Next
Previous
Showing posts with label Usiku wa Matumaini. Show all posts

Sunday, July 7, 2013

0

MATOKEO: PAMBANO LA WOLPER NA HALIMA MDEE | BULAYA NA AUNT EZEKIEL

Posted in , , , ,
mapambano yote, la Bulaya vs Aunt Ezekiel na Halima Mdee vs Jackline Wolper ni DROO.
0

TAMASHA LA MATUMAINI: RAY KIGOSI APATA USHINDI WA MEZANI BAADA ZITTO KABWE KUTOKUEPO

Posted in , ,
Mwigizaji Ray na mbunge Zitto Kabwe pambano halijafanyika, Mh Zitto alipata dharura. ‎

Friday, July 5, 2013

0

RAISI KIKWETE KUWA REFA MECHI YA WABUNGE (USIKU WA MATUMAINI)

Posted in ,


Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, amekubali kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Usiku wa Matumaini litakalo fanyika Jumapili hii, Julai 7 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Aidha, Rais atahutubia katika tamasha na pia atakuwa refa wa mechi za wabunge wa Yanga na Simba.
0

USIKU WA MATUMAINI: RAISI KIKWETE KUWA MGENI RASMI

Posted in , ,



RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Matumaini ambalo litafanyika keshokutwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Mratibu wa tamasha hilo, Abdallah Mrisho, amesema Rais Kikwete ambaye hivi karibuni alikuwa na ugeni mkubwa wa Rais wa Marekani, Barack Obama, amekubali kuwa mgeni rasmi ambapo atatoa neno la matumaini kwa maelfu ya watu watakaojitokeza uwanjani hapo.
Akizungumzia zaidi juu ya ugeni huo mkubwa, Mrisho alisema: “Rais Kikwete amekubali ombi letu la kuwa mgeni rasmi, atatumia nafasi hiyo kutoa neno la matumaini kwa wote watakaojitokeza uwanjani hapo.
“Rais pia ndiye atakayefungua mechi ya Wabunge wa Simba dhidi ya Yanga ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa. Kama ujuavyo rais wetu ni mtu wa watu na ni mpenda michezo, hilo linajulikana siku zote.”

Aidha, Mrisho aliongeza kwa kusema kuwa shabaha ya tamasha hilo ni kuamsha upya imani ya Watanzania kwa nchi yao. Kuwafanya wawe wazalendo na kila mmoja kujiona analo jukumu la kufanya, kuhakikisha Tanzania yetu inapiga hatua.
“Mbali na Rais Kikwete, wengine watakaotoa neno la matumaini siku hiyo ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, January Makamba na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, Eric Shigongo.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ