Thursday, August 30, 2012

0

Je Wajua Kwanini Nigeria Yaongoza Afrika Kwa Soko La Filamu??(Secret To Nollywood's Success)

Posted in ,
Ieleweke Kuwa, Nollywood inatengeneza zaidi ya Movie 1000 kwa Mwaka, Na Si kwamba waigizaji toka Nchini Nigeria ni Wengi, Bali ni Mipango tu. Nollywood imekuwa sana katika miaka ya karibuni na kuliteka soko la Filamu la Dunia kutokana na Maudhui na Hadithi zinazoelezewa atika Movie hizo.
The set of
Utengenezaji wa Movie Mpya 'Journey To Self' Itakayohusu Maisha Ya Kirafiki Ya Marafiki wanne




Ijapokua Nollywood imeendelea teka soko, wengi wanasema imeshika chati kutokana na kujali na kendeleza tamaduni ta Nyumbani na Za Kiafrika kwa ujumla. Muongoza Filamu Lancelot Imasuen, ambaye kwa sasa anatengeneza filamu itakayogharimu kiasi cha Dolla Millioni Mbili itakayoitwa ''Invasion 1987'' anasema Filamu za Nollywood zinatengeneza na wanigeria na waafrika wote kwa ujumla.

''Watu Wanapata Sababu Zaidi na Zaidi, Wanapata machungu, Pia Wanapata msisimko, kwa sababu filamu ziko kiukweli zaidi.''-Lancelot Imasuen, Director


Imasuen ambaye ni miongoni mwa waanzilishi akiwa na miaka zaidi ya 10, wakati akiendelea Kuongea na CNN Alisema, Mandhari inayotumiwa Nollywood, inawafanya watazamaji kujiskia na kujihisi ni sehemu ya Hadithi.
Ndo maana anasemahii ndio faida kubwa walio nao ukilinganisha na Hollywood.

Wakati akiongea na CNN alimaliza kwa Kusema "Sisi tumekuwa na uwezo wa kujenga profile yetu kwa zaidi ya miaka," ALiendelea Kusema, "Sisi tuko tayari kwa ajili ya mabadiliko, tuko tayari kwa wakati huu na bado tunataka kudumisha njia ya KiNigeria ya kufanya filamu, lakini katika utandawazi zaidi."

0 Maoni/comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ