Next
Previous
Showing posts with label Bongo Movies. Show all posts

Wednesday, January 29, 2014

0

HUYU NDIYE MSANII WA BONGO MOVIE ALIYEJINYONGA GESTI

Posted in ,
Marehemu Victor Peter enzi za uhai wake.
MSANII Victor Peter kutoka Bongo Movie amefariki dunia usiku wa jana kuamkia leo 28/01/2014 kwa kujinyonga katika gest moja iliyotambulika kwa jina la SAFARI JUNIOUR ilioko maeneo ya Kisosora huko mkoani Tanga.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo,tulipofatilia tukio hilo ilifanikiwa kuongea na mmoja kati ya wasanii walioshirikishwa na marehemu katika filamu yake ya
mwisho kabla ya kujinyonga huku filamu yake ya kwanza ikiwa bado haijatoka na kuingia sokoni yenye jina la CHOZI.

Msanii huyo aliyetambulika kwa jina la usanii Koba aliiambia kwamba siku moja kabla ya tukio Victor alifanya nao Shuting ya filamu iliotambulika kwa jina OUR FAMILY ambayo ilikuwa ndio filamu ya marehemu Vicktor ya pili tangu ajikite katika tasnia ya filamu Bongo Movie,

MSEMAJI

Cha kushangaza ni kwamba filamu hiyo muhusika mkuu alikuwa ni marehemu Vicktor na katika filamu hiyo alicheza kwamba kuna msiba baba yake kafa na yeye mwenyewe mwisho wa filamu Picha yake hiyo mnayoiona hapo juu ilipigwa Ex na muhusika aliyecheza kama mdogo wake, Matokeo yake alivyomaliza kushut aliondoka na wasanii kadhaa wakaelekea katika ATM iliokwepo maeneo ya mjini kutoa hela ili awalipe wasanii walihusika katika kazi yake,

KABLA YA TUKIO

Kwa bahati mbaya ATM machine ikagomagoma kwa tatizo kidogo la kimtandao katika kusubiria mtandao ukae sawa marehemu Vicktor alibadilika na kuonekana kama amechanganyikiwa na kuonekana hayuko sawa, Basi kwa bahati nzuri baada ya mda mchache ATM ilikaa vizuri na yeye mwenyewe ile hali ikatulia akatoa hela wakaelekea Hospitali ya Ngamiani huko mkoani Tanga,
Kufika Ngamiani daktari akatoa tamko kwamba apelekwe Hospitali kuu Bombo.

UCHUNGUZI

Kufika Bombo akapimwa kila kitu na kukutwa mzima hana tatizo lolote lile ikabidi warudi Gest walikofikia huko maeneo ya Kisosora, Marehemu akawalipa wasanii wote na kuwauliza kuwa kuna mtu anaemdai? Wakamjibu hakuna. Kila msanii akaingia chumbani kwake na kuendelea na zake, Kwa wakati ule marehemu aliingia chumbani kwake na kwakuwa ni Self Contain si rahisi kumuona mtu akitoka nje hovyo hovyo.

Tuesday, August 6, 2013

0

ONA PICHA ZA BEHIND THE SCENE ZA MOVIE ALIYOIGIZA MAMA KANUMBA, LINAH PAMOJA NA LULU

Posted in , , ,
Muigizaji maarufu Swahiliwood Elizabeth Michael(Lulu) na mama Kanumba(Flora Mtegoa) kwa mara ya kwanza wanakuja na filamu inayoitwa Mapenzi ya Mungu. Katika filamu hiyo waigizaji wengine ni Linah Sanga ambaye ni mwanamuziki maarufu wa Bongofleva na Sudi Ali. Angalia baadhi ya picha za behind the scenes za filamu hiyo
Lulu na Linah
 

Friday, August 2, 2013

0

BAADA YA NYOTA KADHAA WA BONGO MOVIE KUANZA KUIMBA, SASA WEMA SEPETU NAYE KUANZA

Posted in ,
Wema Sepetu miss Tanzania aliyegeuka kuwa muigizaji, ameweka wazi kwamba anataka kuimba na katika kuthibitisha hilo ameshaandika mistari kadhaa ya anachotaka kuimba. Wema alishawahi kuimba kwenye wimbo wa kuhamasisha kumchangia msanii Sajuki wakati anaumwa. Wimbo huo unaitwa “Mboni yangu”, so kuingia kwenye booth kurekodi wimbo sio kitu kipya kwa Wema Sepetu. Hii ni baadhi ya mistari ambayo ameshaandika Wema Sepetu kwa ajili ya wimbo huo.

Mwambie wake ni mimi, na kwangu moyoni atabaki ni yeye, tena mwambie bado silali kutwa nawaza penzi langu… ila siku atakugundua kuwa mi ndo mwenyewe..................

Mpaka sasa hivi ni wimbo mmoja Wema alirekodi kwa kushirikiana na Snura ambapo Tunda Man alishiriki pia kuuandika.

Thursday, August 1, 2013

0

HUYU NDO MSANII WA BONGO MOVIE MWENYE ALIYEUMBULIWA KWA MADENI

Posted in ,


STAA wa filamu za Kibongo, Coletha Raymond ‘Koleta’ kwa mara nyingine tena amekumbwa na tuhuma za kukwepa kulipa deni la shilingi 400,000 analodaiwa na staa mwenzake, Husna Iddi ‘Sajenti’..

Kwa mujibu wa chanzo chetu, Koleta alikopa nguo kwenye duka la Sajenti kwa maelezo kwamba angelipa jioni ya siku hiyo lakini mpaka sasa ni miezi saba imepita bila msanii huyo kulipa deni hilo.

Ikazidi kudaiwa kuwa hata Sajenti anapompigia simu Koleta ili kumuulizia kuhusu deni hilo, msanii huyo hapokei simu, hali inayotoa tafsiri kwamba anataka kumdhulumu.

Wednesday, July 31, 2013

0

TRAILER YA MOVIE YA KUMUENZI MAREHEMU KANUMBA (AFTER DEATH) | IKO SOKONI HIVI SASA

Posted in ,

Wednesday, July 24, 2013

0

RAMADHAN SPECIAL: NEW BONGO MOVIE "EDA" COMING SOON

Posted in ,
Poster-24x36 (1)2


EDA  ni kipindi kisichopungua miezi mitatu ambacho anapaswa kukaa mwanamke bila kuolewa wala kushirikiana na mwanamume ama baada ya kutengana na mumewe au baada ya kufiwa na mume.Hii ni kwa mujibu wa dini ya kiislam.
EDA ni filam inayochambua changamoto za maisha ya ndoa katika familia nyingi.


Ndani ya filamu hii yumo Ussi Hajji  kama YUSSUF. Marry Mwita kama YUSRA.Hidaya Njaidi na Abrahman Thomas kama wazazi wa Yusuf.Hashim Kambi na Khadija Ibrahim kama wazazi wa Yusra. Gerry wa Rymes kama OMAR rafiki wa YUSSUF, Sabrina Rupia kama KHAYRA mtumishi wa kampuni ya YUSSUF na rafiki wa yusra. Ahmed Olotu kama mwalimu wa dini. n.k

YUSSUF  ni mtu mwenye uwezo  mzuri kimaisha na wanaishi maisha ya furaha na  uchamungu na mkewe YUSRA.YUSSUF yuko busy sana na masuala ya kazi, wanachelewa kupata mtoto jambo linalopelekea wazazi wa YUSSUF kumsakama  mtoto wao wakitaka amwache mkewe wakidhani ndiye mwenye tatizo.

Huku wazazi wa YUSRA wakimsakama mtoto wao wakitaka atafute suluhisho mapema kabla tatizo hilo halijazua mtafaruku. YUSSUF na YUSRA wanakuwa katika hali ya mashaka ingawa wataalamu wa afya wamewathibitishia kuwa hakuna mwenye tatizo kati yao.

  Jambo hili linawafanya wawashirikishe hata marafiki kwa nyakati tofauti. Hatimaye YUSRA anatafuta ushauri  kwa KHAYRA ili kunusuru ndoa yake.

KHAYRA anamtumbukiza katika njia ngumu. YUSRA anaomba pesa toka kwa mumewe afanye biashara. YUSSUF anampa milioni tano.YUSRA anchukua pesa hizo na kumpelekea OMAR, rafiki wa mumewe. Anamwomba awe naye ili apate ujauzito kama alivyoshauriwa na KHAYRA, anusuru ndoa yake.

Lakini OMAR anamwogopa MUNGU na kuthamini utu wake. Anakataa na kumrudishia taarifa hizo YUSSUF akimwomba amkanye mkewe.

 YUSSUF anakasirika na kumpa talaka moja mkewe. Wazazi wanachanganyikiwa . mama yake YUSRA anamlaumu mwanawe kwa kuchukua ushauri toka kwa rafiki  asiye na ushauri mwema.

YUSRA anaingia katika EDA ya talaka…. Kwa mujibu wa sheria ya kiislam.

Siku 7 kabla ya EDA kwisha. Mama YUSRA anampigia simu YUSSUF kuwa mkewe yu mjamzito. YUSSUF anafurahi sana.  Ananuwia kumrejea mkewe.

Akiwa njiani kwenda kumrejea mkewe anapata ajali na kukutwa na mauti. Jambo linalomfanya YUSRA kuingia katika EDA nyingine ya kufiwa na mume kwa mujibu wa sheria ya kiislam.

HII NI BONGE LA FILAMU KUTOKA TANZANIA NA IKO NJIANI, ITATOKA TAREHE 27 MWEZI HUU … YAANI JUMATATU … KAA MKAO WA KULA.

Wednesday, July 17, 2013

0

BAADA YA NDAUKA, SASA MZEE MAGALI NAYE AAMUA KUIMBA BONGO FLEVA

Posted in , , ,

cd (8)

Wiki kadhaa zilizopita msanii wa bongomovie Rose Ndauka alishirikishwa kwenye collabo na kundi la TNG Squard kwenye wimbo wao mpya, baada ya hapo idadi ya wasanii wa bongomovie ambao wanafanya muziki ilizidi kuongezeka wakiwafuata wakina Snura na Shilole.
Leo hii msanii mkongwe na maarufu sana kwa kuigiza kama mtu katili au wakati mwingine mtu tajiri Mzee Magari, ametoa wimbo wake unaitwa “Dar Raha” ambapo kwenye interview na millardayo.com Mzee Magari anasema “Ninampango wa kuifanya fani hii ya muziki kuwa serious kama ilivyo kwa upande wa movie, sijatoa huu wimbo kwa kujifurahisha bali muziki pia ni kitu ninachokipenda…. kuna baadhi ya wasanii wanafahamu historia yangu na muziki kabla hata sijaanza kuigiza movie“.

Thursday, June 27, 2013

0

VIPANDE VINAVYOCHOCHEA NGONO, VYASABABISHA MUVI YA AUNTY EZEKIEL KUFUNGIWA

Posted in ,


SERIKALI kupitia bodi ya filamu nchini imemkalia kooni mwigizaji, Aunt Ezekiel na kumtaka aondoe baadhi ya vipande vya sinema yake mpya iitwayo Scola vinginevyo haitaruhusiwa kuingia mtaani.

Taarifa kutoka ndani ya bodi hiyo inayosimamia maadili ya sinema za Kitanzania, imeeleza kuwa Aunt aliipeleka  filamu hiyo ili ikakaguliwe kama zilivyo taratibu lakini bahati mbaya ikagundulika kuna ‘sini’ tatu ambazo zilitoka nje ya maadili ya mtanzania.


“Kuna vipande vitatu ambavyo kimsingi vimevuka matakwa ya maadili ya Kitanzania hivyo hakuna jinsi, lazima avitoe kama anataka kuiingiza sokoni sinema hiyo,” kilieleza chanzo makini ndani ya bodi hiyo kilichoomba hifadhi ya jina.

Tuesday, June 18, 2013

0

HII NDO SABABU ALIYOTOA RAY KIGOSI JUU YA KAMPUNI YAKE (RJ) KUWA BORA KWA UZALISHAJI HAPA TANZANIA

Posted in , ,

IMG_4726
Mwigizaji bora wa kiume 2012 ni JB

Mwigizaji bora wa kike 2012 ni Irene Uwoya.
baadhi ya washindi wengine ni pamoja na:

Best movie 2012 ni Kijiji cha Tambua haki ya marehemu Kanumba
Movie iliyouza sana 2012 ni Ndoa yangu ya Steven Kanumba.
Best Action movie ni ya Jimmy Master ya Double J
Best Negative role ameshinda Chek budi
Mwigizaji bora chipukizi ni Niva.
Best Supporting Actress ni Riyama Ally
Mwigizaji bora chipukizi wa kike ni Irene Paul.
Mchekeshaji bora 2012 ni King Majuto
Mwongozaji bora wa filamu 2012 ni Vicent Kigosi (Ray)

Saturday, May 11, 2013

0

BONGO MOVIE YATUMIA PICHA MOJA YA J.B KATIKA COVER 3 ZA MOVIE TOFAUTI: JE TUSEME WANAKOSA UBUNIFU, MAPOZI AU NI UKATA??

Posted in ,
392479_372964486060069_1289403138_n


417781_565255566830959_1850361456_nlerato
Cover ndiyo kitu cha kwanza kumvutia mnunuzi wa movie hata kabla hajaiona trailer ya movie au kusoma intro ya story ya movie kwenye cover. Sasa inakuaje waandaji wa movie wanashinda kutafuta picha mpya ya muigizaji mkubwa kama JB kwa ajili ya cover ya movie. Picha hii ya JB akiwa amevaa mawani na koti ya kaki, kwa mara ya kwanza  ilitumika kwenye movie ya Lerato, then baadaye ikatumika kwenye movie ya I think I hate my wife…leo tena wameitumia picha hiyo hiyo kwenye movie ya Innocent Case..jamani kupiga picha mpya siyo gharama kubwa na JB anapicha nyingi kali na sio hii tu kila siku.Tubadilike na tujali brand na ubora wa kazi.


JE TUSEME WANAKOSA UBUNIFU, MAPOZI AU UKATA??

Friday, May 3, 2013

0

LULU NAYE AYALALAMIKIA MAGAZETI YA UDAKU

Posted in , ,
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjEjK1MDkUP65ibqe7c-aXfcFPt2bIkaw227EY1ftG8Ov6_dsyBl4UP6vPt4mxIpBY9P5SPky7a3Qgxh7wirdPcq0pciC1tRmyj3cnNMsbNWai4WWmp5gdTtdY-qEjSjEWizRUVmS_xfAs/s1600/L2.jpg
Katika kile kinachoonekana kukerwa na vitendo vya vyombo vingi vya habari hususani magazeti ya kadhaa ya udaku yanoyochapisha habari za uongo kuhusu wasanii wa bongo movies kwa ajili ya kuuza magazeti yao, hatimaye msanii Elizabeth Michael  “lulu”naye ameamua kuyaweka wazi ya moyoni mwake bila kuficha baada ya gazeti  moja pendwa (Jina tunalihifadhi) kuchapisha habari iliyopew kichwa kisemacho “Lulu, wema, Diamond afya mgogoro”ambayo imeonekana dhahiri kumkera mrembo huyu na kuamua kaundika haya yafuatayo kwenye ukurasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii.
“..Imekuwa ni kawaida ya mtu kujisikia kusema chochote...muda mwingine mnaweza mkahisi hatuoni au mkahisi kukaa kwetu kimya ni wajinga!!mm kama mm napenda kuwajulisha kuwa LULU mliyekuwa mnamjua sio LULU wa ss...msitegemee kusikia nabisha au kupigizana kelele...fanyeni kazi yenu lakini sio kuchafuana na kuipotosha jamii....!!!nadhani kimya changu kina majibu mengi.. Lulu anakuwa msanii wa pili kwa kipindi cha wiki mbili kukasirika hadharani baada ya mwanadada batuli kulaani kitendo cha gazeti moja la udaku kuandika habari za uongo kuhusu yeye.

Wednesday, May 1, 2013

0

HUU NDO MUONEKANO WA SASA WA MTOTO WA IRENE UWOYA

Posted in ,
irene
IRENE UWOYA AKIWA NA MWANAYE
0

UNAJUA KWANINI JACKLINE WOLPER ANATUMIA JINA LA “WOLPER GAMBE”

Posted in ,
WOLPER GAMBE STYLE
Ukiingia kwenye mitandao ya kijamii…so called Amber-Rose lakini si tunamjua  as Jacklyne Wolper, pande hizo anajiita Wolper Gambe. Jina limetoka la Wolper Gambe limetoka wapi? Gambe maana yake si pombe kama bia na vitu vingi vingine, hiyo ndiyo iliwappa watu kadhaa hamu ya kujua kwanini anajiita hivyo baada ya kuona hadi ndinga yake kaitupia jina hilo kwa upande wa nyuma. Wolper huyu hapa anafunguka kuhusu hilo jina,

Tuesday, April 30, 2013

0

PICHA: LULU AKIWA NA MTOTO WA DR CHENI HAPA

Posted in ,
0

TAZAMA PICHA 8 ZA GARI MPYA YA JACKY WOLPER

Posted in ,
Publication1Jacky Wolper a.k.a Wolper Gambe right about now yupo on road na ndinga yake mpya “Mini Cooper”. Interesting issue kuhusu gari hili ni kwamba, kwa nyuma chini ya plate number mwanadada katupia maandishi ya steel kabisa kama yametoka kiwandani na gari lenyewe..yanasomeka “WOLPER GAMBE” ambalo ni jina analotumia kwenye mitandao mingi ya kijamii. Upande wa pili mpekuzi wa bongomovietz alivyomuuliza Wolper how much zimemtoka kuvuta ndinga hiyo akasema siri yake..nikatafute kwenye internet. Basi sawa.mtandao wa mini.co.za ambao ndio dealers wa Mini Cooper kusini mwa jangwa la Sahara(Sub Sahara Mini official dealers) wameonyesha price ya R233,462 kwa Mini Cooper yenye same look na ya Wolper tukizingatia version ya gari husika..ambapo kwa pesa za madafu ni Tsh 42,012,236.If so Wolper, we gat to hack your bank account…tuvute iyo michuzi na sisi.

Thursday, July 5, 2012

0

Steve Nyerere amkabidhi Mama Maria Nyerere Zawadi ya Movie

Posted in ,
Mwigizaji wa filamu nchini Steve Mangele ‘Steve Nyerere amekabidhi filamu yake ya Mwalimu Nyerere kwa mke wa Hayati Mwalimu Julius Nyerere, Mama Maria Nyerere ikiwa kama shukrani zake,baada ya mama huyo kumsaidia katika kukamilisha filamu hiyo ambayo aliifanyia Butiama.
Steve alisema kwamba kumpa filamu hiyo ni kuweka kumbukumbu kwamba, anathamini msaada na mchango wake katika filamu hiyo na hana kikubwa cha kumpa wala cha kumfanyia zaidi.
Amesema, Mama Maria Nyerere alimsaidia sana kujifunza mengi kumhusu baba wetu wa taifa ikiwemo kumuonyesha vitu gani Mwalimu alikuwa akifanya, na vitu gani mwalimu alikuwa akivipenda,na hata na sehemu ambazo mwalimu alipenda kukaa baada ya kazi zake.
Pia ametoa shukrani kwa wasanii wenzake ambao walijitahidi katika hali moja au nyingine kuhakikisha filamu hiyo ilikamilika.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ