Thursday, April 4, 2013

0

MASTAA WAIGIZAJI MAARUFU WA AFRIKA KUTUA BONGO KATIKA UZINDUZI WA FILAMU YA MAREHEMU KANUMBA

Posted in ,


FILAMU ya mwisho kuigizwa na Steven Kanumba Kanumba The Great iliyopewa jina la Love And Power itazinduliwa kwa aina yake baada ya wasanii kutoka Afrika Magharibi kualikwa.

Mratibu wa tukio hilo, Mosses Mwanyilu, amesema kuwa msanii huyo aliyefariki dunia mwaka jana, alikuwa kipenzi cha wapenda filamu Bongo na nje ya mipaka ya Bongo, hivyo kwa kuliona hilo wameamua kualika wasanii mbalimbali. 

Tunatarajia kufanya tukio la kipekee kabisa katika uzinduzi wa filamu ya Love And Power ya marehemu Kanumba kwa sababu ni mtu wa watu. Kwa hiyo kutokana na habari ambazo tumekuwa tukizipata kutoka sehemu mbalimbali, kuna watu ambao bado hawaamini kuwa Kanumba amefariki, katika kumuenzi tumekusudia kuitendea haki filamu yake, anasema Mwanyilu. 

Filamu hiyo inadaiwa kutabiri kifo cha Kanumba. Katika filamu hiyo pia wapo wasanii kama Irene Paul, Patcho Mwamba, marehemu Sharomilionea na wasanii wengine wengi.

0 Maoni/comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ