
Dj wa kwanza wa kike nchini Tanzania Fatma Hassan aka Dj Fetty wa Clouds
Fm amepewa heshima ya kuwa Dj wa kwanza wa kike kutoka Afrika Mashariki
kutumbuiza kwenye mashindano ya Big Brother Africa.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook Fetty amesema, “Juma mosi hii na
jumapili nitakua nikispin ndani ya Jumba la BBA STARGAME, nitume kwa
kuniandikia playlist itakayo wapagawisha…na shinda very nice cape ya big
brother na high quality Tshirt kutoka CloudsFm…legoooooo.”
Fetty ambaye kwa muda alikuwa amepumzika shughuli za udj na kuendelea
na utangazaji wa kawaida, amesema imemlazimu kujifua tena ili
kuhakikisha kuwa ‘haangushi maembe’ (kumix vibaya nyimbo) wakati
atakapokuwa akipiga ngoma.
Amesema mwaliko huo ameupata katikati ya mwezi May na tangu hapo
amekuwa akijikumbushia ujuzi kwenye ‘wheels of steel’ kwakuwa hiyo ni
nafasi kubwa inayohitaji maandalizi ya kutosha.
Mwaka jana Dj wa kike kutoka kituo cha radio cha YFM cha Ghana Nana
Kessewa Adu aka DJ Kess alialikwa pia kuburudisha kwenye Big Brother
Amplified.
Hiyo si mara ya kwanza kwa Dj wa Clouds FM kupata mwaliko huo. Mwaka
jana Dj Steve B naye alipewa fursa hiyo ya kuonesha ujuzi wa mikono yake
kwenye 1 and 2!
Source: bongo5.com