Next
Previous
Showing posts with label Olasiti. Show all posts

Friday, May 10, 2013

0

HIVI NDIVYO IBADA YA KUWAAGA MAREHEMU WALIOKUFA KATIKA TUKIO LA BOMU KANISANI ARUSHA

Posted in

NI SIMANZI,VILIO NA MAJONZI MAZISHI YA WALIOKUFA KWA BOMU ARUSHA,PICHA HIZI HAPA




Mapadri wa kanisa katoliki wakiwa wamebeba jeneza  lenyenye mwili wa mmoja wa waliokufa katika tukio la kutupwa kwa bomu la mkonokatika kanisa la Olasiti Arusha may 5, 2013. mazishi yaliyofanyika leo 




 Mapadri wa kanisa katoliki wakiwa wamebeba jeneza  lenyenye mwili wa mmoja wa waliokufa katika tukio la kutupwa kwa bomu la mkonokatika kanisa la Olasiti Arusha may 5, 2013.

Thursday, May 9, 2013

0

ALIYEMKAMATA MLIPUA BOMU KANISANI ANENA MAZITO | YASOME HAPA

Posted in

ALIYEMKIMBIZA hadi kumkamata mtu anayedaiwa kuhusika na kulipua bomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, jijini Arusha Jumapili iliyopita na kuua watu 3 na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa ameibuka.

Kijana aliyemkimbiza hadi kumkamata mtu anayedaiwa kuhusika na kulipua bomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, jijini Arusha akiwaelezea wananchi ilivyokuwa.

Wednesday, May 8, 2013

0

HIZI NDO PICHA ZA RAISI KIKWETE AKIHANI MISIBA YA WALIOKUFA KATIKA MLIPUKO WA BOMU KANISA LA OLASITI

Posted in ,

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Bw. Joachim Assey (aliyekaa kushoto kwake) wakati akihani msiba wa msichana Patricia Joachim Assey (10) aliyefariki kutokana na mlipuko wa bomu jumapili iliyopita katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti jijini Arusha Mei 7, 2013.

Monday, May 6, 2013

0

FREEMAN MBOWE ATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI TUKIO LA MLIPUKO WA BOMU KANISANI OLASITI

Posted in

Mbowe atoa pole na rambirambi tukio la mlipuko wa bomu Arusha

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ametuma salaam za pole na rambirambi kwa waumini wa Kanisa Katoliki nchini na Watanzania wote kwa ujumla kutokana na mlipuko uliotokea katika Kanisa la Olasiti, Jijini Arusha, uliosababisha vifo na majeruhi, huku wengine wakipatwa na mshtuko mkubwa kutokana na tukio hilo.

Mwenyekiti Mbowe ametoa salaam hizo alipozungumza kwa njia ya simu na Katibu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Padri Antony Makundi, jioni ya Jumapili, baada ya kupata taarifa za tukio la mlipuko huo unaodhaniwa kuwa ni bomu.

"Tumepokea habari za tukio la mlipuko uliotokea leo (jana) katika Kanisa la Olasiti huko Arusha kwa mshtuko na masikitiko makubwa. Kupitia kwako tunapenda kutoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na waumini wa Kanisa la Olasiti waliopatwa na msiba, waliojeruhiwa na wengine waliopatwa na mshtuko mkubwa kutokana na tukio hilo lisilokuwa la kawaida.
0

VIDEO YA MLIPUKO WA KANISANI OLASITI

Posted in

Sunday, May 5, 2013

0

MLIPUKO WA OLASITI: TAARIFA ZA VIFO NA MAJERUHI

Posted in
Mmoja ya majeruhi

Eneo La Kanisa hilo
Idadi ya watu 3 au zaidi wamefariki dunia na wengine zaidi ya 50 wamejeruhiwa vibaya katika shambulio la kigaidi iliyotokea leo asubuhi katika Kanisa la Katholiki Parokia ya Ola City Jijini Arusha.
Majeruhi wa tukio hilo wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Ausha, Mount Meru
kwa matibabu zaidi, taarifa zilizo hivi sasa zinadai kwamba mtu mmoja anashikiriwa na Jeshi la Polisi kuhusiana na tukio hilo.
Shambulio hilo la kigaidi limeacha maswali mengi bila majibu huku jeshi la Polisi Arusha likiendelea kumhoji mtuhumiwa huyo, shambulio hilo lilifanyika wakati wa uzinduzi wa kanisa hilo.
PICHA ZAIDI>>>
0

AMANI INAENDA WAPI WATANZANIA??? | TAARIFA KUHUSU MLIPUKO WA BOMU KANISANI OLASITI, ARUSHA

Posted in
UPDATES::::

Mbunge Lema amefika eneo la tukio, na baada ya yeye kufika wananchi wanaonekana kutabasamu.
Mbunge anasema: Poleni kwa yaliowakuta, Hakuna mwizi anaweza kurusha bomu ila uchunguzi ufanywe, na anasema anadhani polisi watamkamata haraka kama walivyomkamata yeye.

RPC asema, Mtu alitokea eneo la nyuma la kanisa akiwa amevalia kanzu na kulirusha bomu hilo..
-Na mejeruhi wapo zaidi ya 30, huku wakiwa na majeraha tofauti na wamepelekwa hospitali.
-Kuna majina yametajwa, ila hawayaweki hadharani kwa sababu za kiusalama.

MKUU WA MKOA ARUSHA ATOA POLE ZAKE huku akisema wameitwa wataalam mbalimbali ambao watafanya uchunguzi huo, huku pia akiomba utulivu na amani iwepo kipindi hichi cha upelelezi.
------------------------------------------------------------------------------

Kanisa katoliki la Mt. Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti Arusha ambalo leo hii lilikuwa linapandishwa hadhi na kuwa Parokia limelipuliwa na  kitu  kinachosemekana  kuwa  ni  bomu, watu wengi wamejeruhiwa  na  mtu  mmoja  inasemekana  amefariki  dunia.

Tukio  hilo  limetokea  wakati  Misa ikiwa ndio inaanza .Ilikuwa ni saa 5 kamili...Kabla Askofu hajaanzisha sala , mlipuko mkubwa  ulitokea  ndani  ya  kanisa  hilo. 

Kanisa hilo lilikua likizinduliwa na Askofu Josephat Lobulu akiwa na balozi wa Vatican Francisco Padilla , Tanzania.

Kuna taarifa ambazo zinasema alionekana mtu akilirusha na kisha kukimbia ambapo alisema kijana mdogo aliyekuepo eneo hilo, na baadae tena ukaskika mlipuko mwingine ambao haukua wa nguvu kama ule wa mwanzo.

CHANZO CHA BOMU HILO INASEMEKANA KUWA KUNA  GARI AINA YA HIACE ILIFIKA KANISANI HAPO NA KUSIMAMA BAADAE AKASHUKA MTU ALIYEKUWA AMEVALIA VAZI MITHILI YA KANZU NA KURUSHA BOMU HILO, BALOZI WA PAPA NCHINI NDIYE ALIYEKUWA MGENI RASMI KATIKA UZINDUZI WA KANISA HILO JIPYA JIJINI ARUSHA NA AMENUSURIKA KATIKA BOMU HILO ILA WATU WENGI WAMEJERUHIWA ZAIDI . 

ENDELEA KUWA NASI HAPAHAPA KWA TAARIFA ZAIDI

Mda si mrefu Askofu na mgeni wake wamesindikizwa kwa usalama mkubwa kutoka eneo la tukio.

AMANI inazidi toweka siku zinavyozidi kwenda, Watanzania tunaeleka wapi??? Mhm, Nadhani watu wa usalama watafanya uchunguzi vyema.

#Na Straton Mo Panish : Maoni Juu Ya Mlipuko Parokiani Arusha

LENGO LAO NI MOJA TU,KUHAKIKISHA WANAIGAWANYA TANZANIA KIDINI..MIMI NAAMINI HAKUNA UPANDE HATA MMOJA KATI YA WAISLAMU AMA WAKRISTO UNAOHUSIKA NA MATUKIO KAMA HAYA YA KISHETWANI..NI WATU FLANI TU WALIOPANDIKIZWA KUICHAFUA AMANI YA TZ KWA KIVULI CHA DINI,NA TUSIPOKUA MAKINI WANAELEKEA KUFANIKIWA KATIKA HILI..TUMEKUA WEPESI SANA KUAMINI MANENO MANENO YANAYOZUSHWA NA TUMEKUA WAGUMU MNO KUTUMIA AKILI NA UTASHI TULIOPEWA NA MWENYEZI MUNGU KUCHAMBUA NA KUTAMBUA MAMBO...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Msimamo Ligi Kuu TZ