DIAMOND PLATNUMZ AAIRISHA TOUR YA EUROPE
Posted in Diamond Platnumz
Msanii wa kizazi kipya nchini Tanzania, Diamond Platnumz atosa shows mbili alizokuwa akafanye huko Europe. Diamond anaefanya vizuri kwenye muziki sasa hivi na kujipatia mashabiki wengi ikiwemo nje ya nchi ametoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa facebook kwa mashabiki hao kuhusiana na show aliyokuwa akafanye huko.
Diamond akitoa sababu, alisema hatakuweko kama ilivyotangazwa mwezi huu na ni kwa sababu Kampuni/Promoter hao kushindwa kufikia mahitaji yaliyokuwa yakihitajika ikiwemo pesa pia.
Kupitia ukurasa huo, Diamond aliwaambia fans kuwa yeye na WASAFI hawatakuja kama ilivyotangazwa tarehe 15 mwezi huu na kwamba wasubiri mpaka atakaposema tena.
0 Maoni/comments: