Thursday, May 17, 2012

0

Mchezaji wa Simba Patrick Mutesa Mafisango afariki katika ajali ya gari

Posted in , ,
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, marehemu Patrick alipata ajali maeneno ya TAZARA alipokuwa akiendesha gari na kujaribu kumkwepa mwendesha pikipiki na kwa bahati mbaya gari lake likakosa uelekeo na kuingia mtaroni na kusababisha ajali iliyomwacha na majeraha makubwa ambapo aliaga dunia muda mfupi baadaye.
Patrick alijiunga kuichezea Simba SC akitokea timu ya Azam FC. Alizaliwa tarehe 9 Machi 1980 mjini Kinshasa, Kongo D.R.C lakini alikuwa raia wa Rwanda.
Amefariki siku chache tu baada ya kocha wa timu ta taifa ya Rwanda kumuita kujumuika katika timu ya Taifa ya nchi hiyo.
Poleni nyote mliofikwa na huzuni ya msiba huu!
Apumzike pema Patrick Mafisango.
ETERNAL REST GRANT HIM OH, Lord AND, LET PERPETUAL LIGHT SHINE UPON HIM.
AMEN.

0 Maoni/comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ