Picha Za SIMBA SC Trophy Tour DarLIVE
Posted in Juma Kaseja, Patrick Mutesa Mafisango, Simba SC
KIPA wa Simba, Juma Kaseja
jioni hii ameshindwa kujizuia lilipotajwa jina la Patrick Mafisango
kwenye sherehe za ubingwa wa Ligi Kuu ya klabu hiyo na kujikuta akimwaga
machozi kwenye ukumbi wa Dar Live, Mbagala, Dar es Salaam.
Kaseja alimwaga machozi
wakati alipokuwa akipokea Medali kwa niaba ya marehemu Mafisango
aliyefariki dunia wiki iliyopita kwa ajali ya gari maeneo ya Keko, Dar
es Salaam ambapo alizikwa kwao DRC siku tatu baadae.
Kiungo wa Simba, Salum
Machaku aliitoa Medali aliyokabidhiwa kwenye sherehe hizo kwa marehemu
Mafisango ambapo Kaseja alinyamaza baada ya kubembelezwa na wachezaji
wenzake na kuendelea na shughuli hiyo iliyofana na kuhudhuriwa na mamia
ya wapenzi wa klabu hiyo.
Ukumbi pamoja na mapambo
yaliyowekwa, ulipendeza zaidi kwa mavazi ya mashabiki wa Simba ya rangi
nyekundu na nyeupe ambapo Meneja wa Global Publishers Limited, Abdallah
Mrisho alikabidhi Sh. Milioni 3 kwa Kaseja kama zawadi yao kwa Simba
kutokana na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu.
Baada ya yote hayo, wachezaji
na viongozi wa Simba walifungua shampeni na sherehe ikaanza rasmi, bendi
ya Msongo Ngoma ikianza kutumbuiza, ikiongozwa na mwimbaji wake
mkongwe, shabiki maarufu wa Simba, Mzee Muhiddin Mwalimu Gurumo. (Stori imeandikwa na Bin Zubery wa Bongostaz.blogspot.com )
0 Maoni/comments: