AVB KULIPA KISASI KWA CHELSEA??? NI KATIKA DABI YA LONDON JUMAMOSI. EPL YARUDI, RATIBA KAMILI.
Posted in Andres Villas Boas, Barclays Premier League, Barclays Premier League Preview, Chelsea, Tottenham Hotspurs
Andre Villas-Boas, Meneja alietimuliwa
kazi na Chelsea baada ya Miezi 9 tu mwanzoni mwa Mwaka huu, Jumamosi
atapata nafasi safi ya kulipa kisasi wakati Timu yake anayoiongoza sasa
Tottenham itakapoikaribisha Chelsea Uwanjani White Hart Lane katika
Mechi ya Ligi Kuu England ambayo ni Dabi ya Jiji la London.
Chelsea watatinga White Hart Lane wakiwa
ndio vinara wa Ligi wakiwa na Pointi 19 baada ya kushinda Mechi 6 na
sare 1 na Tottenham wamepanda hadi nafasi ya 5 baada ya kuchinda Mechi
zao 4 za mwisho ukiwemo ule ushindi wao murua huko Old Trafford
walipoifunga Manchester United bao 3-2 huo ukiwa ushindi wao wa kwanza
Uwanjani hapo katika Miaka 23.
Msimu uliopita, Chelsea walimaliza Ligi
wakiwa nafasi ya 6, nafasi mbili nyuma ya Tottenham lakini Chelsea
wakaichukua nafasi ya Tottenham kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI kwa vile
Chelsea ndio Mabingwa watetezi wa Mashindano hayo na wao Tottenham
kutupwa kucheza EUROPA LIGI.
Baada ya kutimuliwa Andre Villas-Boas,
mwenye Miaka 34, nafasi yake huko Chelsea ikachukuliwa na aliekuwa
Msaidizi wake, Roberto Di Matteo, ambae ndie aliiongoza Chelsea kutwaa
Ubingwa wa Ulaya walipoitoa Bayern Munich kwa matuta Mwezi Mei kwenye
Fainali huko Munich, Germany.

Ikiwa Tottenham watamudu kuisimamisha
Chelsea hilo litatoa mwanya kwa Timu zinazoifukuza Chelsea ambazo ni
Manchester United, Mabingwa Manchester City na Everton.
Man United, ambao wako nafasi ya pili na
wenye Pointi 15, wapo kwao Old Trafford kucheza na Stoke City, Man
City, ambao pia wana Pointi 15, wapo ugenini kucheza na WBA ambao wako
nafasi ya 6, na Everton, walio nafasi ya 4, wanacheza na Timu ya mkiani
Queens Park Rangers.
Wachezaji toka Mechi za Kimataifa
Klabu nyingi za Ligi Kuu England
zitakuwa zikisubiri kurudi kwa Wachezaji wao kutoka kuzichezea Nchi zao
huku wakiwa na wasiwasi kama wako fiti lakini Chelsea watacheza na Spurs
bila ya majeruhi Frank Lampard na Ryan Bertrand.
Manchester United, ambao wana listi
ndefu ya majeruhi, wanaweza kupata ahueni baada ya Ashley Young na Chris
Smalling kupona na kurejea mazoezini tangu Wiki iliyopita.
Man City wataenda huko Hawthorns kucheza
na WBA bila ya David Villa ambae aliumia hivi juzi akiichezea Nchi yake
Spain na pia Kiungo Jack Rodwell lakini machachari wao Mario Balotelli
amepona na juzi alifunga bao wakati Nchi yake Italy ilipoichapa Denmark
bao 3-1.
Arsenal, ambao wameteleza hadi nafasi ya
7 wakiwa na Pointi 12, watasafiri kwenda kucheza na Norwich City ambao
Msimu huu hawajashinda hata Mechi moja ya Ligi.
Arsenal watacheza bila ya Theo Walcott
alieumizwa kifua kwenye Mechi ya Nchi yake England ilipocheza na San
Marino Ijumaa iliyopita lakini Straika wao Olivier Giroud anaweza
kucheza baada ya kuifungia Arsenal bao lake la kwanza kwenye Ligi
Arsenal ilipoicharaza West Ham 3-1 katika Mechi iliyopita na pia kufunga
bao muhimu kwa Nchi yake France ilipotoka 1-1 na Mabingwa wa Dunia
Spain katika Mechi ya Kombe la Dunia juzi Jumanne.
RATIBA NA MAREFA wa MECHI za WIKIENDI:
Jumamosi Oktoba 20
Tottenham Hotspur v Chelsea
Refa: M Dean
Wasaidizi: S Ledger, J Brooks
Refa wa Akiba: L Mason
Fulham v Aston Villa
Refa: C Foy
Wasaidizi: M McDonough, D C Richards
Refa wa Akiba: I Williamson
Liverpool v Reading
Refa: R East
Wasaidizi: A Garratt, R West
Refa wa Akiba: K Friend
Manchester United v Stoke City
Refa: A Taylor
Wasaidizi: D Cann, S Long
Refa wa Akiba: M Halsey
Swansea City v Wigan Athletic
Refa: M Jones
Wasaidizi: H Lennard, A Halliday
Refa wa Akiba: K A Woolmer
West Bromwich Albion v Manchester City
Refa: M Clattenburg
Wasaidizi: S Beck, S Child
Refa wa Akiba: C Pawson
West Ham United v Southampton
Refa: N Swarbrick
Wasaidizi: J Collin, L Betts
Refa wa Akiba: J Moss
Norwich City v Arsenal
Refa: L Probert
Wasaidizi: R Ganfield, D Bryan
Refa wa Akiba: A Marriner
Jumapili Oktoba 21
Sunderland v Newcastle United
Refa: M Atkinson
Wasaidizi: M Mullarkey, S Burt
Refa wa Akiba: A Taylor
Queens Park Rangers v Everton
Refa: J Moss
Wasaidizi: J Flynn, C Breakspear
Refa wa Akiba: P. Dowd
0 Maoni/comments: