BEN POL KUACHIA ALBUM HIVI KARIBUNI
Posted in Ben Pol
Mwanamuziki wa miondoko ya RnB, Bernard Paul maarufu kama Ben Pol ambae bado anafanya vizuri kwenye hii tasnia ya muziki wa hapa nyumbani, anategemea kuachia album yake hivi karibuni.
Ben Pol ambae anatamba sana na wimbo wake wa PETE, sasa yuko mbioni kuachia Album yake hiyo ambayo itakwenda kwa jina la ''Ben Pol Love CD'' mwishoni mwa mwezi huu.
Ben kwa sasa yupo katika hatua ya mwisho ya kuikamilisha album hiyo ambayo itakuwa na mchanganyiko wa nyimbo za zamani na mpya ambazo bado hazijasikika kabisa.
0 Maoni/comments: