Tuesday, April 23, 2013

0

NA SOKA IN BONGO: GERRARD KUCHEZEWA MECHI MAALUM, RIO KUONGEZEWA MKATABA!

Posted in , ,
>>MECHI YA GERRARD; LIVERPOOL v OLYMPIAKOS, ANFIELD AGOSTI 3!
>>RIO MKATABA MPYA, SCHOLES KUSTAAFU!!
NAHODHA wa Liverpool, Steven Gerrard, ili kumtukuza, atachezewa Mechi maalumUwanjani Anfield na huko Old Trafford, Mabingwa wapya wa England, Manchester United, wamedokeza kuwa Beki wao Rio Ferdinand atasaini Mkataba mpya.
STEVEN GERRARD: KUENZIWA KWA MECHI MAALUM!
Liverpool wametangaza kuwa Nahodha wao Steven Gerrard, Miaka 32, atatukuzwa kwa kuwekewa Mechi maalum hapo Agosti 3 Uwanjani Anfield Liverpool watakapocheza na Olympiakos ya Ugiriki.
Pesa zitakazoingizwa kwenye Mechi hiyo zitakwenda kwenye Mfuko wa Hisani wa Steven Gerrard.
Gerrard ameichezea Liverpool Mechi 439 za Ligi tangu Novemba 1998.
+++++++++++++++++++++++
GERRARD-Historia:
-Mechi 628 kuichezea Liverpool
-Mabao 159 kwa Liverpool
-Mataji:
=1 Champions League
RIO_NA_UBINGWA=1 Uefa Cup
=2 FA Cup
=2 Kombe la Ligi
+++++++++++++++++++++++
Hapo Tarehe 29 Novemba 1998, Steven Gerrard aliichezea Liverpool Mechi yake ya kwanza kwenye BPL, Barclays Premier League, dhidi ya Blackburn Rovers.
Mwaka 2003, Steven Gerrard alimrithi Sami Hyypia na kuwa Nahodha wa Liverpool.
Katika Misimu ya 2004-05, 2005-06 na 2008-09, Gerrard ndie alikuwa Mfungaji Bora wa Klabu ambae ameifungia Jumla ya Mabao 159 katika Mechi 628.
Mkataba wa sasa wa Gerrard unamalizika mwishoni mwa Msimu wa 2013/14.
RIO FERDINAND KUPEWA MKATABA MPYA MANCHESTER UNITED
Rio Ferdinand anatarajiwa kusaini Mkataba mpya wa Mwaka mmoja kabla ya mwisho wa Msimu huu mara tu baada ya jana Klabu yake Manchester United kutwaa Ubingwa wa England kwa mara ya 20.
Zipo ripoti kuwa Ferdinand, Miaka 34, amepewa Ofa za kuvutia kucheza huko China na USA lakini matakwa yake mwenyewe ni kucheza Old Trafford.
Msimu huu, baada ya kuandamwa na majeruhi mfululizo Msimu uliopita, Rio Ferdinand, ambae anatimiza Miaka 11 kuwepo Man United, alikuwa moja ya nguzo thabiti ya Timu yake na kuiwezesha kutwaa Ubingwa huku wakiwa na Mechi 4 mkononi.
Wakati Ferdinand anatarajiwa kuongeza Mkataba, Kiungo Veterani, Paul Scholes, ambae amekuwa nje ya Uwanja tangu Januari 26, anategemewa kustaafu mwishoni mwa Msimu.
Msimuu huu, Scholes ameichezea Man United mara 19.

0 Maoni/comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ