,Giorgio Armani ya 9..Gucci haikufua dafu hapo japo watu wanaona kama iko midomoni kwa watu sana,Huniamini?tembelea (http://luxpresso.com/photogallery-couture/top-10-valuable-luxury-fashion-brands/10594/9)

SUMMARY YANGU SASA

Nazipa heshima hizi brand mbili kwa ubora na umaarufu wa hali ya juu sana,GUCCI ina status yake ukivaa na LV ina status yake ukivaa,ila kinachowasumbua watu hapa ni kitu kinaitwa Brand Loyalty.Yaani mapenzi binafsi kwenye brand,ni kama ugomvi wa Android na Apple,pamoja watu kujua kuwa kuna moja lazima imeizidi mwenzake lakini bado kila mtu atapigania upande wake na kutetea cha kwake.
Gucci ni nzuri,sikatai ila kwa wanaojua fashion hasa kwa wale walioko deep sana watakubaliana na mimi kuwa LV ni bei mbaya sana ukilinganisha na GUCCI,ni rahisi kuvaa GUCCI kuliko kuvaa LV,Louis Vuitton haipatikani kirahisi rahisi kama Gucci.
 So nikawaambia wale ndugu zangu wabishani,nyote mmevaa vitu vya ukweli ila LV ni mwisho wa matatizo,so salute kwa yule MNIGERIA aliyevaa LV na heshima pia kwa yule mkongo aliyetilia kitu cha Gucci.

Ikabidi niwaage niwahi kwangu,yule Mnigeria akasema hahaha ''YU DE SPEAK WELL WELL OOH'' huku naye yule mkongo akiniambia ''MERCI MON AMI s'il vous plaît passer d'ici demain pour une autre conférence,'' akimaanisha thank you my friend,please pass by tomorrow for another lecture.

HUYOOOO NIKAJIKATAA ZANGU MITAA YA CHALGROVE TOTTENHAM.


jifurahishe na baadhi ya picha hapa chini;


























0 Maoni/comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ