Next
Previous
Showing posts with label Joshua Nassari. Show all posts

Saturday, June 22, 2013

0

HIKI NDICHO ALICHOKISEMA MREMA JUU YA CHADEMA

Posted in , ,
Nassari akiwa Hospitali

Akizungumza na Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari aliyelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kupigwa na Wanachama wa CCM wakati wa uchaguzi mgodo wa Udiwani Kata ya Makuyuni Wilayani Monduli Mkoani Arusha Juni 16

“Dola haina huruma kupiga mabomu wananchi,kutesa viongozi na kuwafungulia kesi ili wawadhoofishe wasifanye kazi ya kuwatumikia wananchi, au kufanya shuguli za kisiasa”alisema Mrema. Mrema aliongeza kuwa ingawa Serikali inatumia nguvu kama walizotumia kumdhoofisha yeye, lakini ana imani kuwa mbinu hizo kwa CHADEMA hazitafua dafu, kwa chama hiki wamekutana na kisiki cha mpingo,huku akishauri pande zote mbili zitumie busara katika kufanya siasa ili wasije waka hatarisha amani ya nchi.


"Mbinu za Serikali hazifui dafu kwa CHADEMA"-Mrema

Friday, April 26, 2013

0

BAADA YA ZITTO, NASSARI NAYE AANDIKA UJUMBE KUHUSU KUKAMATWA KWA LEMA USIKU WA JANA

Posted in , ,
Nimepata kwa mshtuko na nikakataa kuamini kama ni kweli kuwa polisi wa Arusha wamevamia na kuizingira nyumba ya mbunge mwenzangu wa Arusha, Lema.

Nimelazimika kumpigia simu RPC kuthibitisha na cha ajabu akaniambia ni kweli.

Nimemshauri kama kiongozi mwenzake mwenye dhamana ya kusaidia kuilinda
kweli na haki ili kuleta Amani ya kweli kwenye mkoa wangu wa Arusha. Sidhani kama ni busara kutaka kuvamia nyumbani kwa Raia mwema achilia mbali Kiongozi mkubwa kama mbunge. "Kama watawala wanafanya hivi kwa mti mbichi, itakuwaje kwa mti mkavu" itakuwaje kwa mwananchi wa kawaida anayeishi usa river au unga ltd? Ukifuatilia na kuangalia video ya tukio la uhasibu chuoni arusha, utagundua makosa ya mtawala mkuu wa mkoa, ambaye kimsingi ni mkiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa kuwa sehemu ya sababu ya uvunjifu wa amani, kutokujua hata kusoma saikolojia ya watu.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ