FALL OF SUPER POWERS IN SOCCER KATIKA UEFA CL
Posted in Arsenal, Real Madrid, UEFA Champions League
MATOKEO:
FC Porto 3 FC Dynamo Kyiv 2
GNK Dinamo 0 Paris SaintvGermain 2
Arsenal FC 0 FC Schalke 2
Montpellier 1 Olympiacos 2
FC Zenit St. Petersburg 1 RSC Anderlecht 0
Málaga 1 AC Milan 0
AFC Ajax 3 Manchester City FC 1
Borussia Dortmund 2 Real Madrid 1
++++++++++++++++++++++++++
Katika MECHI DEI 3 ya UEFA CHAMPIONZ
LIGI, Mabingwa wa England, Manchester City walipata kipondo cha 3-1 toka
kwa Ajax Amsterdam Mjini Amsterdam na vile vile hali hiyo kuwakuta
wenzao Arsenal, wakiwa nyumbani, walichapwa 2-0 na Schalke ya Germany
wakati huko Germany Mabingwa wa Nchi hiyo Borussia Dortmund
waliwakung’uta Real Madrid bao 2-1.
AJAX 3 MAN CITY 1
Yale mategemeo ya Manchester City
kusonga mbele kuingia Raundi ya Mtoano ya UEFA CHAMPIONZ LIGI yamepata
pigo kubwa baada ya kucharazwa Bao 3-1 na Ajax ndani ya Amsterdam ArenA
katika Mechi ya Kundi F.
Huku Ajax wakitawala, Samir Nasri aliipa
Man City bao la kuongoza lakini Siem de Jong akaisawazishia Ajax kabla
haftaimu na baadae Kipindi cha Pili Niklas Moisander akapiga bao la pili
kwa Ajax na Christian Eriksen kuipigia bao la 3.
++++++++++++++++++++++++++
KUNDI D-MSIMAMO
[Kila Timu imecheza Mechi 3]
1 Borussia Dortmund Pointi 7
2 Real Madrid 6
3 Ajax 3
4 Manchester City 1
++++++++++++++++++++++++++
Matokeo haya yamewaacha Man City wakiwa
mkiani mwa Kundi lao wakiwa na Pointi 1 tu kwa Mechi 3 na Mechi
inayofuata ni ya wao kuwa Wenyeji wa Ajax hapo Novemba 6 na pia kuwa
mwenyeji wa Real Madrid Novemba 21 na kumalizia ugenini na Borussia
Dortmund.
VIKOSI:
Ajax: Vermeer, Van Rhijn, Alderweireld, Moisander, Blind, Schone, Poulsen, Eriksen, Sana, De Jong, Babel
Akiba: Cillessen, Enoh, Sulejmani, Boerrigter, Veltman, Dijks, Fischer.
Man City: Hart, Richards, Kompany, Lescott, Clichy, Toure, Barry, Milner, Aguero, Nasri, Dzeko
Akiba: Pantilimon, Sinclair, Kolarov, Tevez, Nastasic, Balotelli, Evans.
Refa: Svein Oddvar Moen (Norway)
ARSENAL 0 SCHALKE 2
Schalke wamewastua Arsenal wakiwa kwao
Emirates kwa kuwachapa bao 2-0 huku bao zote zikija katika Dakika 15 za
mwisho kupitia Klaas Jan-Huntelaar na Ibrahim Afellay na kuifanya Klabu
hiyo ya Bundesliga Germany itwae uongozi wa Kundi B.
Huku Arsene Wenger akikaa kwenye Jukwaa
la Watazamaji akitumikia Kifungo cha Mechi ya mwisho alichoshushiwa na
UEFA, benchi la Arsenal liliongozwa na Msaidizi wake Steve Bould lakini
Timu yao ilonyesha udhaifu kwenye Difensi hasa upande wa kushoto ambako
Andre Santos alionekana ni uchochoro.
++++++++++++++++++++++++++
KUNDI B-MSIMAMO
[Kila Timu imecheza Mechi 3]
1 Schalke Pointi 7
2 Arsenal 6
3 Olympiacos 3
4 Montpellier 1
++++++++++++++++++++++++++
Hata hivyo, Arsenal wana nafasi kubwa ya
kufuzu kuingia Raundi ya Mtoano baada ya kushinda Mechi zao mbili za
kwanza dhidi ya Montpellier na Olympiakos.
VIKOSI:
Arsenal: Mannone, Jenkinson, Mertesacker, Vermaelen, Andre Santos, Ramsey, Coquelin, Arteta, Podolski, Cazorla, Gervinho
Akiba: Shea, Koscielny, Giroud, Djourou, Arshavin, Chamakh, Gnabry.
Schalke 04: Unnerstall, Uchida, Howedes, Matip, Fuchs, Hoger, Neustadter, Holtby, Afellay, Farfan, Huntelaar
Akiba: Hildebrand, Marica, Jones, Barnetta, Moritz, Draxler, Kolasinac.
Refa: Jonas Eriksson (Sweden)
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumanne Novemba 6
FC Dynamo Kyiv v FC Porto
Paris SaintvGermain FC v GNK Dinamo
FC Schalke 04 v Arsenal FC
Olympiacos FC v Montpellier Hérault SC
RSC Anderlecht v FC Zenit St. Petersburg
AC Milan v Málaga CF
Manchester City FC v AFC Ajax
Real Madrid CF v Borussia Dortmund
Jumatano Novemba 7
Juventus v FC Nordsjælland
Chelsea FC v FC Shakhtar Donetsk
Valencia CF v FC BATE Borisov
FC Bayern München v LOSC Lille
SL Benfica v FC Spartak Moskva
Celtic FC v FC Barcelona
CFR 1907 Cluj v Galatasaray A.S.
SC Braga v Manchester United FC
0 Maoni/comments: