PREZZO KUFANYA SHOW DAR HIVI KARIBUNI
Posted in A.Y, Prezzo, Shosteez
Ule wakati uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu kwa rapper kutoka Kenya maarufu kama Amb Prezzo kuja kupiga show ndani ya jiji la Dar Es Salaam sasa umewadia.
Prezzo anatarajia kupiga show moja katika ukumbi disco wa New Maisha Club, Oysterbay jijini Dar.
Katika show hiyo Prezzo atasindikizwa na baadhi ya wasanii kutoka Bongo kama kundi la Shosteez, Stereo, AY, MwanaFA na wengine wengi. Show hii inatarajia kufanyika tarehe 5 April mwaka huu.
0 Maoni/comments: