Friday, December 20, 2013

0

KAMA HUWEZI YA RAMA DEE NA JAY DEE KUFANYIWA VIDEO NDANI YA NCHI TATU

Posted in ,

Msanii mkongwe wa r&b Bongo, Rama Dee ambaye anamiliki tuzo ya wimbo bora wa RnB aliyoichukua kupitia wimbo wake wa ‘Kuwa na subira’, ambaye kwa sasa maskani yake yapo sana Australi ambapo anaisi na mkewe wakiwa na mtoto mmoja amefunguka juu ya mpango wake wa kushuti video ya ‘Kama huwezi’.

http://baabkubwamagazine.com/wp-content/uploads/2013/12/Rama-dee1.jpg‘Kama huwezi’ ni wimbo aliomshirikisha mwanadada Lady Jay Dee ambao umekuwa gumzo sana kiasi cha watu wengi kuhitaji kuona kwenye video ile chemist iliyotumika kuitengeneza ngoma hiyo kiasi cha watu wengine kutengeneza slide show yenye wimbo huo na kuitupia youtube huku ikikamata viewers kibao. Akizungumza kwa njia ya simu ndani ya Power Jams ya East Africa Radio alifunguka juu ya sababu inayoichelewesha video hiyo.
“Nia yangu ipo palepale kwamba ‘Kama Huwezi’ itahusisha nchi tatu kama location ya video hiyo. Nchi hizo ni hapa Australia, South Africa ambapo ndege nitakayopanda kuja nayo Dar itapita na kukaa muda mrefu kabla ya kuja huko na mwisho ni Tanzania jijini Dar es salaam ambapo ndipo hata shot zote za Jide zitapigwa hapo.” – Rama Dee.

“Sasa tatizo ninalokutana nalo ni kwamba kwenye hizi nchi nyingine wanahitaji muda mrefu sana hadi kufanya video kwa uhuru hadi waangalie kwanza video zetu huwa zina nini hasa but lazima nitafanya na pia zipo video nyingi sana ambazo nimeshazifanya zinakuja, kwa kifupi fans wangu wategemee makubwa kutoka kwangu na uzuri kwa sasa nipo likizo ya masomo yangu ya muziki ambayo nimeamua kusomea ili kujiongezea ujuzi zaidi.” – Rama Dee.














0 Maoni/comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ