Diamond Platnumz Big Brother Perfomance
Posted in Big Brother Africa, Big Brother Africa Star Game, Diamond PlatnumzJana (May 27) kwenye Big Brother eviction day, Diamond ameifanya Tanzania na Afrika Mashariki kujivunia kwa kudondosha show ya kufa mtu.
Akiwa amevalia shati jeupe, neck tie, mkoti mweusi, suruali nyekundu na miwani mieusi alivyovikwa na si mwingine zaidi ya mwandani wake Jokate Mwegelo aka Kidoti, Diamond alionesha kuwa Tanzania muziki upo!
“Diamond, wearing Kidoti, all the way representing, 4 the 2nd tym kidoti represent kwa BBA7! Proud of u sicy!”
Kwa performance yake iliyowatoa vinywele vya baridi (goose bumps ) watanzania na watazamaji wengine wa Afrika Mashariki, mtangazaji rasmi wa Big Brother IK amemtunuku rasmi jina la ‘R.Kelly wa Tanzania.’
“And @ik_osakioduwa @diamondplatnumz is officially the 'R. Kelly of Tanzania'.
Watu maarufu na wa kawaida Afrika Mashariki nzima wamempa Diamond nyota tano begani kwa kuwakilisha vyema jana.
marya ogopadjs @maryaogopadjs
“Tz your BOY @diamondplatnumz leo ametoklezea yake yote. He made EA proud. "Nenda kamwambie" amefanya poa.”
Wengine walienda mbali zaidi hadi kusema show yake imeifunika show ya J.Cole wa Marekani aliyetumbuiza siku ya ufunguzi wa Big Brother Africa 2012 “Yes he did!proud of him!RT @AyTanzania: RT @HUDDAHMONROE: He @diamondplatnumz has done it,better than J Cole, we should appreciate our own.”
Baada ya kumaliza show ya kwanza @diamondplatnumz hakusita kutaka kujua watanzania wameionaje na kuamua kuwauliza “Hiyo ni ya kwanza ndugu zangu? Imekuaje? Ya pili nakuja na Dancers#teamProudlyTanzanian”.
Hakuna kilichoandikwa zaidi ya kumpongeza kwa kazi yake;”
RT @Chrisintah: Proudly Tanzanian RT @jokateM: S/O to @diamondplatnumz for repping #Tanzania vizuuurriiiiiii on the #BBA7.”
#Proudly East African. # RT @HUDDAHMONROE: Huyu @diamondplatnumz @AyTanzania ako juu sana.1st great performance on #BIGBROAFRICA .Proudly East African. #One♥.”
Hamisi Mandi @BDozen
Show kali...umetisheer!!”
ChannelOAfrica @ChannelOAfrica
“Hongera sana Diamond umewakilisha vizuri Tanzania.” @diamondplatnumz #OriginalAfricanFamily
Kilimanjaro Lager @Kili_Lager
“Pongezi kwa @diamondplatnumz kwa show nzuri ndani ya @BigBroAfrica usiku huu. 100% Tanzanian Flava”.
@cremedj: Diamond has killed it on “Bigbrother!!!!whaaaaat!!havent seen a performance like that on Bigbrother.”
Baada ya show hiyo Diamond hakusita kutoa shukrani zake kwa watanzania, “Watanzaniaaa, nashukuru sana kwa Support yenuu, bila nyinyi me si kitu, God bless Africa,God bless Tanzania, God bless Diamond Platnumz.”
Akaongeza nyingine, “WaTz, wenzangu bila nyinyi mimi si kitu, nawashukuru sana kwa maombi yenu, pia namshukuru Mamangu mzazi, na woote mnaonisupport! One Love.”
Bila shaka show hiyo ya jana ya Diamond itamfungulia milango mingi ya show za kimataifa kama hizo. All the best homeboy, tunajivunia sana kwa kutuwakilisha vyema.
0 Maoni/comments: