Next
Previous
Showing posts with label Steve Nyerere. Show all posts

Tuesday, August 6, 2013

0

TV SHOW YA IRENE UWOYA KUSHIRIKISHA NYOTA KADHAA (HAWA NDO WALIOSHIRIKISHWA KWA SASA)

Posted in , , , , ,


“Nafurahi kuona jinsi kioo cha jamii hivi sasa kimeigusa familia kabisa, ukizungumzia nyumba unagusa swala la familia ambalo ndiyo msingi wa Taifa lolote.” Haya yalikuwa ni baadhi ya maneno ya Mtitu, mmoja kati ya watu maarufu ambao walihusika kwenye show ya Irene Uwoya. Katika harakati za kutengeneza kipindi chake, Irene amekutana na mastaa tofauti na kuzungumza nao mambo mengi ambayo yatakuwa kwenye show yake. Chukua time yako ya kuona jinsi ilivyokuwa na upate sababu nyingine ya kuangalia hii show kupitia @CloudsTV na pia unaweza kucheki promo yake hapo pembeni.
Mtitu wa 5effects

Thursday, July 5, 2012

0

Steve Nyerere amkabidhi Mama Maria Nyerere Zawadi ya Movie

Posted in ,
Mwigizaji wa filamu nchini Steve Mangele ‘Steve Nyerere amekabidhi filamu yake ya Mwalimu Nyerere kwa mke wa Hayati Mwalimu Julius Nyerere, Mama Maria Nyerere ikiwa kama shukrani zake,baada ya mama huyo kumsaidia katika kukamilisha filamu hiyo ambayo aliifanyia Butiama.
Steve alisema kwamba kumpa filamu hiyo ni kuweka kumbukumbu kwamba, anathamini msaada na mchango wake katika filamu hiyo na hana kikubwa cha kumpa wala cha kumfanyia zaidi.
Amesema, Mama Maria Nyerere alimsaidia sana kujifunza mengi kumhusu baba wetu wa taifa ikiwemo kumuonyesha vitu gani Mwalimu alikuwa akifanya, na vitu gani mwalimu alikuwa akivipenda,na hata na sehemu ambazo mwalimu alipenda kukaa baada ya kazi zake.
Pia ametoa shukrani kwa wasanii wenzake ambao walijitahidi katika hali moja au nyingine kuhakikisha filamu hiyo ilikamilika.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ