Next
Previous
Showing posts with label Godbless Lema. Show all posts

Monday, April 29, 2013

0

MBUNGE LEMA AACHIWA KWA MDHAMANA (ANGALIA MABANGO YA WAFUASI WA CHADEMA YAKIMKOSOA MKUU WA MKOA)

Posted in ,
mH.akiwa kizimbani

Saturday, April 27, 2013

0

HAYA NDO MAKOSA YANAYOSEMEKANA YAMEMSABABISHA LEMA KUNYIMWA DHAMANA.

Posted in
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhTnquSvuUu9VAZAn7P3zjHxUFVJL8qfiambfudQjzsy23S0tJrICQNNSNHxXaFy6dDgMrPqH1h7Ok1Bapx4Nl6eEkFJ4qqtDTLv_QiOzco9IS_XRWEScYUizjZsh5lOgGveaGd_HZ4CVA/s1600/TAKUKURU2.JPG
Mambo yaliyomfanya Mbunge wa arusha Godbless Lema akamatwe na kunyimwa dhamana jioni hii ni haya yafuatayo baada ya kuongea na Mwanasheria wa Lema wakili Humphrey Mtui

i)Kosa la kwanza ni kuwaambia wanafunzi wa chuo cha uhasibu alipoenda kuwatuliza kuwa ‘dhambi kubwa kuliko zote ni woga ‘.Haki hutafutwa na kupiganiwa ikiwa jambo unalipigania ni la msingi na linafaa kupiganiwa(Worth fighting for)

ii)Kosa la pili ni pale alipotamka kuwa ‘’Tumemtafuta mkuu wa mkoa juu ya Matatizo yenu na mlivyoshuhudia hapa amechukua muda mrefu na kuingia kama vile anaingia kwenye send-off.Hawa ndiyo viongozi wetu ambao hawajali matatizo ya wananchi’’Kwa hiyo huo ni uchochezi

Friday, April 26, 2013

0

BAADA YA ZITTO, NASSARI NAYE AANDIKA UJUMBE KUHUSU KUKAMATWA KWA LEMA USIKU WA JANA

Posted in , ,
Nimepata kwa mshtuko na nikakataa kuamini kama ni kweli kuwa polisi wa Arusha wamevamia na kuizingira nyumba ya mbunge mwenzangu wa Arusha, Lema.

Nimelazimika kumpigia simu RPC kuthibitisha na cha ajabu akaniambia ni kweli.

Nimemshauri kama kiongozi mwenzake mwenye dhamana ya kusaidia kuilinda
kweli na haki ili kuleta Amani ya kweli kwenye mkoa wangu wa Arusha. Sidhani kama ni busara kutaka kuvamia nyumbani kwa Raia mwema achilia mbali Kiongozi mkubwa kama mbunge. "Kama watawala wanafanya hivi kwa mti mbichi, itakuwaje kwa mti mkavu" itakuwaje kwa mwananchi wa kawaida anayeishi usa river au unga ltd? Ukifuatilia na kuangalia video ya tukio la uhasibu chuoni arusha, utagundua makosa ya mtawala mkuu wa mkoa, ambaye kimsingi ni mkiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa kuwa sehemu ya sababu ya uvunjifu wa amani, kutokujua hata kusoma saikolojia ya watu.
0

KAULI YA KWANZA YA ZITTO KABWE KWA FAMILIA YA GODBLESS LEMA BAADA YA KUKAMATWA USIKU WA MANANE

Posted in ,


 Hii inatupa wasiwasi na kubaini kua kuna mchezo nyuma ya pazia unaochezwa na kundi la watu wa chache katika siasa upande wa pili wa upinzani kibaya zaidi ni ma'askari waliovamilia nyumbani kwa mbunge usiku wa jana na kulipua mabomu na wakiwa na silaha kali utadhani wamekwenda kumkamata jambazi au mtu mwenye kesi ya mauaji kitu ambacho sio kizuri. 
#Pole kwa familia ya Godbless Lema.
-Hii  ni  kauli  ya  Zitto  kabwe  Baada  ya mbunge  wa  Arusha  kutiwa  mbaroni  jana  usiku.. 

Wednesday, April 24, 2013

0

VURUGU CHUONI ARUSHA: HABARI KAMILI NA JINSI GARI LA LEMA LILIVYOCHUKULIWA

Posted in ,

Kikosi cha kutuliza ghasia mkoani Arusha kililazimika kutumia Mabomu ya Machozi kuwatuliza wanafunzi waliokuwa wakishinikiza kuandamana baada ya mwanafunzi mwenzao kuuawa kwa kuchomwa kisu na watu wasiojulikana majira ya saa nne usiku wa kuamkia leo. 

Tukio hilo liliamsha hisia za wanafunzi hao na kuwafanya wakusanyike kuelekea kwa mkuu wa mkoa wa Arusha kwa madai kwamba matatizo yao huwa hayafikishwi ipasavyo, hivyo wanataka kuyawasilisha wenyewe.

  Juhudi za uongozi wa chuo kuwatuliza wanafunzi hao zilishindikana, na ilipofika majira ya saa nne asubuhi, Mbunge wa jimbo la Arusha alifika katika eneo hilo kuwasikiliza wanafunzi hao.

  "Tunatoa dakika thelathini mkuu wa mkoa awe ameshafika hapa, kama hajafika ndani ya muda huo, tunaandamana wote, mimi mbele nyie nyuma mpaka ofisini kwake" alisema Mheshimiwa Lema.


Baada ya mkuu wa mkoa kufika eneo la tukio aligoma kuzungumza na wanafunzi hao, akidai kwamba hawezi kuongea mpaka Mh.Lema aondoke, ndipo atapanda kuzungumza na pia alilalamika kwamba hamna kipaza sauti kwa hiyo hawez kupaza sauti yake kuzungumza na watu wasio na nidhamu. 
Maneno hayo yalipandisha hasira ya wanafunzi hao lakini walitulizwa, na kipaza sauti kikaandaliwa katika ukumbi wa chuo maaruf kama "main cafetaria" ili mkuu huyo azungumze.


Wanafunzi walikusanyika eneo hilo kumsikiliza lakini alivyoanza kuongea, wanafunzi walisikika wakimzomea kwa madai kwamba ameonesha dharau.

Wanafunzi walianza kuzomea na kumrushia chupa zaa maji na mawe mkuu wa mkoa na hapo ndipo ilibidi mabomu ya machozi yatumike kuwatuliza wanafunzi wa chuo hicho.

Kwa muda wa masaa mawili imekuwa ikisikika milio ya mabomu chuoni hapo mpaka hali ilipo tulia kabisa.

Kwa sasa hali ni shwari chuoni hapo ila polisi wametapakaa huku na kule wakisema wanamtafuta Mbunge wa jimbo la Arusha kwa madai kuwa ndiye anaye chochea mgomo huo wa wanafunzi.

Mbunge huyo alikimbia kuelekea kusikojulikana na kutelekeza gari yake chuoni hapo, ambayo polisi walilazimika kuivuta kwa "breakdown" car kuelekea kituo cha polisi. kama inavyoonekana katika picha. 

Gari ya Mh.Godbless Lema ikiochukuliwa na polisi kutoka eneo la tukio



Polisi wakichukua gari ya mbunge wa jimbo la Arusa
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ